TCRA yatolea ufafanuzi sheria ya umiliki wa laini moja iliyoanza kutumika leo

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2009
Posts
2,935
Reaction score
3,346
Sheria ya umiliki wa laini moja ya simu kwa kila mtandao imeanza kutumika leo Julai Mosi 2020 ambapo ndio siku ya kwanza ya mwaka wa fedha wa serikali.

Hata hivyo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa sheria hiyo haimzuii mtu kumiliki laini zaidi ya moja kwa mtandao mmoja, isipokuwa atalazimika kutolea ufafanuzi laini ya ziada, na kwamba lengo la sheria hiyo ni kudhibiti umiliki holela wa laini za simu na kudhibiti uhalifu.

“Kuna wengine wanasajili [laini zaidi ya moja] kwa ajili ya matumizi ya biashara au majumbani, hivyo huwezi kuwafunga kwa kuwaambia wamiliki laini moja,” amenukuliwa Msemaji wa TCRA, Semu Mwakyanjala wakati akizungumza na Gazeti la Mwananchi.

Kifungu cha 18 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, sheria ya usajili wa laini za simu ya mwaka 2020 inaeleza kuwa mtu anatakiwa kumiliki laini moja ya simu kwa mtandao kwa ajili ya matumizi ya kupiga, kutuma jumbe na huduma za intaneti.

Sheria hiyo inaeleza kuwa mtu atakayemiliki laini zaidi ya moja kwa mtandao kinyume cha sheria atatozwa faini ya TZS 5 milioni au kifungo jela kwa miezi 12 au vyote kwa pamoja.

Na katika kila siku ambayo laini ya ziada ilitumika mhusika atalipa faini ya TZS 75,000 kwa siku.

Aidha, sheria hairuhusu kampuni kumiliki laini zaidi ya 30 ambazo zitatumika katika kupiga, kutuma jumba au huduma ya intaneti. Endapo kampuni itakiuka sheria hiyo, itatozwa faini isiyopungua TZS 50 milioni pamoja na TZS 175,000 kwa kila siku ambayo laini za/ya ziada ilitumika.

Wananchi kupitia mitandao ya kijamii wameonekana kuilalamikia sheria hiyo ambayo baadhi wamedai kuwa inaminya uhuru wao.

Screen Shot 2020-07-01 at 17.52.41.png

Screen Shot 2020-07-01 at 17.53.07.png

Pia soma > Ukimiliki laini zaidi ya moja ya mtandao mmoja utalipa faini Tsh 5M au kufungwa gerezani kwa miezi 12 au vyote kwa pamoja kuanzia 1 Julai, 2020
 
"Hata hivyo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa sheria hiyo haimzuii mtu kumiliki laini zaidi ya moja kwa mtandao mmoja, isipokuwa atalazimika kutolea ufafanuzi laini ya ziada".

Hayo maelezo unaenda kuyatolea wapi?Tcra/police/kwny Co. Ya simu husika au?
 
Yaani hii ndio wenzetu wanaita "Undue Burden" on the citizen.
 
Wapuuzi sana sasa mbona kwenye sheria yenyewe hawajasema kama unatakiwa laini nyingine utolee ufafanuzi wa matumizi? Wakitaka kutunga visheria vyao vya hovyo wangekusanya maoni kutoka kada mbali mbali sio wanakurupuka kama "TAJIRI WA KIGOMA BROTHER K".
 
Ndiyo imetoka hiyo. Itakuwa inawalenga watu fulani fulani.
 
JoJiPoJi,

Ni aibu kwa TCRA kutoa majibu mepesi hivi. Wanatakiwa watueleze utaratibu wa kumiliki laini zaidi ya moja unafanyikaje.
Kama ni barua kwenda TCRA basi watoe template tujaze online na hard copy maisha yaendeleee.

Kitu kidogo ila wanafanya linakuwa jambo kubwaaa kutuvuruga wananchi.

I'm sure hata wabunge wa CCM waliopitisha huu wehu nao hawana habari na kitanzi walichojisetia.
 
"Hata hivyo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa sheria hiyo haimzuii mtu kumiliki laini zaidi ya moja kwa mtandao mmoja, isipokuwa atalazimika kutolea ufafanuzi laini ya ziada".

Hayo maelezo unaenda kuyatolea wapi?Tcra/police/kwny Co. Ya simu husika au?
Hawa jamaa wanapuyanga sana, kwahiyo wanataka watupangishe tena foleni?
 
Sheria ya umiliki wa laini moja ya simu kwa kila mtandao imeanza kutumika leo Julai Mosi 2020 ambapo ndio siku ya kwanza ya mwaka wa fedha wa serikali.

Hata hivyo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa sheria hiyo haimzuii mtu kumiliki laini zaidi ya moja kwa mtandao mmoja, isipokuwa atalazimika kutolea ufafanuzi laini ya ziada, na kwamba lengo la sheria hiyo ni kudhibiti umiliki holela wa laini za simu na kudhibiti uhalifu.

“Kuna wengine wanasajili [laini zaidi ya moja] kwa ajili ya matumizi ya biashara au majumbani, hivyo huwezi kuwafunga kwa kuwaambia wamiliki laini moja,” amenukuliwa Msemaji wa TCRA, Semu Mwakyanjala wakati akizungumza na Gazeti la Mwananchi.

Kifungu cha 18 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, sheria ya usajili wa laini za simu ya mwaka 2020 inaeleza kuwa mtu anatakiwa kumiliki laini moja ya simu kwa mtandao kwa ajili ya matumizi ya kupiga, kutuma jumbe na huduma za intaneti.

Sheria hiyo inaeleza kuwa mtu atakayemiliki laini zaidi ya moja kwa mtandao kinyume cha sheria atatozwa faini ya TZS 5 milioni au kifungo jela kwa miezi 12 au vyote kwa pamoja.

Na katika kila siku ambayo laini ya ziada ilitumika mhusika atalipa faini ya TZS 75,000 kwa siku.

Aidha, sheria hairuhusu kampuni kumiliki laini zaidi ya 30 ambazo zitatumika katika kupiga, kutuma jumba au huduma ya intaneti. Endapo kampuni itakiuka sheria hiyo, itatozwa faini isiyopungua TZS 50 milioni pamoja na TZS 175,000 kwa kila siku ambayo laini za/ya ziada ilitumika.

Wananchi kupitia mitandao ya kijamii wameonekana kuilalamikia sheria hiyo ambayo baadhi wamedai kuwa inaminya uhuru wao.

Swahili Times

photo_2020-07-01_08-17-23.jpg
 
Kwanini walazimishe laini 30 kwa ajiri ya kampuni? Kwanini sio 100 au 200? 30 kwa vigezo gani?

Hivi hawa jamaa huwa wanatumia kiungo gani kufikiri?
 
Hivi vitu vya ajabu sana wakati tunatumia kiholela hakuna finger print walikaa kimya nahapo ndo mtu alikua anaweza kufanya uhalifu Sasa tunafinger print mnaanza Visa mtu mzima anajitambua kuwa na lain mbili zinazo fanana hajakosea anamaana yake Hawa tcra hivi wanna nn mbona mnataka watanzania tuishi kama tupo kaburini mbona kila siku ni vikwazo au hamtaki tuwe namawasiliano acheni roho mbaya ukiona mkeo anatumia vibaya sio wote tuacheni
 
"Hata hivyo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa sheria hiyo haimzuii mtu kumiliki laini zaidi ya moja kwa mtandao mmoja, isipokuwa atalazimika kutolea ufafanuzi laini ya ziada".

Hayo maelezo unaenda kuyatolea wapi?Tcra/police/kwny Co. Ya simu husika au?
... halafu hayo ni maelezo ya huyo afisa wa TCRA aliyekuwa anahojiwa; sheria haitamki hivyo; haiko wazi kwenye hilo; haitoi hiyo provision! Wanaotunga hizi sheria sijui wanakuwa wamesinzia?
 
Yaani hii ndio wenzetu wanaita "Undue Burden" on the citizen.

Sure! Wanatuwekea mizigo mizito isiyo na sababu mkuu. Badala ya sheria kurahisisha maisha kwa walio wengi always ni vikwazo na usumbufu usio wa lazima. Sheria ilitakiwa ieleze very clearly mimi kama mwananchi nifanye nini. Anyway, labda kuna kanuni sijui nazo zinasemaje maana tumeletewa sheria tu hatuelezwi kanuni zinasemaje.
 
Wapuuzi sana sasa mbona kwenye sheria yenyewe hawajasema kama unatakiwa laini nyingine utolee ufafanuzi wa matumizi? Wakitaka kutunga visheria vyao vya hovyo wangekusanya maoni kutoka kada mbali mbali sio wanakurupuka kama "TAJIRI WA KIGOMA BROTHER K".
Exactly Mkuu! Sheria ilitakiwa iwe wazi bila kufichaficha baadhi ya mambo hadi sijui afisa gani atolee ufafanuzi! Sheria ya kipumbavu sana hii.
 
Kwanini walazimishe laini 30 kwa ajiri ya kampuni? Kwanini sio 100 au 200? 30 kwa vigezo gani?

Hivi hawa jamaa huwa wanatumia kiungo gani kufikiri?
Hoja muhimu sana hii. Fikiria kampuni kama Bakhresa & Co and the like! Hata mimi nimejiuliza sana hilo swali why 30? Sipati jibu.
 
Hivi vitu vya ajabu sana wakati tunatumia kiholela hakuna finger print walikaa kimya nahapo ndo mtu alikua anaweza kufanya uhalifu Sasa tunafinger print mnaanza Visa mtu mzima anajitambua kuwa na lain mbili zinazo fanana hajakosea anamaana yake Hawa tcra hivi wanna nn mbona mnataka watanzania tuishi kama tupo kaburini mbona kila siku ni vikwazo au hamtaki tuwe namawasiliano acheni roho mbaya ukiona mkeo anatumia vibaya sio wote tuacheni
 
Wananchi kupitia mitandao ya kijamii wameonekana kuilalamikia sheria hiyo ambayo baadhi wamedai kuwa inaminya uhuru wao.

Siyo inanyima uhuru tu bali ni sheria gandamizi.--- ni sheria isiyostahili kwa mwanadamu.
 
Back
Top Bottom