TCRA yaipiga faini ya Tsh. bilioni 11.89 Kampuni ya Intaneti ya Raha Limited kwa kuendesha shughuli zake bila kuwa na kibali

Ukiwa mfanyabiashara hakuna jambo linakera kama kupigwa faini ambayo haiendani na uhalisia na mtaji au mapato ya biashara yako.

Mamlaka ziwaangalie wafanyabiashara. Wasitumike kama kitega uchumi.

Sheria zipo. Zinapokiukwa waangalie na uhalisia sio kuweka kizingiti kwa wafanyabiashara.

Uchumi utakuwa kwa kujali wafanyabiashara. Isifikie kipindi waonewe kwa misingi ya sheria kandamizi au maamuzi ya kuumiza.

Serikali iangalie hili. Isije kupelekea kuua biashara binafsi bila kujua ni kuua uchumi wa nchi.
 
UPUUZI MTUPU! Kampuni thamani yake haifiki hata bilioni moja halafu faini yake ni bilioni 11? 😳😳😳😳
Itakuwa ni typo tu ya mleta mada. Ukijumlisha pesa zote haifiki hata 50m
 
Reactions: BAK
Walikuwa wapi kuwapa hiyo fine mwezi March. Biashara za kuviziana ni sawa na uchawi
 
Swali ni kwann ulifanya kazi bila kibali ndoshida inaanzia hapo, yaani utajitetea vipi kwamfano aiseee? Tena hiyo ndgo ukiangalia na formula zake kwa usahihi unaweza kukuta unatakiwa kulipa T na sio B

Wasingeiba hayo masafa je tcra wangepata Hizo billions?
 
hawa wanaadhibiwa sababu wamejirock down na kupunguza wafanyakazi sababu ya madhara ya corona. sasa sielewi TCRA ilitegemea wafanyeje wakati wateja wamewakimbia sababu ya corona.

Yeah na wamepunguza wafanyakazi sana
 
hawa wanaadhibiwa sababu wamejirock down na kupunguza wafanyakazi sababu ya madhara ya corona. sasa sielewi TCRA ilitegemea wafanyeje wakati wateja wamewakimbia sababu ya corona.
Acha uongo! Wakati wa corona ndiyo Kampuni zinazotoa huduma za mawasiliano wamepata faida zaidi na zaidi kwa kuwa bandwith zimetumika zaidi kwa sababu kampuni nyingi zilikuwa zinafanya kazi toka home! Sawa na Pharmacy. Kama hujui nyamaza.
 
Tunahangaika kutafuta pesa za kampeni na vilevile ni hela ya kisukuma uchumi wa kufikia uchumi wa Kati kutoka B2 na Sasa hapo tumefondoka mpaka B1.
 
UPUUZI MTUPU! Kampuni thamani yake haifiki hata bilioni moja halafu faini yake ni bilioni 11? [emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]
Nadhani kuna kitu nyuma ya pazia voda tigo airtel halotel wana husika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…