Pre GE2025 TCRA yailima Barua Jambo TV kwa kurusha taarifa za Tundu Lissu na Kabendera kuhusu shutuma kwa Tigo na Vodacom

Pre GE2025 TCRA yailima Barua Jambo TV kwa kurusha taarifa za Tundu Lissu na Kabendera kuhusu shutuma kwa Tigo na Vodacom

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Walirusha hotuba ya Lissu akituhumu Tigo kumfuatilia kabla ya kupigwa risasi. Sheria ya utangazaji inasema kuwa lazima mpe nafasi ya kusikilizwa upande wa pili kabla ya kurusha tuhuma ili upande wa pili upata nafasi ya kujitetea.
Vipi Kwa tukio ambalo liko mubashara 'live' huo upande wa pili unatakiwa kujitetea saa ngapi?
 
TCRA wanaangalia materiality hiyo habari ina damage kiasi gani kwa usalama wa nji na uchumi na wawekezaji na mapato ya kodi za serikali

Ila kama damage ndogo sijui Mafwele anatuhumiwa sijui nini waweza ignore

Lakini ku damage image ya kampuni za wawekezaji za kimataifa walipa kodi wakubwa kama Tigo au Vodacom wabaochangia kodi kubwa sana ambazo hata vyama vya siasa ruzuku hutoka hapo lazima moto uwake tena sio wa kitoto sababu tuhuma kama hizo zinaua investors confidence kwenye nchi

Hivyo local media hopeless mrusha ujinga unakiuka vigezo lazima akutane na rungu la dola

Nchi inahangaikq kutafuta wawekezaji.wa simu ambao ukiweka vocha pesa inaingia kodi ukipiga nk pesa ya kodi inaingia halafu mwehu tu mwandishi wa habari anataka kuua huo uwekezaji kirahisi rahisi tu bila ushahidi eti freedom of the press lazima akutane na mkono wa serikali na Mahakama
Kwa hio wewe sababu hayajakukuta unasema hio kituo ni hopeless ila yakikukuta utafanyaje?
 
Ok. Ili taarifa ikamilike, walitakiwa waende Vodacom na TCRA kuwauliza warushe au wasirushe
Siyo hivyo, kurusha au tokurusha maudhui si kazi ya watuhumiwa na haihitaji ruhusa kutoka popote.

Kubalonce story ni kwenda kuhoji na upande wa pili mf:Voda na Tigo, sasa wao walihoji upande mmoja na kurusha.
 

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia Kamati yake ya Maudhui imefungua mashitaka dhidi ya Jambo Online TV, ikidai kuwa kituo hicho cha habari kimekiuka Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kuhusu Maudhui ya Mtandaoni za mwaka 2020, zilizofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

Hatua hii inatokana na matangazo ya maudhui yaliyotajwa kuwa natuhuma nzito yaliyotolewa na kituo hicho bila kuwapa nafasi wahusika kutoa ufafanuzi wao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa tarehe 9 Oktoba 2024, Mamlaka ya Mawasiliano kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, inadai kuwa tarehe 1 Oktoba 2024, Jambo Online TV inadaiwa kurusha hotuba ya Mheshimiwa Tundu Lissu, ambayo iliibua tuhuma dhidi ya viongozi wa serikali na kampuni ya Tigo.

Hotuba hiyo, ambayo ilichapishwa mtandaoni, iliweka wazi madai mazito yaliyohusisha kampuni ya mawasiliano ya simu ya Tigo, ambapo Tundu Lissu alieleza kuwa Tigo ilihusika katika njama za kumfuatilia kabla ya kushambuliwa.

Katika hotuba yake, Lissu alinukuliwa akisema, “Tigo walikuwa wakinifuatilia sio kwa njia ya kawaida tu, bali walitumia wachunguzi wa ndani kunifanyia ufuatiliaji wa kina. Mtu mmoja aliyekuwa mfanyakazi wa Metropolitan Police ya London ndiye alikuwa mchunguzi wao wa ndani, akichunguza matendo ya wafanyakazi wa Tigo. Siku tano baada ya mimi kushambuliwa, mchunguzi huyo alisikika akisema kuwa walikuwa wanajua taarifa zangu zote, hata mahali nilipokuwa.”

TCRA imeendelea kudai kuwa, siku iliyofuata tarehe 2 Oktoba 2024, Jambo Online TV ilirusha hotuba nyingine ya Bw. Erick Kabendera, mwandishi wa habari, ambapo naye alitoa tuhuma kali dhidi ya kampuni ya mawasiliano ya Vodacom. Kabendera alidai kuwa Vodacom ilihusika na mpango wa kumteka.

Katika hotuba hiyo, Kabendera alisema: “Baada ya uchunguzi wa miaka mitatu, mimi na wanasheria wangu tumekusanya ushahidi unaoonyesha wazi kwamba kampuni ya Vodacom Tanzania ilihusika katika njama za kutaka kuniteka. Kama si hatua za haraka zilizochukuliwa na mitandao ya kijamii kufichua njama hizo, pengine ningetekwa au hata kuuawa. Ushahidi huu ni mzito na unatosha kabisa kufungua mashtaka dhidi ya Vodacom hapa Tanzania na hata tanzu zake zilizoko Afrika Kusini na Uingereza.”

Kwa mujibu wa TCRA, Jambo Online TV inatuhumiwa kwa kukiuka Kanuni za Maudhui ya Mtandaoni kwa kurusha maudhui haya bila kutoa nafasi kwa kampuni husika, pamoja na viongozi wa serikali, kutoa ufafanuzi au kujitetea. TCRA imesema kuwa hatua hii si tu imekiuka maadili ya uandishi wa habari, bali pia imeharibu sifa za taasisi za umma na kampuni za kibinafsi.

Kwa mujibu wa kanuni za TCRA, kitendo cha Jambo Online TV kueneza maudhui ya namna hii kinakiuka Kanuni ya 9 (a), inayosema kuwa mtoa huduma wa maudhui mtandaoni lazima kuhakikisha maudhui yanayotangazwa ni salama na hayavunji sheria yoyote ya nchi. Aidha, kanuni za maudhui mtandaoni zinawataka watoa huduma kuhakikisha maudhui yao yanazingatia viwango vya kitaaluma vya uandishi wa habari na kuwapa wahusika fursa ya kutoa maoni yao pale wanapotuhumiwa.

Kamati ya Maudhui ya TCRA imeitisha kikao na uongozi wa Jambo Online TV tarehe 17 Oktoba 2024 katika makao makuu ya TCRA jijini Dar es Salaam ili kutoa utetezi wao kwa tuhuma hizo. Katika barua hiyo, TCRA imeonya kuwa iwapo Jambo Online TV itashindwa kufika katika kikao hicho, hatua kali za kisheria na kiudhibiti zitachukuliwa dhidi yake.

“Kamati ya Maudhui inakitaka Kituo cha Jambo Online TV kuwasilisha utetezi rva maandishi na kufika mbele ya Kamati kujieleza kwa nini hatua za kisheria zisichukuliwe dhidi yake kwa kukiuka Kanuni za Maudhui Mtandaoni, 2020 kama zilivyofanyiwa Marekebisho Mwaka 2022”, imeeleza taarifa hiyo.

Chanzo: Jambo TV
Kwa nn jambo TV peke ake
Wakati hata online nyingine zilirusha
 
Siyo hivyo, kurusha au tokurusha maudhui si kazi ya watuhumiwa na haihitaji ruhusa kutoka popote.

Kubalonce story ni kwenda kuhoji na upande wa pili mf:Voda na Tigo, sasa wao walihoji upande mmoja na kurusha.
Kumbuka tukio la Lisu lilikua live.
 
Yaani TCRA bhana wanataka kila kituo cha habari kiwe kama TCRA! Kuanzia asubuhi mpaka jioni! Masaa 24 iwe ni mapambio ya Mama kaupiga mwingi! Yaani leseni walipe kwa pesa zao halafu na maudhui yawe ya upande mmoja!

Dkt. Jabiri Kuwe Bakari ni kweli kabsa umepata uteuzi kutoka kwa Rais lakini haina maana utumie nafasi hiyo ya kuwa kwenye chombo kikubwa kama hicho kwa ajili ya kusifu na kupiga mapambio! Kazi zinaisha Daktari acha kabsa kuifanya TCRA ni mali ya Samia au mali yenu! TCRA ni chombo cha watanzania.

Yaani kuna vituo vingi vinarusha matangazo yenye maudhui mabaya lakini hamtolei onyo wala makatazo yoyote. Vituo vinarusha taarifa za ngono (connection za ngono), zinarusha maudhui ya matusi ka kukicha! Halafu mnapiga onyo matangazo kuhusu Mheshimiwa Tundu Lissu! Mnafanya vitu vya ovyo sana! Kuna mambo mengi ya kufuatilia kuliko kufuatilia hayo!

Dkt. Jabiri Kuwe Bakari jitathimini mzee wangu! Wewe ni mtumishi wa Watanzania sio Samia!​
 
Screenshot_20241010-221458.png
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia Kamati yake ya Maudhui imefungua mashitaka dhidi ya Jambo Online TV, ikidai kuwa kituo hicho cha habari kimekiuka Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kuhusu Maudhui ya Mtandaoni za mwaka 2020, zilizofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

Hatua hii inatokana na matangazo ya maudhui yaliyotajwa kuwa natuhuma nzito yaliyotolewa na kituo hicho bila kuwapa nafasi wahusika kutoa ufafanuzi wao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa tarehe 9 Oktoba 2024, Mamlaka ya Mawasiliano kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, inadai kuwa tarehe 1 Oktoba 2024, Jambo Online TV inadaiwa kurusha hotuba ya Mheshimiwa Tundu Lissu, ambayo iliibua tuhuma dhidi ya viongozi wa serikali na kampuni ya Tigo.

Hotuba hiyo, ambayo ilichapishwa mtandaoni, iliweka wazi madai mazito yaliyohusisha kampuni ya mawasiliano ya simu ya Tigo, ambapo Tundu Lissu alieleza kuwa Tigo ilihusika katika njama za kumfuatilia kabla ya kushambuliwa.

Katika hotuba yake, Lissu alinukuliwa akisema, “Tigo walikuwa wakinifuatilia sio kwa njia ya kawaida tu, bali walitumia wachunguzi wa ndani kunifanyia ufuatiliaji wa kina. Mtu mmoja aliyekuwa mfanyakazi wa Metropolitan Police ya London ndiye alikuwa mchunguzi wao wa ndani, akichunguza matendo ya wafanyakazi wa Tigo. Siku tano baada ya mimi kushambuliwa, mchunguzi huyo alisikika akisema kuwa walikuwa wanajua taarifa zangu zote, hata mahali nilipokuwa.”

TCRA imeendelea kudai kuwa, siku iliyofuata tarehe 2 Oktoba 2024, Jambo Online TV ilirusha hotuba nyingine ya Bw. Erick Kabendera, mwandishi wa habari, ambapo naye alitoa tuhuma kali dhidi ya kampuni ya mawasiliano ya Vodacom. Kabendera alidai kuwa Vodacom ilihusika na mpango wa kumteka.

Katika hotuba hiyo, Kabendera alisema: “Baada ya uchunguzi wa miaka mitatu, mimi na wanasheria wangu tumekusanya ushahidi unaoonyesha wazi kwamba kampuni ya Vodacom Tanzania ilihusika katika njama za kutaka kuniteka. Kama si hatua za haraka zilizochukuliwa na mitandao ya kijamii kufichua njama hizo, pengine ningetekwa au hata

Kamati ya Maudhui inakitaka Kituo cha Jambo Online TV kuwasilisha utetezi rva maandishi na kufika mbele ya Kamati kujieleza kwa nini hatua za kisheria zisichukuliwe dhidi yake kwa kukiuka Kanuni za Maudhui Mtandaoni, 2020 kama zilivyofanyiwa Marekebisho Mwaka 2022”, imeeleza taarifa hiyo. kuuawa. Ushahidi huu ni mzito na unatosha kabisa kufungua mashtaka dhidi ya Vodacom hapa Tanzania na hata tanzu zake zilizoko Afrika Kusini na Uingereza.”

Source: DARMPYA TV Twitter /X page
 
Nchi hii ina taasisi .kuna vitu unasoma mpaka unashangaa kuwa kiwango cha upumbavu ni kikubwa isivyo kawaida.
 
Naona TCRA Sasa inatumika vibaya Sana na Watu waovu au Wahalifu. Hao Tigo, Voda na serikali ambao wanawatetea hawabebeki hata kwa mbeleko ya chuma, ni wahalifu waliokubuhu ambao sisi wengine tunazo data za kutosha Sana kuhusu uhalifu wao.

Hayo masuala ya Lissu na Kabendera ni miongoni mwa Kesi chache Sana kuhusu uhalifu wao. Mimi binafsi ni pia ni mmojawapo wa Wahanga wa uhalifu wao, na kutokana na mienendo hii mibaya ya TCRA naona kama kuna ULAZIMA wa Mimi kuweka wazi juu ya uhalifu wa hao Watu waliofanya dhidi yangu.

Nitafuatilia kwa ukaribu Sana suala hili la Mgogoro huu ambao TCRA wameibua dhidi ya Jambo TV, nitakapobaini kwamba Jambo TV hawatendewi haki Basi nitalazimika kuweka kila kitu wazi kuhusu uovu niliofanyiwa na hao Watu ili kuuthibitishia ulimwengu wote juu ya uhalifu wa Watu hao.

Ninajua pia kwamba ndani ya TCRA mwenyewe pia wapo watu (agents) ambao nao kwa namna Moja ama nyingine pia walihusika kwenye suala langu hilo, nao nitawataja kwa Majina yao halisi na namna jinsi walivyohusika katika mkasa huo. Acha lizame ili tugawane mbao, na liwalo na liwe! I have nothing to lose.
 
Sheria ni fair ili tusiumizane kwa tuhuma za uongo.

HABARI YA TIGO TANZANIA IMESAMBAA DUNIA NZIMA SOURCE MAHAKAMA YA KAZI JIJINI LONDON

Somo kinachoendelea kesi jijini London ya mfanyakazi wa TIGO / MILLICOM akimshitaki mwajiri kwa kumwashisha kazi wakati alipewa kazi kufuatilia mienendo isiyofaa ya kuvunja sheria, kukiuka faragha za wateja akakumbana na sakata la Tundu Lissu lililoonesha fingerprint za mienendo ya kiuhalifu ya dola dhidi ya mteja wa TIGO / MILLICOM.

The case has taken four years to reach trial, partly as a result of efforts by Millicom to have Clifford’s claim heard under reporting restrictions. At one point the firm argued that unless it was granted a secrecy order it would be unable to defend the claim. The secrecy application was dismissed earlier this year.

The report concluded that “information had been provided to the Tanzanian government since 22 August 2017”, the lawyers said. “From 29 August 2017, the intensity of the tracking increased and [Millicom] used its human and electronic resources to livetrack 24/7 the location of two of Mr Lissu’s mobile phones.”

The data was passed to the government via WhatsApp messages, which Millicom was later asked to delete. No formal legal request for the data appeared to have been filed.

“In the claimant’s reasonable belief, this information tended to show that [Millicom] was involved in an attempted political assassination and act of terrorism,” Clifford’s lawyers said.
 
Lakini fikiria pia upande wa pili kupewa nafasi ya kujitetea kabla hujatoa tuhuma la sivyo unaweza kuharibu image ya upande wa pili kwa tuhuma ya uongo.
sasa mkuu mkutano wa lissu dhidi ya tigo ulikuwa live Jambo online Tv huo muda upande wa pili wapewe nafasi kujitetea ni kwa namna gani kwa mkutano unaokuwa live.?
 
When brothers fight to death, a stranger inherits their father's estate - Chinua Achebe
 

Tanzania’s Tundu Lissu Takes Action Against Millicom Over Alleged Pre-Attempt Surveillance​

September 25, 2024


By Adonis Byemelwa

lissu.jpg
The investigation into Lissu's shooting has remained open, but frustration is palpable as police have yet to apprehend anyone linked to the attack. Photo courtesy

Former Singida East MP Tundu Lissu has intensified his quest for justice against Millicom, alleging that the company leaked his phone data to Tanzanian authorities before a 2017 assassination attempt.

This unfolding saga raises critical questions about corporate complicity, governmental accountability, and the fundamental right to privacy, setting a precedent for how such violations are addressed in Tanzania.

Lissu, now the Deputy Chairperson of Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mainland, has called on his legal team to initiate proceedings to uncover the identities of those responsible for the attack on his life, stating, “We need to know the entire truth—who sent them, their ranks, and their names.”

Addressing the press on September 25, 2024, at Chadema’s headquarters in Mikocheni, Dar es Salaam, Lissu expressed frustration at the lack of accountability following the violent incident that left him seriously injured.

The allegations come on the heels of a report published by The Guardian in London, which revealed details from court documents presented by Michael Clifford, a former Millicom investigator who was dismissed after raising concerns about the company’s actions.

The details surrounding Lissu’s attack are chilling. On the afternoon of September 7, 2017, he was shot multiple times outside his home in Dodoma after returning from a parliamentary meeting. Following the attack, he was rushed to Dodoma Referral Hospital for initial treatment before being transferred to Nairobi, Kenya, for more comprehensive medical care.

His journey for justice has since been marred by unanswered questions and allegations of complicity involving major telecommunications entities.

Lissu's renewed push for transparency comes as Clifford's revelations claim that Millicom provided the Tanzanian government with real-time data on Lissu’s phone and whereabouts in the weeks leading up to the attack.

According to Clifford, who later took Millicom to court, the company acted unlawfully by sharing sensitive information without a proper legal request.


“Five days after Lissu was attacked, I began my investigation after overhearing a call that indicated Millicom was sharing his mobile data with the Tanzanian authorities,” he stated in his court submissions.

Despite efforts to reach out to both the Tanzanian government and Tigo Tanzania for comments on the allegations, the responses have been elusive. Millicom, which operates in both South America and Africa, has vehemently denied Clifford's claims, asserting that his dismissal was due to operational downsizing and not because of any misconduct related to the surveillance of Lissu.

The investigation into Lissu's shooting has remained open, but frustration is palpable as police have yet to apprehend anyone linked to the attack. Lissu’s plea for information intensified as he highlighted the critical role that his assault has had on his family, stating, “This incident has not only scarred me but also deeply affected my family. My wife and children long to return home, but the trauma from what they witnessed in Nairobi is unbearable.”

The shadows of doubt loom larger as Lissu questioned the effectiveness of security measures in his residential area, which is known for hosting high-profile officials, including the current Speaker of the National Assembly. “On the day of my attack, security was noticeably absent, and questions arise as to where they were during such a critical moment. There are CCTV cameras in the area; why were they not utilized to capture the assailants?” he queried, pressing for answers that have remained elusive for years.

Now armed with new evidence from Clifford’s ongoing case in the UK, Lissu feels emboldened to pursue legal action against Millicom and the Tanzanian government. “We have a starting point. When we take this matter to court, we will demand that they present Clifford’s findings. What we have now is substantial enough to file a case,” he proclaimed. Lissu has engaged international attorney Bob Amsterdam and a team of lawyers to gather evidence and prepare for potential lawsuits in international courts.

“Through this case, we aim not only to seek justice but also to unravel the web of complicity that allowed this attack to occur. We demand transparency regarding who ordered my surveillance, the names and ranks of the individuals involved, and whether Millicom was financially compensated for their actions,” he emphasized.

The implications of Lissu’s case are vast, raising questions about corporate responsibility, governmental oversight, and the fundamental right to privacy. As Lissu gears up for legal action, he remains resolute: “The truth will come to light, and we will expose those who think they can act with impunity.”

Millicom’s transition in Tanzania, culminating in the sale of its operations to Axian Telecom in April 2022, has not diminished the pressure on the company to respond to these serious allegations. Axian, in acquiring Tigo, inherited a complex legacy, and it remains to be seen how this situation will impact the newly restructured telecommunications landscape in Tanzania.

As the legal proceedings unfold in the UK and Lissu’s calls for justice grow louder, the story highlights not just a personal battle but a broader struggle for accountability in a political landscape fraught with uncertainty and unanswered questions. For Lissu, the pursuit of truth is a necessity not just for his healing but for the sake of justice in Tanzania.

In a world where technology intersects with governance, the stakes have never been higher. Lissu’s determination to bring the perpetrators to justice signals a pivotal moment for accountability in Tanzania, challenging corporations and government entities alike to uphold ethical standards in their operations. The path forward may be fraught with challenges, but for Lissu and his supporters, the quest for justice is a mission that cannot be compromised
 
Back
Top Bottom