Team Ally Kiba na Team Diamond Platinums tujongee Hapa kuombana Msamaha kwa matusi tuliyotoleana.

Kusema timu kiba na timu diamond ni kumshusha diamond.. Ally bushman hana timu ana watu hawapungui kumi wenye akaunti fake tano tano ndo mnaleta upuuzi hapa..!! Timu kibakuli muwe na adabu na msanii wetu WA kimataifa na mkubali ukweli kuwa jamaa yenu hajui kuimba hata dimpoz mwenyew hamfikii..!! Naona sasa hivi mmehamia kwa darasa timu bushman.. Msanii wenu hajui kuimba..msanii tokea Cinderella bado habadiliki..
 
Umeandika vyema unaweza kuwa unatembea kisha ukampiga mtu kikumbo kibahati mbaya kisha kama ni muungwana unarudi na kumuomba msamaha japo nae anajua hukukusudia lakini neno linamfariji ila mpige mtu kumbo kisha uendelee na safari ugomvi wake si wa kitoto.
Tukirudi kwa vijana hawa bado umri unawaruhusu kwenda mbali zaidi kama wamoja kuliko kuwa na migogoro ambayo pengine haina kichwa wala miguu najua pana wadau humu wana nafasi ya kuwashauri kwa mustakbali wa sanaa yao.
 
Mtuombe msamaha na sisi Team Le Mutuz, maana mmetutukana sana kwa miaka yote hii.
 
Team Kibakuli ujinga wao ni kutokutaka kubali ukweli kwamba Diamond ndio jina la Mchezo. Wakiri kwanza hilo then tuendelee.
 
Mkuu umeongea maneno yenye hekma na busara sana.
 
good idea...nashukuru nishaamua kuachana na uteam nikawa nashabikia mziki mzuri

nimesamehe wote na mnisamehe pia
I don't hold any grudge...

one luv..
but I know kuna watu hawatachange tuwaombee wabadilike waondoe vinyongo vyote...!!
 
Hongera Mkuu kwa kuonyesha ukomavu wa akili na kukubali makosa yako. Wote hawa ni Watanzania wenzetu huwa nashangaa sana kuona chuki za kutisha dhidi ya kambi hizi mbili za washabiki wa Kiba na DP. Kwani tusiwapende wote na kufurahia mafanikio yao bila kutukanana na kuwadhalilisha wao wenyewe kwa kila namna!? Hivi baadhi ya Watanzania wamerogwa na nani?


Namuomba msamaha Daudi Mchambuzi nilikutukana kisa tofauti zetu nisamehe na kuanzia Leo nitamjadili Ally Kiba kwa lengo la kumjenga
 
Team za Kimasikin Maskin maskin iz

Wachache sana ndio wana ushabiki wa kwer

Kuna watu wana jua kesho na kesho Kutwa Mond na Kiba watapa4m Wap....??

Wakitoa Album zao hawa hawa mashabiki wanakimbilia ktk mitandao kudwnload

Wala hawana mpango wa kununua album zao
 
ni ngumu kupatana maana kuna watu wananufaika nazooo
Of course hiyo ni business ya watu.
But ninachojiuliza kwanini watu wagombane na kutukanana sababu ya ushabiki wa watu ambao hata hawajui kama tuna-exist? Let them quarrel/beef by themselves, but it does not have to affect our social morals and virtues. Watu wamekuwa kama vichaa sababu ya huu ushabiki.

Sioni haja ya kupatana kwenye ugomvi ambao hautuhusu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…