TECNO kutwaa tuzo ya simu pendwa baada ya kuishinda Samsung

TECNO kutwaa tuzo ya simu pendwa baada ya kuishinda Samsung

Shadow7

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
24,606
Reaction score
39,289
Utafiti wa soko la teknolojia, uliofanywa na Kampuni ya utafiti ulimwenguni inayojishughulisha na bidhaa katika tasnia ya teknolojia ya vyombo vya habari na mawasiliano ya simu. Mwishoni mwa mwezi wa nne wametoa report ikionyesha kuwa kampuni ya simu TECNO imechukua nafasi ya kwanza kama simu bora Afrika kwa mwaka 2020 baada ya kuipindua kampuni ya simu Samsung na hii ni kufuatia uzalishaji wa simu za TECNO kuwa na viwango vya kuridhisha na kwa bei rafiki.

IMG_20210421_141816_424-scaled.jpeg
Rekord za shirika la usafirishaji wa simu janja Afrika 2020.
TECNO imefanikiwa kuwa kinara kufuatia anguko la asilimia 6.7% katika usafarishaji wa simu janja barani Afrika mnamo mwaka 2020. Uharibifu mkubwa ulifanyika katika nusu ya kwanza ya mwaka kwa sababu ya usumbu wa usambazaji uliosababisha na COVID-19, nakupelekea uhitaji kuwa mkubwa katika nusu ya pili.

Akizngumza juu ya mienendo ya soko, Mchambuzi Muandamizi Yang Wang alisema, kuangalia mwaka mzima soko la simu janja Afrika katika mikoa yake lilifanya vizuri lakini haikuweza kupigana na uharibu ulioletwa na COVID-19.

Robo ya pili ya mwaka 2020 ulikuwa mgumu zaidi baada ya uhitaji kuwa mkubwa lakini nchi nyingi zilikuwa zinapitia sheria ya kujifungia ‘lockdown’. Usafirishai wa simu janja wakati wa robo ya pili ulisababisha kushuka kwa asilimia 27%.

tttt.png

:Rekord za shirika la usafirishaji wa simu janja Afrika 2020.


Wang aliongeza, vizuizi vilianza kushuka mwezi Julai. Mahitaji yalifuata vivyo hivyo na kuongezeka kwa shughuli za uendelezaji, hata wakati kesi za COVID-19 zilipopanda juu kuelekea msimu wa ununuzi Christmas. Robo ya 4 kwa mwaka 2020 ilitoa faida ya asilimia 1.5% kwa maeneo ya robo bora zaidi kwenye rekodi.

Kulingana na report, TECNO ilikuwa namba moja katika mwaka 2020 licha ya kuwa soko la simu liliyumba barani Afrika kutoka na janga la COVID-19 hali ilipoanza kuwa shwari TECNO ilifanya vizuri sokoni kutokana na uzalishaji wa simu bora kwa bei rafiki.

TECNO iko tayari kupata faida zaidi kwa 2021. Samsung imeona soko lake likishuka kutokana na mvurugiko wa usambazaji wa mapema mwanzoni mwa mwaka, TECNO imekuwa kwa kasi barani Afrika na kufikia hadi nchi 60 na zaidi barani Asia, Latini America na Middle East katika miaka ya hivi karibuni huku lengo lake kuu likizingatiwa kwa uendaji sambamba na teknolojia katika bidhaa mpya na kufikia vijana zaidi.

Mabadiliko makubwa yameonyeshwa na TECNO CAMON na TECNO Spark Series zilizozinduliwa mnamo mwaka 2020 na kuzingatia teknolojia katika mfumo wa camera.

 
Uzuri wameweka wazi kuwa moja ya sababu ni Corona.

Umetoka kupigika kiuchumi baada ya lockdown, Bila shaka utatafuta cha bei nafuu.

Wapinzani wengi(Samsung, iphone, Nokia, Google n.k) walikua ndio kwanza experience lockdown hivyo nguvu kazi ilipungua viwandani na pia hakukua na Shipping au ilikua ndogo sana huku Tecno akirahisisha zaidi kwa kua na kiwanda africa.
 
Kampuni ya tecno imebamba sana kitaa lakini humu haina sifa

Humu kila member anasema anatumia iphone

Watu wa humu wengi wanamaisha ya kuigiza kwa kuandika andika tu,wanajifanya matawi alafu unamkuta kwenye uzi unaohusu ugumu wa maisha mtu wa matawi anacomment"nimewekewa kufuli na maza house kwasababu ananidai kodi ya miezi minne sijui ntalala wapi"
 
Swali Kwa Mtoa Mada.
Umekwenda Dukani Kununua Simu Ukakuta TECNO na SAMSUNG Zenye Uwezo Unaofanana Zinauzwa Bei Moja Wewe Utanunua Simu Gani?.
 
katika kampuni ambayo ni uchafu tecno na itel yani hawa watu kama ni mfanya biashara kuanzia vifaa vya simu ,kuuza simu na kutengeneza simu basi jua utafirisika yani simu zao ni kama sahani ya kulia na kutupa zile za sheree uswahilini.

siri
•simu hizi azina mlolongo kila siku toleo jipya kilicho ongezeka hakuna mpaka inafikia ujui nani mwenye simu gani.

•ulinzi ni ziro kabisa hata ukiibiwa ukienda polisi ukisema ni hizo simu polisi hana kwambia hakuna jinsi.

• kwa wauza simu wenye maduka unaweza kuanguka maana umeleta leo hii kesho inakuja nyengine,pili kampuni hii inauza watu wakauze ila cha kushangaza na yenyewe inauza kwa bei ya chini.
 
Watu wa humu wengi wanamaisha ya kuigiza kwa kuandika andika tu,wanajifanya matawi alafu unamkuta kwenye uzi unaohusu ugumu wa maisha mtu wa matawi anacomment"nimewekewa kufuli na maza house kwasababu ananidai kodi ya miezi minne sijui ntalala wapi"

usiamini kila andiko la humu.

hata hilo la kufungiwa usilitilie maanani.
 
katika kampuni ambayo ni uchafu tecno na itel yani hawa watu kama ni mfanya biashara kuanzia vifaa vya simu ,kuuza simu na kutengeneza simu basi jua utafirisika yani simu zao ni kama sahani ya kulia na kutupa zile za sheree uswahilini..

[emoji38][emoji38]hata mwanaume na akili timamu,ukiishaonekana unatumia hiyo brand watu wanapoteza umakini na wewe.

mtu unatoa laki 350 unachukua tecno[emoji16]kweli!!!!
 
Back
Top Bottom