Pre GE2025 TCRA yailima Barua Jambo TV kwa kurusha taarifa za Tundu Lissu na Kabendera kuhusu shutuma kwa Tigo na Vodacom

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
View attachment 3121252
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia Kamati yake ya Maudhui imefungua mashitaka dhidi ya Jambo Online TV, ikidai kuwa kituo hicho cha habari kimekiuka Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kuhusu Maudhui ya Mtandaoni za mwaka 2020, zilizofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

Hatua hii inatokana na matangazo ya maudhui yaliyotajwa kuwa natuhuma nzito yaliyotolewa na kituo hicho bila kuwapa nafasi wahusika kutoa ufafanuzi wao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa tarehe 9 Oktoba 2024, Mamlaka ya Mawasiliano kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, inadai kuwa tarehe 1 Oktoba 2024, Jambo Online TV inadaiwa kurusha hotuba ya Mheshimiwa Tundu Lissu, ambayo iliibua tuhuma dhidi ya viongozi wa serikali na kampuni ya Tigo.

Hotuba hiyo, ambayo ilichapishwa mtandaoni, iliweka wazi madai mazito yaliyohusisha kampuni ya mawasiliano ya simu ya Tigo, ambapo Tundu Lissu alieleza kuwa Tigo ilihusika katika njama za kumfuatilia kabla ya kushambuliwa.

Katika hotuba yake, Lissu alinukuliwa akisema, “Tigo walikuwa wakinifuatilia sio kwa njia ya kawaida tu, bali walitumia wachunguzi wa ndani kunifanyia ufuatiliaji wa kina. Mtu mmoja aliyekuwa mfanyakazi wa Metropolitan Police ya London ndiye alikuwa mchunguzi wao wa ndani, akichunguza matendo ya wafanyakazi wa Tigo. Siku tano baada ya mimi kushambuliwa, mchunguzi huyo alisikika akisema kuwa walikuwa wanajua taarifa zangu zote, hata mahali nilipokuwa.”

TCRA imeendelea kudai kuwa, siku iliyofuata tarehe 2 Oktoba 2024, Jambo Online TV ilirusha hotuba nyingine ya Bw. Erick Kabendera, mwandishi wa habari, ambapo naye alitoa tuhuma kali dhidi ya kampuni ya mawasiliano ya Vodacom. Kabendera alidai kuwa Vodacom ilihusika na mpango wa kumteka.

Katika hotuba hiyo, Kabendera alisema: “Baada ya uchunguzi wa miaka mitatu, mimi na wanasheria wangu tumekusanya ushahidi unaoonyesha wazi kwamba kampuni ya Vodacom Tanzania ilihusika katika njama za kutaka kuniteka. Kama si hatua za haraka zilizochukuliwa na mitandao ya kijamii kufichua njama hizo, pengine ningetekwa au hata kuuawa. Ushahidi huu ni mzito na unatosha kabisa kufungua mashtaka dhidi ya Vodacom hapa Tanzania na hata tanzu zake zilizoko Afrika Kusini na Uingereza.”

Kwa mujibu wa TCRA, Jambo Online TV inatuhumiwa kwa kukiuka Kanuni za Maudhui ya Mtandaoni kwa kurusha maudhui haya bila kutoa nafasi kwa kampuni husika, pamoja na viongozi wa serikali, kutoa ufafanuzi au kujitetea. TCRA imesema kuwa hatua hii si tu imekiuka maadili ya uandishi wa habari, bali pia imeharibu sifa za taasisi za umma na kampuni za kibinafsi.

Kwa mujibu wa kanuni za TCRA, kitendo cha Jambo Online TV kueneza maudhui ya namna hii kinakiuka Kanuni ya 9 (a), inayosema kuwa mtoa huduma wa maudhui mtandaoni lazima kuhakikisha maudhui yanayotangazwa ni salama na hayavunji sheria yoyote ya nchi. Aidha, kanuni za maudhui mtandaoni zinawataka watoa huduma kuhakikisha maudhui yao yanazingatia viwango vya kitaaluma vya uandishi wa habari na kuwapa wahusika fursa ya kutoa maoni yao pale wanapotuhumiwa.

Kamati ya Maudhui ya TCRA imeitisha kikao na uongozi wa Jambo Online TV tarehe 17 Oktoba 2024 katika makao makuu ya TCRA jijini Dar es Salaam ili kutoa utetezi wao kwa tuhuma hizo. Katika barua hiyo, TCRA imeonya kuwa iwapo Jambo Online TV itashindwa kufika katika kikao hicho, hatua kali za kisheria na kiudhibiti zitachukuliwa dhidi yake.

“Kamati ya Maudhui inakitaka Kituo cha Jambo Online TV kuwasilisha utetezi rva maandishi na kufika mbele ya Kamati kujieleza kwa nini hatua za kisheria zisichukuliwe dhidi yake kwa kukiuka Kanuni za Maudhui Mtandaoni, 2020 kama zilivyofanyiwa Marekebisho Mwaka 2022”, imeeleza taarifa hiyo.

Tusubiri na sarakasi za uchaguzi mkuu, demo si November?
 
Tuhuma kwamba jambo tv hawakuwapa wahusika nafasi ya kujieleza hazina msingi wa kutosha.

Hotuba ya Mheshimiwa Tundu Lissu na Bw. Erick Kabendera: Kama vyombo vya habari, wana wajibu wa kuripoti mambo yenye maslahi kwa umma, na hotuba hizi zilikuwa na umuhimu wa umma kutokana na uzito wa madai yaliyotolewa.

Binafsi nadhani wahusika waliotajwa ama kuhusishwa na tuhuma hizo na wao wawaite waandishi hao na watoe ufafanuzi wao ili mizani ibalance sasa.
 
Jambo TV, wao ni chombo cha habari walioalikwa na CHADEMA kupewa habari motomoto yenye maslahi mapana kwa umma na siyo tu Tundu Lissu.

Na ya Eric Kabendera pia habari zake zina manufaa mapana siyo Kabendera tu bali umma mpana wa Tanzania wanaotumia huduma za simu za mkononi walio wateja wa kampuni hiyo ya mawasiliano ya simu

Serikali kupitia TCRA wanataka kubinya haki ya msingi kabisa, raia kupata taarifa na hususan katika hili linawagusa wateja wengi wa kampuni hiyo ya mawasiliano ya simu.
Lakini fikiria pia upande wa pili kupewa nafasi ya kujitetea kabla hujatoa tuhuma la sivyo unaweza kuharibu image ya upande wa pili kwa tuhuma ya uongo.
 
Mkono wa mabeberu yanapoungana na dola gandamizi kuwaangamiza raia

03 October 2024
Dar es Salaam, Tanzania

Mwenyekiti wa makampuni ya Vodacom Afrika atua Tanzania

Mwenyekiti wa makampuni ya Vodacom Afrika Bw. Sakumzi Macozoma akiwa katika ziara ya kikazi akutana na mabosi wa Vodacom Tanzania na pia akutana na viongozi wa serikali ya Tanzania

Vodacom Tanzania PLC we are honored to welcome and host Shameel Joosub, Vodacom Group CEO, and the Vodacom Group Board, led by the Chairman Sakumzi Macozoma
1728580481983.png

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania akimpokea mwenyekiti wa makampuni ya Vodacom Afrika Group, na pamoja wafanya mazungumzo Kushirikisha Serikali katika Mabadiliko ya Kidijitali​

Vodacom Tanzania ilikutana na Waziri wa TEHAMA wa Tanzania kujadili ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi na kuendeleza mageuzi ya kidijitali nchini.

Katika ziara hiyo ujumbe wa Vodacom ulikutana na Mhe. Jerry Silaa, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia wa Tanzania. Majadiliano yalihusu mada kuu, ikijumuisha jukumu muhimu la ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) katika kuendesha maendeleo ya taifa, na njia ambazo Vodacom inaweza kuunga mkono dira ya serikali ya mabadiliko ya kidijitali. Mkutano huo ulisisitiza umakini wa Vodacom katika ushirikiano ili kuharakisha utumiaji wa teknolojia, na hivyo kusaidia kujenga mustakabali wenye uhusiano na ubunifu zaidi kwa Tanzania.

Vodacom Tanzania imesisitiza kujitolea kwake kufanya kazi kwa karibu na serikali ili kuleta maendeleo na kuwezesha kila Mtanzania kupitia teknolojia. Kampuni inalenga kupanua ufikiaji wa kidijitali, kuziba mapengo ya muunganisho, na kukuza siku zijazo ambapo teknolojia inasaidia ukuaji wa uchumi na maendeleo ya kitaifa.
 
Makampuni ya kibeberu ya kimataifa, yanapochagiza kubinywa haki
Lobby groups with opaque funding who are determined to undermine facts about the climate emergency and other established science.

Authoritarian states with no regard for the freedom of the press.

03 October 2024
Ikulu
Dar es Salaam, Tanzania

1728580575914.png

Bw. Sakumzi Macozoma pamoja na ujumbe wake vigogo wa Vodacom walipifika Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dr. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kundi la Makampuni ya Vodacom Bw. Sakumzi Macozoma pamoja na ujumbe wake mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
 
Fikiria kama ungekuwa umetuhumiwa wewe na usipewe nafasi ya kusikilizwa kabla ya tuhumu kutolewa kwa public ungejisikiaje?

Makampuni ya Vodacom Afrika, TIGO / MILLICOM yana rasilimali watu wafanyakazi, fedha kibao, kuajiri wanasheria kuwashauri na hatimaye kuweza kuita media kibao ikiwemo Jambo TV wakatoa ufafanuzi kuhusu sakata hili, tujiulize wanaogopa nini kuitisha press conference?

Hili la kampuni kubwa ya kimataifa kutaka kutishia raia mmoja mmoja halikubaliki, ni ubeberu mkongwe kujificha nyuma ya TCRA wakati kuna jukwaa la kuja wao Vodacom kuelezea walichowafanyia Tundu Lissu na Eric Kabendera waliotumwa na nani au ni mfanyakazi ndani ya VODACOM au TIGO / MILLICOM alitumika n.k n.k

Umma uweze kufahamu yanayoendelea nyuma ya pazia, ili wateja wawe na imani ya kuwa wapo salama.
 
Fikiria kama ungekuwa umetuhumiwa wewe na usipewe nafasi ya kusikilizwa kabla ya tuhumu kutolewa kwa public ungejisikiaje?
Wewe mjinga unatetea kitu gani, nini ambacho hukijui kuhusu Tigo kuuza location za Lissu?

Kwanza kiherehere cha TCRA kimetoka wapi? Maana Tigo hawakuwahi kukanusha zaidi walisema hayo ni ya Uongozi wao uliopita, Viongozi wapya akina Rostam hawahusiki
 
Back
Top Bottom