Pre GE2025 TCRA yailima Barua Jambo TV kwa kurusha taarifa za Tundu Lissu na Kabendera kuhusu shutuma kwa Tigo na Vodacom

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Tusubiri na sarakasi za uchaguzi mkuu, demo si November?
 

Tuhuma kwamba jambo tv hawakuwapa wahusika nafasi ya kujieleza hazina msingi wa kutosha.

Hotuba ya Mheshimiwa Tundu Lissu na Bw. Erick Kabendera: Kama vyombo vya habari, wana wajibu wa kuripoti mambo yenye maslahi kwa umma, na hotuba hizi zilikuwa na umuhimu wa umma kutokana na uzito wa madai yaliyotolewa.

Binafsi nadhani wahusika waliotajwa ama kuhusishwa na tuhuma hizo na wao wawaite waandishi hao na watoe ufafanuzi wao ili mizani ibalance sasa.
 
Lakini fikiria pia upande wa pili kupewa nafasi ya kujitetea kabla hujatoa tuhuma la sivyo unaweza kuharibu image ya upande wa pili kwa tuhuma ya uongo.
 
Mkono wa mabeberu yanapoungana na dola gandamizi kuwaangamiza raia

03 October 2024
Dar es Salaam, Tanzania

Mwenyekiti wa makampuni ya Vodacom Afrika atua Tanzania

Mwenyekiti wa makampuni ya Vodacom Afrika Bw. Sakumzi Macozoma akiwa katika ziara ya kikazi akutana na mabosi wa Vodacom Tanzania na pia akutana na viongozi wa serikali ya Tanzania

Vodacom Tanzania PLC we are honored to welcome and host Shameel Joosub, Vodacom Group CEO, and the Vodacom Group Board, led by the Chairman Sakumzi Macozoma

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania akimpokea mwenyekiti wa makampuni ya Vodacom Afrika Group, na pamoja wafanya mazungumzo Kushirikisha Serikali katika Mabadiliko ya Kidijitali​

Vodacom Tanzania ilikutana na Waziri wa TEHAMA wa Tanzania kujadili ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi na kuendeleza mageuzi ya kidijitali nchini.


Katika ziara hiyo ujumbe wa Vodacom ulikutana na Mhe. Jerry Silaa, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia wa Tanzania. Majadiliano yalihusu mada kuu, ikijumuisha jukumu muhimu la ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) katika kuendesha maendeleo ya taifa, na njia ambazo Vodacom inaweza kuunga mkono dira ya serikali ya mabadiliko ya kidijitali. Mkutano huo ulisisitiza umakini wa Vodacom katika ushirikiano ili kuharakisha utumiaji wa teknolojia, na hivyo kusaidia kujenga mustakabali wenye uhusiano na ubunifu zaidi kwa Tanzania.

Vodacom Tanzania imesisitiza kujitolea kwake kufanya kazi kwa karibu na serikali ili kuleta maendeleo na kuwezesha kila Mtanzania kupitia teknolojia. Kampuni inalenga kupanua ufikiaji wa kidijitali, kuziba mapengo ya muunganisho, na kukuza siku zijazo ambapo teknolojia inasaidia ukuaji wa uchumi na maendeleo ya kitaifa.
 
Makampuni ya kibeberu ya kimataifa, yanapochagiza kubinywa haki
Lobby groups with opaque funding who are determined to undermine facts about the climate emergency and other established science.

Authoritarian states with no regard for the freedom of the press.

03 October 2024
Ikulu
Dar es Salaam, Tanzania


Bw. Sakumzi Macozoma pamoja na ujumbe wake vigogo wa Vodacom walipifika Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dr. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kundi la Makampuni ya Vodacom Bw. Sakumzi Macozoma pamoja na ujumbe wake mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
 
Fikiria kama ungekuwa umetuhumiwa wewe na usipewe nafasi ya kusikilizwa kabla ya tuhumu kutolewa kwa public ungejisikiaje?

Makampuni ya Vodacom Afrika, TIGO / MILLICOM yana rasilimali watu wafanyakazi, fedha kibao, kuajiri wanasheria kuwashauri na hatimaye kuweza kuita media kibao ikiwemo Jambo TV wakatoa ufafanuzi kuhusu sakata hili, tujiulize wanaogopa nini kuitisha press conference?

Hili la kampuni kubwa ya kimataifa kutaka kutishia raia mmoja mmoja halikubaliki, ni ubeberu mkongwe kujificha nyuma ya TCRA wakati kuna jukwaa la kuja wao Vodacom kuelezea walichowafanyia Tundu Lissu na Eric Kabendera waliotumwa na nani au ni mfanyakazi ndani ya VODACOM au TIGO / MILLICOM alitumika n.k n.k

Umma uweze kufahamu yanayoendelea nyuma ya pazia, ili wateja wawe na imani ya kuwa wapo salama.
 
Kwahiyo hawatakiwi kuripoti? Mana hapo aliyesema hayo maneno si Lissu na Kabendera? Hao waliotoa taarifa wamekosea nini? Naomba elimu tafadhali
Ndio ubaya wa kua na sheria uchwara zinazobinya waandishi na wapashaji habari
 
Fikiria kama ungekuwa umetuhumiwa wewe na usipewe nafasi ya kusikilizwa kabla ya tuhumu kutolewa kwa public ungejisikiaje?
Wewe mjinga unatetea kitu gani, nini ambacho hukijui kuhusu Tigo kuuza location za Lissu?

Kwanza kiherehere cha TCRA kimetoka wapi? Maana Tigo hawakuwahi kukanusha zaidi walisema hayo ni ya Uongozi wao uliopita, Viongozi wapya akina Rostam hawahusiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…