kweli wajinga ndio waliwao, yaani utafikiri ni epidode ya "vitimbi"maanake miaka nenda rudi, story ni ile ile "oooh wajanja wamechangamkia dili, serikali itafanya nini?" lakini ndugu zangu nakwambieni ya kwamba ole wako uliepigia kura ccm alafu unalalamika jinsi hali ilivyo, umejitakia mwenyewe, cha kushangaza zaidi shuhudia uchaguzi ujao na jinsi ccm itashinda tena. Kuna matatizo ambayo sisi kama binadamu hatuwezi kwepa (mf ajali ya gari, kupigwa na radi nk.), lakini yapo yale ambayo ni uamuzi wetu tu, yaani umejirostisha (mf kutega shule, ukimwi, utawala wa ccm nk) kwahiyo kabla ya kupiga mayowe ya walahi mtumee, jiulize "hivi ni nini nimefanya kuchangia hili janga?"