TCRA: Yatoa neno kwa Vyombo vya Habari vinavyowatumia watangazaji wasio na Taaluma ya Habari

TCRA: Yatoa neno kwa Vyombo vya Habari vinavyowatumia watangazaji wasio na Taaluma ya Habari

Dida ana diploma au degree?!

Maana kwa mujibu Wa sheria Mpya waandishi Wa habari wenye certificate tu hawatakiwi mjengoni,,, wanaokuwa verified or justified ni wale wenye tu either degree (shahada) or diploma (stashahada)
Dida ana diploma.
 
Kuna vipindi vya umbea, matusi, kuchambana halafu unataka uwe na taifa lenye watu waelevu hii sheria imechelewa sana
 
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA(TCRA) YATOA ONYO KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUAJIRI WATANGAZAJI WASIO NA TAALUMA.

Mamlaka ya Mawasiliano nchini imetoa onyo kwa vyombo vya habari hususani redio na televisheni kwa kile inachodai kuwa vyombo hivyo vimekua na tabia ya kuajiri watangazaji wasio na taaluma hiyo.

Katika tarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo leo Septemba 14 imewataka wamiliki wa vyombo hivyo kuzingatia matakwa ya sheria na masharti ya leseni ya utangazaji kwa kuhakikisha kuwa wanaotangaza katika vyombo vyao wana vigezo vya kitaaluma kama waandishi wa habari.

Mamlaka hiyo imefafanua kuwa kwa mujibu wa sheria ya vyombo vya habari ya mwaka 2016 kifungu cha 19(1) kinaeleza kuwa kufanya kazi kama mwandishi wa habari pasipo kuthibitishwa kwa mujibu wa sheria ni kuvunja sheria na kwa mujibu wa kanuni ya 17(2) ya vyombo vya habari ya mwaka 2017 ili mtu athibitishwe kuwa mwandishi pamoja na mambo mengine anatakiwa kuwa na shahada au stashahada ya uandishi wa habari au inayohusiana na masuala ya vyombo vya habari kutoka chuo kinachotambulika kinachotoa elimu ya masuala hayo au shahada au stashahada ya masuala ya Vyombo vya Habari.

Kuwa na watangazaji wasio na elimu juu ya masuala ya habari na utangazaji kunapelekea kutendeka kwa makosa mengi ya kutozingatia miiko ya uandishi na utangazaji wa habari, hivyo kuwa kinyume na matakwa ya kifungu cha 7(2)(a)(iii) cha sheria ya vyombo vya habari ya mwaka 2016 kinachotaka vyombo vya habari kuzingatia misingi na miiko ya uandishi wa vyombo vya habari.

Aidha, Mamlaka imevikumbusha na kuvionya vyombo vya habari kuwa hatua zaidi zitachukuliwa, ikiwa ni pamoja na kutoza faini, au kufuta leseni ya chombo chochote kitakachokiuka masharti ya leseni, kanuni na Sheria.

Ikumbukwe kuwa mamlaka hiyo ilitoa taarifa kuwa mpaka kufikia mwaka 2021 Vyombo vyote vya Habari vinatakiwa kuwa na waandishi na watangazaji waliokidhi vigezo vya kitaaluma.

Kumekucha🤣🤣🤣 watoto wa mjini sijui wataishije maana vipindi vya burudani watangazaji wake wengi hata chuo baadhi hawajakanyaga ,
 
Hii kitu inanikumbusha sakata la vyeti vya bwana Bashite
 
Nadhani wangesema tu uwe na digrii au diploma yoyote lakini sio lazima iwe ya uandishi wa habari..maana mtu anaweza kuajiriwa kama mtangazaj na mchambuzi wa masuala ya siasa na labda ana digrii ya political science...mtu aliesoma journalism au mass comm anaweza kuchambua habari za uchumi au siasa vzr?
 
steve nyerere arudi mtaani akakusanye rambirambi, huenda kaka pascal mayala akapata ajira akaacha kutusumbua na kampeni za JF
 
Nadhani wangesema tu uwe na digrii au diploma yoyote lakini sio lazima iwe ya uandishi wa habari..maana mtu anaweza kuajiriwa kama mtangazaj na mchambuzi wa masuala ya siasa na labda ana digrii ya political science...mtu aliesoma journalism au mass comm anaweza kuchambua habari za uchumi au siasa vzr?
Wacha kuongelea professional za watu kirahisi rahisi namna hyo, kwahyo hao wanaosomea journalism utawaajiri ww, ofcz ur name reflects how shallow u r, sorry km ntakuwa nimekukwaza but uwe unafikiria kwnz.
 
Back
Top Bottom