Hili jukwaa ni muhimu sana ndugu zangu,ni moja kati ya jamvi muhimu sana kwa walio masomoni na hata wahitimu waliopo mtaani kama nyie vijana.
Najua hapa form six mpo wengi tu mkisubiri kujiunga na Elimu ya juu.
Ila kuna sintofahamu imezuka miongoni mwenu japo siyo wote,hii tabia ya kuanzisha thread bila hata kufikiri,leo hii kuna zaidi ya thread kumi zenye maudhui ya aina moja !! Mtu bila kusoma thread tangulizi kujua kinachojadiliwa ili kama anatatizo alitue hapo but huyoo kupost mara sijui breaking news....tetesi na kadha wa kadha.
Jf inategemewa na wengi kama ndio chanzo chao cha habari za uhakika, kwa trend hii huko mbeleni watu watashindwa kuiamini sababu ya post kamq ya huyu mleta mada. Unaleta kitu then unaishia kutukanwa kama hivi hii haipendezi na sio dalili njema,mleta mada jifunze kuitumia jamiiforums( hii hata kwa wenye tabia kama yako) jf ni kisima cha Elimu itumie vyema.
Hawa mliowakuta kama wangeweka nyuzi za ajabu ajabu sidhani kama leo hii jf ingekuwepo hapa ilipo ! Acheni hizo,hapa hatushindani kama fb wangapi wame like na ku comment.
Kumbuka nyie ndio mnategemewa kuja kuweka threads zenye manufaa kwa UMMA siku za usoni,sijui kwa uandishi huu utasadikika vipi ?
Litumieni vyema hili jukwaa.
NB:
Huu ni ushauri tu sitegemei kuanzisha majibizano na mdau yeyote hapa jamvini.
Wasalaaaam.