Uchaguzi 2020 TEF yamaliza Mgogoro wa TBC na CHADEMA, wapeana Mkono

TBC Waache tabia yao mbovu. Wakiwa kwenye mikutano ya wapinzani hawaonyeshi uwepo wa watu wanaosikiliza hizo hotuba tofauti na mikutano ya CCM
 
Daah yaani hii tume ya uchaguzi imeona hili la TBC na CDM ni la muhimu sanaaaaa kuliko issue ya msingi ya kukatwa kwa wagombea na wagombea wa chama kimoja tuu kupita bila kupingwa???
 
Huko ni kupoteza muda. Hao wajinga wa tbc wao waendelee tu na kutangaza kampeni za ccm maana ccm ndio inawalipa mishahara.
 
Naona TBCCM wanataka umaarufu kduniani kwa kurusha habari za Chadema. Chadema haibabaishwi kibwege, wamehangaika kuiua na kuitabiria kifo imeshindikana. Sasa wanataka suluhu mezani hata hivyo hatuwahitaji. Wameona I.T.V. ilipo rusha mahojiano na Tundu Lissu Dunia nzima imeangalia wamepata kiwewe ghafla.
 
Waoneshe mikutano 5 mfululizo ya Lissu bila kukata
 
Heri ya mpatanishi. Ila TBC wajirekebishe.
 
kwani bila tbc siasa hazifanyiki? hakuna haja ya suluhu wao wafanye kazi za Ccm..chadema wameanza udhaifu sasa
 
Si mlisema hamuombi samahani? Imekuaje tena? Mmeona mambo hayaendi?
Unajua kusoma au mihemko ya taarabu na mipasho ya TOT imekujaa? JUKWAA LA WAANDISHI WA HABARI NDIO LILILOWAKUTANISHA. Wigwaga?
 
Muda aliopoteza Mbowe kwenda kupatana na TBC bora angeutumia kwa kufanya jambo jingine, kama Mimi ni muongo basi mtasubiri sana.

Mmoja wa wagombea wa chama kimojawapo ndiye aliyewatuma TBC wawahujumu CHADEMA kwa makombora yanayorushwa na mzee baba sidhani kama yataruhusiwa kupaa angani.

Mfano kwa waliofuatilia kampeni za CHADEMA jana sidhani kama zilirushwa hewani na TBC.
 
Jana kwenye Mkutano wa uzinduzi wa kampeni za NCCR-Mageuzi, kila Mbatia na Maganja walipokuwa wanatema cheche kuhusu upendeleo wa Tume ya uchaguzi na uharamia unaofanywa na serikali hususani kipindi hiki cha uchaguzi hao TBC wakawa wanafanya ile mnaita censoring, na kucheza nyimbo za uchaguzi. Kweli naunga mkono hoja, hayo mapatano hayatadumu hata kidogo
 
Hao ni ccm b.
 
Kiukweki nafasi ya Mbowe angeipata Heche..unajipendekeza kwa bwanyenye Hilo ili iweje? Aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…