Magu
Senior Member
- Jun 13, 2011
- 156
- 56
Ndg wana Jf kumekuwa na taarifa mkanganyiko mtaani (taarifa zisizo rasmi) kuwa vyuo vingi nchi hii vinatoa degree ambazo ziko chini ya viwango, hii inasababisha watu kutoleana maneno ya kukejeliana na kukashifiana kuhusu elimu zetu. Vyuo vinatolewa maneno machafu kutoa degree chini ya viwango ni Tumaini University, SAUTI, UDOM, TEKU, MZUMBE.
MZUMBE wanatuhumiwa kutoa masters ambazo zinaitwa njegere/maharage ya mbeya, Tumaini university degree ya sheria kutotambuliwa na waajiri na pia Masters zake kutotambuliwa na kutosajiriwa na TCU.
Je wadau ni sahihi kwa TCU kukaa kimya kwa nchi kuwa na elimu inayotuhumiwa kwa kiwango kikubwa namna hiyo?
Wadau pia naombeni tujadili ukweli wa tuhuma hizi kiundani ili kuwasaudia TCU kujua kama hawajajua au kusikia ili wachukuwe hatua stahili.
TCU chukuweni hatua au mtoe tamko kwa hizi tuhum, kama ni za ukweli bora mvifungie vyuo ambavyo vinatoa elimu chini ya kiwango na kama baadhi ya kozi hazisajiriwa inakuwaje zitolewe na nyie mpo?