TCRA watakagua simu za Watanzania wote kuwajua wanaotumia VPN?

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Nimeona katazo la Tcra kuzuia matumizi ya Vpn nakusema kuwa kuna faini ya mil 5. Sasa kwa sababu karibu kila Mtanzania mwenye smart foni amedownload VPN na anaitumia kuangalia mambo yake binafsi ya kifaragha .

Je, TCRA itawag'amua vipi watu wakiwa na simu zao mkononi.

Msaada wa kitalaamu
 
TCRA ni wafia dini siku hizi?
 
Wangese,huko ni kuingilia faragha za watu wanajua kazi za VPN ni nini kwani? wengine tunazitumia kupata vitu vya maana sio wanavyovifikiria wao vichwani mwao. Nikiwambia wanipe ninachokipata kwa VPN wakiweza natoa vpn kwa simu yangu.
 
Wanajua
IMEI NUMBER YAKO WANAYO.
Ukiwasha tu.wanaisoma.
Unashangaa upo kitandani kwako bizeee mlango unagongwa[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Waka kague kwanza ya mama yao kwani nae aaangaliagi pilau
 
Mikwara tu hii. Hawa TCRA wameshindwa kufanya kazi zao za msingi kama kuwakamata matapeli ya mitandaoni.

Hawana uwezo wa kumkamata mtumiqji wa VPN. Ndiyo maana Kigogo 2014 ameisumbua serikali mpk leo kwasabb ni mtumiqji mzuri wa VPN.

VPN inabadili location na kumfanya mtu wa Manzese aonekane kama vile yuko New York.
 
Je Tcra itawag'amua vipi watu wakiwa na simu zao mkononi.

Wasikutishe, wangekuwa na teknolojia hiyo wasingechimba biti...

Ukisoma hicho walichokiandika, maelezo yote yamewalenga wenye kujificha nyuma ya VPN na kuweka maudhui mtandaoni yaliyo kinyume na sheria ya matumizi ya mitandao...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…