TEC yalaani Shambulizi Dhidi ya Padre Charles Kitima, yataka uchunguzi wa haraka na uwazi pasipo na upotoshaji

Dalton Elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
968
Reaction score
1,978
Baraza la Maaskofu Tanzania Limetoa wito kwa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania na vyombo vingine vya usalama kuchukua hatua za haraka za kuwabaini na kuwakamata wale wote husika na kuwakamata kwa ajili ya kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria

Aidha Baraza limeesa jeshi la polisi kufanya uchunguzi na kutoan taarifa kwa uwazi ili kurahisha mchkato wa kupatikana kwa haki




TAARIFA KWA UMΜΑ​

KUVAMIWA NA KUUMIZWA KWA KATIBU MKUU WA BARAZA LA MAASKOFU (TEC) - PADRE CHARLES KITΙΜΑ

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limesikitishwa sana na linalaani tukio baya la uovu la kuvamiwa, na kujeruhiwa kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Padre Charles Kitima, lililotokea tarehe 30 Aprili 2025 majira ya saa 4 usiku katika makazi na Makao Makuu ya Baraza la Maaskofu, Kurasini Dar es Salaam. Padre Kitima alipata majeraha makubwa na amelazwa katika hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es salaam. Tunawashukuru wote waliomsaidia na kumfikisha Padre Kitima hospitalini mapema na kwa madaktari na wauguzi wanaomhudumia mpaka sasa.

Wito wetu kwa vyombo vinavyohusika:

Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama kuchukua hatua za haraka za kuwabaini na kuwakamata wale wote waliohusika katika kupanga na kutekeleza uhalifu huu wa kinyama na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Aidha, uchunguzi wa tukio hili ufanyike kwa haraka na taarifa zilitolewe kwa uwazi na bila upotoshwaji wowote ili kurudisha imani na matumaini kwa watu wetu.

Soma Pia: Padri Kitima ashambuliwa na watu wasiojulikana. Inadaiwa hali yake ni mbaya


Tunashukuru mpaka sasa kwa ushirikiano mzuri tunaoupata kutoka Serikalini na kwa vyombo vyetu vya usalama. Pia tunawashukuru watu binafsi, taasisi za ndani na za kimataifa zinazoendelea kulaani na kutupa pole kwa tukio hili baya na la aibu kwa Taifa letu. Tunaomba Waamini na watu wenye mapenzi mema muendelee kumuombea neema ya uponyaji Padre Kitima, na pia kuliombea Taifa letu amani na umoja. Aidha, tunawaomba muwe na subira na uvumilivu wakati tukisubiri matokeo ya uchunguzi wa vyombo vinavyohusika.

Katika Kristo Mfufuka,

Askofu Eusebius Nzigilwa Makamu wa Rais - Baraza la Maaskofu Tanzania
1 Mei 2025
 
Nyie badala ya kuandamana mnalaani mkiwa maofisini? eti tunasshukuru taasisi na watu wanao endele kulaani...seriously??? ANDAMANENI, TUMIENI HILI GAP KUIFUKUZA CCM MADARAKANI.
 
Msifikiri mtalitumia Kanisa Katoliki Tanzania kwa maslahi yenu. Huo ni ujinga na kujilisha upepo. Hata Askofu wa Katoliki anaweza akafa kwa kushambuliwa na nchi ikabaki salama zaidi ya kabla hajafa huyo Askofu. Usiichezee Mama Tanzania!!!
Tuna safari ndefu sana ya kuishi na watu kama wewe..!!
 
Msifikiri mtalitumia Kanisa Katoliki Tanzania kwa maslahi yenu. Huo ni ujinga na kujilisha upepo. Hata Askofu wa Katoliki anaweza akafa kwa kushambuliwa na nchi ikabaki salama zaidi ya kabla hajafa huyo Askofu. Usiichezee Mama Tanzania!!!
Mkuu unaongea ni kama vile ndani ya kanisa hakuna waumini ambao ni CCM au Chadema.Waumini wa kanisa katoliki nao ni watanzania kama wewe inawezekana tunatofautiana kiwango cha ujinga tu.
 
Lengo la Serikali ni kutokutii mawazo ya watu wengine.Kazi yao ni kumlinda mama Samiah kwa namna yoyote ile bila kujali nani anaumia.
 
ni muhimu kanisa kua wastahimilivu na wenye subra,
ni vyema polisi wakapewa fursa na nafasi ya kufanya kazi yao kwa uhuru
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…