Team Ally Kiba na Team Diamond Platinums tujongee Hapa kuombana Msamaha kwa matusi tuliyotoleana.

Team Ally Kiba na Team Diamond Platinums tujongee Hapa kuombana Msamaha kwa matusi tuliyotoleana.

mockers

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2013
Posts
12,843
Reaction score
35,442
Heshima kwenu Wakuu.
Sina mengi sana , lakini naomba team mbili Hapo juu tuliokwaruzana na kuvunjiana heshima tufike Hapa tuombana msamaha na tuanze kutoa michango ya kuwajenga wasanii wetu kwa maslahi mapana ya muziki wetu.
 
Inawezekana tukawapandisha wote kuliko kutukanana kila siku kama watoto
Wewe unadhani ni wewe shabiki wenyewe wanaojiita wadau Wa muziki kuna mengi kuna watu wanataka kuwa miungu watu kwenye huu mziki kuna watu wanaona fulani ndio Bora ili maisha yao yaendelee kuwa Bora lazima wampige Vita mmoja Na mmoja wampandishe
 
ngoja nikae high table....niwe nawaangalia usoni ili nione kama nyuso zenu zitakuwa zinamaanisha yale mnayoyasema
 
Kipindi kile enzi zetu bado vijana wadogo ilikuwa ni rahisi sana kuomba msamaha ingawa ni neno gumu kutamka " naomba unisamehe sitarudia tena".
*vijana wa sasa hawawezi kujishusha na kuomba msamaha wa kweli sababu÷
-ubishi kila kitu wanajua
-masikini jeuri
-kama mbwai na iwe mbwai liwalo na liwe
-kupata unyonge na kudharaulika
**samahani ni neno lenye hekma na busara kubwa likitumika katika sanaa, siasa, michezo, mahusiano ya ndoa.
_Friends never say sorry..
 
Baada ya waliojiita team kiba kuamia kwa Darasa mmeona mtafute suluhu maana hamzungumziwi kabisa.
 
Mimi nashukuru Mungu sijawahi kumtukana mtu,ila kanuni yangu ukinitukana au kunikejeri sikuachi na ndio maana tokea niwe humu sijawahi kufungiwa.Ila mimi ndio naongoza kwa kutukanwa ktk jukwaa hili.
 
diamond in msanii wa kimataifa na huyo kibwabwa ni msanii wa kariakoo na vitongoji vyake
 
Wangeanza wamiliki wa timu hizo kwanza alafu hawa wengine watafuata nyayo
 
Back
Top Bottom