Pre GE2025 TCRA yailima Barua Jambo TV kwa kurusha taarifa za Tundu Lissu na Kabendera kuhusu shutuma kwa Tigo na Vodacom

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kawaulize TCRA lakini pia kumbuka Kampuni, Taasisi na Serikali si sawa na mtu binafsi.
Jibu, kwakuwa wewe ndio umejitolea kuwa mtetezi wao hapa jukwaani
 
Walirusha hotuba ya Lissu akituhumu Tigo kumfuatilia kabla ya kupigwa risasi. Sheria ya utangazaji inasema kuwa lazima mpe nafasi ya kusikilizwa upande wa pili kabla ya kurusha tuhuma ili upande wa pili upata nafasi ya kujitetea.
Lini umesikia ya ccm yakifata taratibu hizo
 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia Kamati yake ya Maudhui imefungua mashitaka dhidi ya Jambo Online TV, ikidai kuwa kituo hicho cha habari kimekiuka Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kuhusu Maudhui ya Mtandaoni za mwaka 2020, zilizofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

Hatua hii inatokana na matangazo ya maudhui yaliyotajwa kuwa natuhuma nzito yaliyotolewa na kituo hicho bila kuwapa nafasi wahusika kutoa ufafanuzi wao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa tarehe 9 Oktoba 2024, Mamlaka ya Mawasiliano kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, inadai kuwa tarehe 1 Oktoba 2024, Jambo Online TV inadaiwa kurusha hotuba ya Mheshimiwa Tundu Lissu, ambayo iliibua tuhuma dhidi ya viongozi wa serikali na kampuni ya Tigo.

Hotuba hiyo, ambayo ilichapishwa mtandaoni, iliweka wazi madai mazito yaliyohusisha kampuni ya mawasiliano ya simu ya Tigo, ambapo Tundu Lissu alieleza kuwa Tigo ilihusika katika njama za kumfuatilia kabla ya kushambuliwa.

Katika hotuba yake, Lissu alinukuliwa akisema, “Tigo walikuwa wakinifuatilia sio kwa njia ya kawaida tu, bali walitumia wachunguzi wa ndani kunifanyia ufuatiliaji wa kina. Mtu mmoja aliyekuwa mfanyakazi wa Metropolitan Police ya London ndiye alikuwa mchunguzi wao wa ndani, akichunguza matendo ya wafanyakazi wa Tigo. Siku tano baada ya mimi kushambuliwa, mchunguzi huyo alisikika akisema kuwa walikuwa wanajua taarifa zangu zote, hata mahali nilipokuwa.”

TCRA imeendelea kudai kuwa, siku iliyofuata tarehe 2 Oktoba 2024, Jambo Online TV ilirusha hotuba nyingine ya Bw. Erick Kabendera, mwandishi wa habari, ambapo naye alitoa tuhuma kali dhidi ya kampuni ya mawasiliano ya Vodacom. Kabendera alidai kuwa Vodacom ilihusika na mpango wa kumteka.

Katika hotuba hiyo, Kabendera alisema: “Baada ya uchunguzi wa miaka mitatu, mimi na wanasheria wangu tumekusanya ushahidi unaoonyesha wazi kwamba kampuni ya Vodacom Tanzania ilihusika katika njama za kutaka kuniteka. Kama si hatua za haraka zilizochukuliwa na mitandao ya kijamii kufichua njama hizo, pengine ningetekwa au hata kuuawa. Ushahidi huu ni mzito na unatosha kabisa kufungua mashtaka dhidi ya Vodacom hapa Tanzania na hata tanzu zake zilizoko Afrika Kusini na Uingereza.”

Kwa mujibu wa TCRA, Jambo Online TV inatuhumiwa kwa kukiuka Kanuni za Maudhui ya Mtandaoni kwa kurusha maudhui haya bila kutoa nafasi kwa kampuni husika, pamoja na viongozi wa serikali, kutoa ufafanuzi au kujitetea. TCRA imesema kuwa hatua hii si tu imekiuka maadili ya uandishi wa habari, bali pia imeharibu sifa za taasisi za umma na kampuni za kibinafsi.

Kwa mujibu wa kanuni za TCRA, kitendo cha Jambo Online TV kueneza maudhui ya namna hii kinakiuka Kanuni ya 9 (a), inayosema kuwa mtoa huduma wa maudhui mtandaoni lazima kuhakikisha maudhui yanayotangazwa ni salama na hayavunji sheria yoyote ya nchi. Aidha, kanuni za maudhui mtandaoni zinawataka watoa huduma kuhakikisha maudhui yao yanazingatia viwango vya kitaaluma vya uandishi wa habari na kuwapa wahusika fursa ya kutoa maoni yao pale wanapotuhumiwa.

Kamati ya Maudhui ya TCRA imeitisha kikao na uongozi wa Jambo Online TV tarehe 17 Oktoba 2024 katika makao makuu ya TCRA jijini Dar es Salaam ili kutoa utetezi wao kwa tuhuma hizo. Katika barua hiyo, TCRA imeonya kuwa iwapo Jambo Online TV itashindwa kufika katika kikao hicho, hatua kali za kisheria na kiudhibiti zitachukuliwa dhidi yake.

“Kamati ya Maudhui inakitaka Kituo cha Jambo Online TV kuwasilisha utetezi rva maandishi na kufika mbele ya Kamati kujieleza kwa nini hatua za kisheria zisichukuliwe dhidi yake kwa kukiuka Kanuni za Maudhui Mtandaoni, 2020 kama zilivyofanyiwa Marekebisho Mwaka 2022”, imeeleza taarifa hiyo.
kwani kufanya hivyo ni kosa gani? au tigo nao ni ccm?
 
Walirusha hotuba ya Lissu akituhumu Tigo kumfuatilia kabla ya kupigwa risasi. Sheria ya utangazaji inasema kuwa lazima mpe nafasi ya kusikilizwa upande wa pili kabla ya kurusha tuhuma ili upande wa pili upata nafasi ya kujitetea.
Hii sheria haiwahusu wanaowatuka wapinzani?!
 
Makampuni ya Vodacom Afrika, yana rasilimali watu wafanyakazi, fedha kibao, kuajiri wanasheria kuwashauri na hatimaye kuweza kuita media kibao ikiwemo Jambo...
Rushwa tu ,makampuni hayo yameona wapitie njia hiyo kujisafisha kuliko waitishe vyombo vya habari wamwage ugali kabendera na LISu wamemwaga mboga
 
Mtoa taarifa ndio mwenye jukumu la ku-confirm upande unaotuhumiwa. Hivyo Jambo TV walipashwa kuupa nafasi upande unaotuhumiwa kabla ya kurusha tuhuma kwenye chombo chao. Voda na Tigo pia wanaweza kuwafikisha mahakama.
Kwa mfano RAIS alivyosema kuhusu mikia ya watu ,haikutakiwa kurushwa habari hiyo hadi wakahojiwe upande wa pili?
 
Unaota au unaoteshwa TCRA kila habari ikipelekwa pale ili waruhusu irushwe au isirushwe patatosha?
TCRA wanaangalia materiality hiyo habari ina damage kiasi gani kwa usalama wa nji na uchumi na wawekezaji na mapato ya kodi za serikali

Ila kama damage ndogo sijui Mafwele anatuhumiwa sijui nini waweza ignore

Lakini ku damage image ya kampuni za wawekezaji za kimataifa walipa kodi wakubwa kama Tigo au Vodacom wabaochangia kodi kubwa sana ambazo hata vyama vya siasa ruzuku hutoka hapo lazima moto uwake tena sio wa kitoto sababu tuhuma kama hizo zinaua investors confidence kwenye nchi

Hivyo local media hopeless mrusha ujinga unakiuka vigezo lazima akutane na rungu la dola

Nchi inahangaikq kutafuta wawekezaji.wa simu ambao ukiweka vocha pesa inaingia kodi ukipiga nk pesa ya kodi inaingia halafu mwehu tu mwandishi wa habari anataka kuua huo uwekezaji kirahisi rahisi tu bila ushahidi eti freedom of the press lazima akutane na mkono wa serikali na Mahakama
 
Jambo TV, wao ni chombo cha habari walioalikwa na CHADEMA kupewa habari motomoto yenye maslahi mapana kwa umma na siyo tu Tundu Lissu.

Na ya Eric Kabendera pia habari zake zina manufaa mapana siyo Kabendera tu bali umma mpana wa Tanzania wanaotumia huduma za simu za mkononi walio wateja wa kampuni hiyo ya mawasiliano ya simu

Serikali kupitia TCRA wanataka kubinya haki ya msingi kabisa, raia kupata taarifa na hususan katika hili linawagusa wateja wengi wa kampuni hiyo ya mawasiliano ya simu.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia Kamati yake ya Maudhui imefungua mashitaka dhidi ya Jambo Online TV, ikidai kuwa kituo hicho cha habari kimekiuka Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kuhusu Maudhui ya Mtandaoni za mwaka 2020, zilizofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

Hatua hii inatokana na matangazo ya maudhui yaliyotajwa kuwa natuhuma nzito yaliyotolewa na kituo hicho bila kuwapa nafasi wahusika kutoa ufafanuzi wao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa tarehe 9 Oktoba 2024, Mamlaka ya Mawasiliano kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, inadai kuwa tarehe 1 Oktoba 2024, Jambo Online TV inadaiwa kurusha hotuba ya Mheshimiwa Tundu Lissu, ambayo iliibua tuhuma dhidi ya viongozi wa serikali na kampuni ya Tigo.

Hotuba hiyo, ambayo ilichapishwa mtandaoni, iliweka wazi madai mazito yaliyohusisha kampuni ya mawasiliano ya simu ya Tigo, ambapo Tundu Lissu alieleza kuwa Tigo ilihusika katika njama za kumfuatilia kabla ya kushambuliwa.

Katika hotuba yake, Lissu alinukuliwa akisema, “Tigo walikuwa wakinifuatilia sio kwa njia ya kawaida tu, bali walitumia wachunguzi wa ndani kunifanyia ufuatiliaji wa kina. Mtu mmoja aliyekuwa mfanyakazi wa Metropolitan Police ya London ndiye alikuwa mchunguzi wao wa ndani, akichunguza matendo ya wafanyakazi wa Tigo. Siku tano baada ya mimi kushambuliwa, mchunguzi huyo alisikika akisema kuwa walikuwa wanajua taarifa zangu zote, hata mahali nilipokuwa.”

TCRA imeendelea kudai kuwa, siku iliyofuata tarehe 2 Oktoba 2024, Jambo Online TV ilirusha hotuba nyingine ya Bw. Erick Kabendera, mwandishi wa habari, ambapo naye alitoa tuhuma kali dhidi ya kampuni ya mawasiliano ya Vodacom. Kabendera alidai kuwa Vodacom ilihusika na mpango wa kumteka.

Katika hotuba hiyo, Kabendera alisema: “Baada ya uchunguzi wa miaka mitatu, mimi na wanasheria wangu tumekusanya ushahidi unaoonyesha wazi kwamba kampuni ya Vodacom Tanzania ilihusika katika njama za kutaka kuniteka. Kama si hatua za haraka zilizochukuliwa na mitandao ya kijamii kufichua njama hizo, pengine ningetekwa au hata kuuawa. Ushahidi huu ni mzito na unatosha kabisa kufungua mashtaka dhidi ya Vodacom hapa Tanzania na hata tanzu zake zilizoko Afrika Kusini na Uingereza.”

Kwa mujibu wa TCRA, Jambo Online TV inatuhumiwa kwa kukiuka Kanuni za Maudhui ya Mtandaoni kwa kurusha maudhui haya bila kutoa nafasi kwa kampuni husika, pamoja na viongozi wa serikali, kutoa ufafanuzi au kujitetea. TCRA imesema kuwa hatua hii si tu imekiuka maadili ya uandishi wa habari, bali pia imeharibu sifa za taasisi za umma na kampuni za kibinafsi.

Kwa mujibu wa kanuni za TCRA, kitendo cha Jambo Online TV kueneza maudhui ya namna hii kinakiuka Kanuni ya 9 (a), inayosema kuwa mtoa huduma wa maudhui mtandaoni lazima kuhakikisha maudhui yanayotangazwa ni salama na hayavunji sheria yoyote ya nchi. Aidha, kanuni za maudhui mtandaoni zinawataka watoa huduma kuhakikisha maudhui yao yanazingatia viwango vya kitaaluma vya uandishi wa habari na kuwapa wahusika fursa ya kutoa maoni yao pale wanapotuhumiwa.

Kamati ya Maudhui ya TCRA imeitisha kikao na uongozi wa Jambo Online TV tarehe 17 Oktoba 2024 katika makao makuu ya TCRA jijini Dar es Salaam ili kutoa utetezi wao kwa tuhuma hizo. Katika barua hiyo, TCRA imeonya kuwa iwapo Jambo Online TV itashindwa kufika katika kikao hicho, hatua kali za kisheria na kiudhibiti zitachukuliwa dhidi yake.

“Kamati ya Maudhui inakitaka Kituo cha Jambo Online TV kuwasilisha utetezi rva maandishi na kufika mbele ya Kamati kujieleza kwa nini hatua za kisheria zisichukuliwe dhidi yake kwa kukiuka Kanuni za Maudhui Mtandaoni, 2020 kama zilivyofanyiwa Marekebisho Mwaka 2022”, imeeleza taarifa hiyo.
Naona TCRA Sasa inatumika vibaya Sana na Watu waovu au Wahalifu. Hao Tigo, Voda na serikali ambao wanawatetea hawabebeki hata kwa mbeleko ya chuma, ni wahalifu waliokubuhu ambao sisi wengine tunazo data za kutosha Sana kuhusu uhalifu wao. Hayo masuala ya Lissu na Kabendera ni miongoni mwa Kesi chache Sana kuhusu uhalifu wao. Mimi binafsi ni pia ni mmojawapo wa Wahanga wa uhalifu wao, na kutokana na mienendo hii mibaya ya TCRA naona kama kuna ULAZIMA wa Mimi kuweka wazi juu ya uhalifu wa hao Watu waliofanya dhidi yangu.

Nitafuatilia kwa ukaribu Sana suala hili la Mgogoro huu ambao TCRA wameibua dhidi ya Jambo TV, nitakapobaini kwamba Jambo TV hawatendewi haki Basi nitalazimika kuweka kila kitu wazi kuhusu uovu niliofanyiwa na hao Watu ili kuuthibitishia ulimwengu wote juu ya uhalifu wa Watu hao.
Ninajua pia kwamba ndani ya TCRA mwenyewe pia wapo watu (agents) ambao nao kwa namna Moja ama nyingine pia walihusika kwenye suala langu hilo, nao nitawataja kwa Majina yao halisi na namna jinsi walivyohusika katika mkasa huo. Acha lizame ili tugawane mbao, na liwalo na liwe! I have nothing to lose.
 
Sasa hapo wamekosea wapi na wakati wameuhabalisha umaa............ile si habari tu kama habari nyingine.......kama uhusiki na kesi huwezi kufungwa
Nchi ya kiduwanzi sana hii
 
Mkuu naona unachanganya issue mbili tofauti hii ni issue ya Tigo na Lissu wala si Sativa.
Na mimi nimegusia kama wao walivyotaka busara ingetumika kuhoji na upande wa pili........ndio maana na mimi nikatoka kidogo ili nihoji mbona kule hakuna kubalance mipasho.......maana sioni kama kulikuwa kunahitajika kuhoji tena zaidi ya kukamata huyo mafwele na yeye aende kwa p did
 
Kwahiyo hawatakiwi kuripoti? Mana hapo aliyesema hayo maneno si Lissu na Kabendera? Hao waliotoa taarifa wamekosea nini? Naomba elimu tafadhali
Nenda kasome kanuni za mawasiliano za Kieliktroniki na posta kuhusu mahudhui ya mtandaon ya mwaka 2020 zilizofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

Huu utaratibu wa kupenda kulishwa lishwa, mtakuja kulishwa matango pori mkawaona TCRA wanatumika kumbe hawatumiki.
 
Back
Top Bottom