Teak Wood Tree - Loan

Poa mkuu na kutumia kwa inbox number ya huyo sister, i hope atakuwa na contacts za huyo mteja.
 

Mkuu 1800, mitiki inastawi sana katika mikoa ya pwani,tanga na morogoro. Mikoa ambayo inajoto kiasi na mvua za wastani kulingana na ukweli kwamba mitiki huvumilia sana ukame na inatunza maji mengi sana.
Pia ni miti ambayo hukua kwa kasi ya ajabu kama utazingatia hatua za awali kuandaa shamba lako kwa kulitifua na trekta ili kuruhusu mizizi kupenya kwa urahisi. Ukizingatia hilo na ukadhibiti uchafuzi ufanywao na mifugo hasa ng'ombe pia moto, utastaajabu jinsi inavyokimbia katika ukuaji.
Ni mti ambao unavumilia sana ukame na nzuri zaidi huendelea kuchipua hata kama umekatwa na kubaki kisiki.
Nawasihi
 
Last edited by a moderator:
Issue ya ng'ombe na moto unadhibiti vp mkuu?
Tayari nishakutumia.
 
Issue ya ng'ombe na moto unadhibiti vp mkuu?
Tayari nishakutumia.

Utadhibiti ng'ombe kwa kuweka ulinzi hasa ukipata mtu aliyeoa na kuhusu moto ni kwa kupalilia mara kwa mara na kutengeneza barabara kuzunguka shamba. Pia ni mhimu sana kujenga mahusiano mazuri na wananchi wa eneo husika ili kuhakikisha ulinzi mbadala kwa waharifu wengine zaidi hasa wafugaji ambao ni sugu kwa uchafuzi huku mashambani. Mathalani kuingiza ng'ombe shambani, kukatakata miti kusiko na mpango etc.
Kadharika, miti ikishakuwa mikubwa zaidi unaweza kufuga mifugo michache kwajili ya malisho ili kusaidia zoezi la upaliliaji kadri watakavyokuwa wakila nyasi ndani ya shamba. Unaweza ukaona sasa ni jinsi gani ambavyo unaweza kulimudu shamba la miti kwani kadri ikuwavyo gharama za kutunza zinazidi kuwa chini zaidi.
 

large scale nikuanzia hekaringapi?..
 
Wakuu mi nina hekta 15 Hale-Tanga;- natafuta mnunuzi, sijui wanapatikana wapi? Miti yangu ina miaka 17. If you can direct me please!
 
Mkuu kindege534 nitumie namba yako PM. Ningependa kujua ulichoandika ni hekta 15 kwa maana ya ekari 37.5? Au umeandika hekta kimakosa kumbe ni ekari15?
Kama ina umri huo basi mi nakuja na wateja hapo Hale.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu vp ngombe/mbuzi wanakula majani ya mitiki napenda kufahamu. Pili kwa maeneo ya segera hii miti inastawi? asanteni
 
Wakuu vp ng'ombe/mbuzi wanakula majani ya mitiki napenda kufahamu. Pili kwa maeneo ya segera hii miti inastawi? asanteni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…