Tetesi: TCRA Wanaomiliki laini (simkadi) zaidi ya moja katika mtandao mmoja kupokonywa ifikapo June 2020

Tetesi: TCRA Wanaomiliki laini (simkadi) zaidi ya moja katika mtandao mmoja kupokonywa ifikapo June 2020

Nashindwa kuelewa walio tunga hizi sheria walikuwa wamelewa ? Au walidownload file Google's la hizi sheria bila kufanya editing zikapitishwa ili zitumike.

Maana bunge limejaa wasomi na ndo moja ya kazi yao ya kutunga miswada kuwa sheria sasa hii ya laini 1 sijui ilipita vip.

Itafika kipindi kusajili laini unatuma maombi na vyeti juu kama vile tunaomba kazi, maana hii ya vidole hawaiamini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu bora umemwambie wewe, Watu wamekuwa walalamishi mpaka inakera, anyway wengine wanajitetea kwa uhalifu wao waendeleee na Simu ya Mke na Mchepuko kivyake. Kwa wale Wafanyabiashara Rasmi upo utaratibu wa Simu za Kibiashara unapata mpaaka Laini 50 ktk mtandao mmoja. Sasa kama biashara yako hulipi kodi kazi kwako.
Mwanaume unamiliki laini za Simu kila mtandao kwani wewe Dalaliiii! Hizi dalili mbaya
Hapo kwa hiyo post unajiona booooonge la mjanjaaaa! Kumbe hovyo tu mavi kinuka
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Mmi nina sim card mbili moja ni ya biashara ipo kwenye social media na vipepereshi hii naizima ikifika saa kumi na mbili jion pia juma pili na sikukuu siiwashi na line nyingine ndio matumiz yangu binafsi hii sheria ni ya ki whack balaa

Nenda kaisajiri June 2020 sio mbali....
 
Hawa TCRA wamekua wasanii wasanii tu mimi mpaka leo sijasajili na bado nipo hewani kama kawa (hawajafunga) dogo walimfungia line zake baada ya muda akaziweka hewani zinapiga kazi kama kawaida (kuweka vocha kupiga simu na kujibu msg vyote vinafanyika)

kimsingi naweza kusema ni wazee wa kuzua taharuki tu ili wapate kiki hamna kazi wanafanya kama tu wameshidwa kuwathibiti wale wazee wa "ile hela tuma kwenye namba hii" sasa wataweza nini?

Sent using Jamii Forums mobile app

Cha msingi hiyo line isihusishwe na matukio ya uhalifu.... Ya Idris Sultan umeyasikia?!.
 
Nashindwa kuelewa walio tunga hizi sheria walikuwa wamelewa ? Au walidownload file Google's la hizi sheria bila kufanya editing zikapitishwa ili zitumike.

Maana bunge limejaa wasomi na ndo moja ya kazi yao ya kutunga miswada kuwa sheria sasa hii ya laini 1 sijui ilipita vip.

Itafika kipindi kusajili laini unatuma maombi na vyeti juu kama vile tunaomba kazi, maana hii ya vidole hawaiamini

Sent using Jamii Forums mobile app
yaani tutapata tabu
 
Mimi nashauri tcra ingejikita kuhakikisha hizi huduma za mawasiliano zinaboreshwa,,huduma ziwe Bei nafuu kwa raia,I wafanye raia kuwa na maisha Bora na wafurahie maisha,,Hilo ndo lengo la kuishi Hapa duniani,
Sio unapata kacheo,unaanza kuleta sheria ngumu ngumu zinazofanya maisha yazidi kuwa complicated.
Hakunaga mtu Hapa duniani ataishi na cheo milele.make life better at least for the sake of your siblings
 
Halotel wameshaanza kutukumbusha.Nimetumiwa hii sms.

Dear customer. To ensure communication Please dial *106# and select 3 to choose main number for voice. Thank you!
 
Mimi nashauri tcra ingejikita kuhakikisha hizi huduma za mawasiliano zinaboreshwa,,huduma ziwe Bei nafuu kwa raia,I wafanye raia kuwa na maisha Bora na wafurahie maisha,,Hilo ndo lengo la kuishi Hapa duniani,
Sio unapata kacheo,unaanza kuleta sheria ngumu ngumu zinazofanya maisha yazidi kuwa complicated.
Hakunaga mtu Hapa duniani ataishi na cheo milele.make life better at least for the sake of your siblings
umeongea kwa hisia Sana! good advice!
binadam wengi wakipata wengine huwaona Kama punda tu
 
Unaandika tetesi wakati kanuni ziko wazi tangia mwezi wa 2 tarehe 7! Na usipoteshe eti watapokonywa ila sema utapaswa kuchagua ni lain hipi uitumie na nyingine uziache na pia unaruhusiwa kuwa na lain zaid ya moja ndani ya mtandao mmoja isipokuwa lazima uireport utaitumia kwa matumizi ya modem tu na si vinginevyo.
Wewe boya kabisa kwani wewe ni msemaji wao? Hatuhitaji majibu kutoka kwako wewe ndo mpotishaji usumbufu tupatao kwa TCRA tunaujua sisi wewe kama unatumia simu ya shangazi yako kaa pembeni
 
Awamu hii ni usumbufu mwanzo mwisho kuna NIDA,TCRA,na uchafu kibao.
 
Mabadiliko ya Mara kwa Mara yanayofanywa na regulators wa jambo lolote yanaonyesha hali ya kutojiamini....imagine hivi punde tu RAIA walikuwa wanahangaika kusajili laini kwa alama za vidole.....regulator ameona mini kiasi kwamba hata miaka miwili haijaisha usumbufu unaanza.Kwa nini hilo halikuwekwa wazi wakati wa usajili ili kuwapunguzia wananchi usumbufu?
Kama hofu ni ihalifu utaratibu ule haukukidhi haja ya kuwakamata wahalifu.Mimi binafsi naona kuwa ikiwa MTU anamiliki laini zaidi ya moja mtandao mmoja na hazitumii kihalifu aachwe tu.
NB.Afrika kusini ya jangwa LA sahara kuendelea itachukua muda!!!!!
 
Kusema ukweli kwa hili TCRA mnatuchanganya! Inaonesha hamjajipanga!
Usumbufu umekuwa mwingi mno!
  • Tulisajili kwa majina mara ya kwanza, mkasema ni batili mkasema zoezi lirudiwe,
  • Tukarudia tukasajili kwa vitambulisho vya kura, napo mkasema ni batili
  • Mkasema tukamilishe usajili kwa kupiga picha mwaka juzi tukafanya hivyo lakini bado ikawa ni batili;
  • Mwaka jana mkadai tusajili kwa vitambulisho vya NIDA kwa alama za vidole, tumefanya hivyo bado mnaona hiyo haitoshi!
  • Mnataka mwaka huu wenye laini zaidi ya moja kwenye mtandao mmoja muwazimie simu zao walizozisajili
TCRA kwa hili sasa sio ungwana kabisa! Naona kama ni usumbufu mnaofanya wala siyo weledi!

Kuna majibu mepesi eti; kwa wamiliki wanaohitaji laini zaidi ya moja watatakiwa kusaini fom maaalum;
Swali!
  1. Kama electronic data za vidole hamziamini mtu amiliki laini apendavyo, je hizo fomu maalum ndo zitaaminika?
  2. Hizo fomu zinawafikiaje wananchi huko vijijini?
  3. Kuna wafanya biashara ambao wana office zaidi ya moja ambazo zinahitaji namba za simu zaidi ya moja hilo hamjalifikilia?
TCRA mtatukosea sana
Huemda mlengwa hajapatikana.
 
Sasa tukimiliki laini zaidi ya moja kuna madhara gani? labda waje watueleweshe kama kuna sababu yoyote ya msingi. vinginevyo ni kuipunguzia mapato nchi kwa huo muda watakaozima.
 
Back
Top Bottom