Ukweli ulio wazi Berkane "quality" yao ipo juu kuliko Simba. Lakini hiyo bado haifanyi kuwa Simba hawezi kubeba ubingwa. Mimi kwa upande wangu kuna mambo ambayo nayaona wazi iwapo Simba itaamua kuyafanya basi sio ajabu wao kushinda na kubeba kombe.
1. Hizi mechi sio za maonyesho kwa hiyo waache upuuzi wao wa kujifanya Barcelona na kutaka kila mpira lazima waanzie nyuma au warudishe nyuma na hasa wanapokutana na timu inayokabia juu na yenye kasi kama Berkane badala yake wacheze "direct football" . Nilitoa angalizo hili hapa JF kabla ya mechi ya kwanza na kweli lilitokea na kusababisha goli la pili. Na kwa kasi ile ya Berkane wakirudia tena upuuzi wao wa kuanza mpira nyuma wataadhibiwa kwani beki za Simba wakipigwa presha ile ya unatoa hutoi hawawezi kuhimili. Kikubwa mpira unatakiwa kwa muda mwingi uchezewe katikati na kwenye goli la Berkane na si vinginevyo na mabeki wajulishwe kuwa kubutua sio kosa kwenye mchezo wa mpira wa miguu.
2. Fowadi fowadi fowadi inahitjika kuwa na utulivu sana. Hili ni tatizo kubwa sana pale Simba. Kwenye mechi kama hizi nafasi chache sana zinapatikana kuliko kwenye ligi yetu na ni lazima zitumike kwa usahihi. Napata sana shida kuielewa fowadi ya Simba kwanini hawakupata hata goli moja ugenini wakati walipata nafasi zaidi ya moja ya wazi. Na kama ile aliyopata Ateba kutoka kwenye krosi ya Kapombe badala apige kichwa cha kuchumpa yeye anataka afunge kwa miguu. Na mbaya zaidi alipoupata ule mpira Ahoua badala ampe Kibu aliyekuwa kwenye nafasi nzuri yeye anataka afunge mwenyewe kwa ubinafsi wake.
3. Mipira iliyokufa/kona. Hili ni jipu lingine pale Simba. Timu inatafuta goli wachezaji wamejipanga kwenye goli la timu pinzania halafu eti mchezaji anaanza pasi fupi akipigwa presha anarudishwa mpira nyuma mpaka unafika kwa Camara. Na Camara mwenyewe naye akirudishiwa akipigwa presha na yeye anabutua mbele sasa hiyo ni akili au matope maana unaua shambulizi ambalo linaweza kukupatia goli halafu unarudisha mpira nyuma ukabutuliwe na kipa. Na kumbuka kuwa huo mpira unaobutuliwa na Camara unakuwa hauna macho na hata wale mabeki waliongezeka kwenye goli la timu pinzani wanakuwa wameshaondoka kurudi kuzuia.
4. Kuna wakati timu pinzani inaamua kubaki nyuma ili wazuie tu. Utaona benchi la ufundi linaamua kupunguza beki au kiungo na kuongeza washambuliaji kule mbele kitu ambacho ni sahihi kabisa kiufundi. Lakini cha kuchekesha ni kuwa badala Simba sasa kupeleka mipira kwa wingi na kwa haraka kwa washambuliaji ili kulazimisha makosa kwa mabeki wa timu pinzani na hasa ukizingatia timu imeshakuwa na namba kubwa ya washambuliaji lakini bado utashangaa Simba wanaanza "back pass" zao mpira unaanza kwa kipa unaguswa na mabeki wote wale nyuma hata mara mbili mbili wakati fowadi inasubiri na dakika zinazidi kuyoyoma. Kwa hili sijiwahi kulielewa benchi la ufundi la Simba. Na benchi la ufundi kama linaamua kuingiza mshambuliaji wa ziada halafu mipira haifiki mbele kwa haraka basi inakuwa haina maana yoyote.
5. Mwisho na la muhimu sana ni kuwa kwa sababu "quality" ya Berkane ipo juu na kasi yao ipo juu japo hupungua kadri mchezo unavyoenda basi lil Simba waweze kuwadhibiti hao jamaa ni kucheza kwa "jihad" tu mwanzo mwisho. "Jihad" ya kujitoa nguvu, jasho na damu ndio itawapa Simba ubingwa si vinginevyo kwani kiufundi jamaa wapo vizuri sana. Na kubwa zaidi litakalowasaidia ni kulazimisha lazima magoli yatokee kwa njia yoyote ile na hili linawezekana tu iwapo wachezaji wenye kwa wenyewe watahamasishana.
Ni mtizamo tu.