TCU kumbukeni Waziri Mkuu aliwaambia acheni kunyanyasa na kuonea Vyuo Vikuu Binafsi

TCU kumbukeni Waziri Mkuu aliwaambia acheni kunyanyasa na kuonea Vyuo Vikuu Binafsi

saigilomagema

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2015
Posts
4,683
Reaction score
7,222
Hii taasisi ya serikali inayosimamia vyuo vikuu nchini imekuwa na tabia ya kuonea, kunyanyasa vyuo vikuu binafsi. Kuna kipindi hasa miaka ya 2016 walifungia sana either chuo kabisa au baadhi kozi. Hii ilipekea taharuki kubwa sana nchini. Ilifungia matawi ya vyuo vikuu hasa kutokea nchi za Kenya na Uganda kama vile Jomo Kenyata University of Agriculture and Technology (JKUAT) na Kenyatta University (KU) vyote vya Kenya vilivyopo mjini Arusha. Matawi mengine yalikuwa Dar Es Salaam.

Chuo kikuu binafsi kupata ruhusa ya kuanzisha kozi mpya ili angalau ijipanue itasota sana, watakiwekea vigingi vingi sana hasa suala la staff, inajulikana hivi vyuo vinajiendesha kwa ada za wanafunzi kulipia kuanzia mishahara na matumizi mengineyo (OC) ya chuo. Shida hasa inakuja kwenye tafsiri ya equivalent qualifications, kwa mfano mtu ana MSc. in Management and Information Systems au MSc. in Information Technology, eti huyu hafai kufundisha programmes za informatics hata km first degree ni ya Computer Science au IT. Wao watataka first degree kwa mfano ktk Computer Science, Masters(Computer Science) na PhD (Computer Science) ili chuo kionekane kina right staff kufundisha kozi related to computer Studies. Hizi akili za hovyo kabisa utafikiri siyo binadamu.

Shida ya hawa watu wanajenga mazingira ya rushwa au shida yao ni nini. Au pengine wao wenyewe ni disqualified wanashindwa kuchambua qualifications za Staff wahusika. Kwanini wasichambue transcript waangalie zile core components? Ni watu wenye negativity kuhusu wenzao, wenye roho mbaya. Hawataki kuona hivi vikikua, waziri aliwaeleza kazi yenu si kufungia vyuo au kozi au kuzuia kozi mpya kuanzishwa ila kuvilea vyuo vikue.

Hayo siyo mambo watanzania wenzetu, tokeni ofisini mkajifunze hata kwa majirani zetu. Ruhusuni vyuo vikue
 
Back
Top Bottom