Tegeta, Dar: Maafisa wa TRA washambuliwa na wananchi kwa mawe

Tegeta, Dar: Maafisa wa TRA washambuliwa na wananchi kwa mawe

Mnyenz

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2014
Posts
2,933
Reaction score
8,112
Gari ya serikali namba STL 9923, Usiku huu imeshambuliwa kwa mawe na wananchi wenye hasira butu, na watumishi waliokuwemo ndani wameumizwa.

Chanzo cha kizaa zaa hicho inasemekana hilo gari la serikali lilikua linaifuatilia gari nyingine ndogo aina ya BMW.

Baada ya kufika maeneo ya tegeta kwa ndevu, ile gari ya serikali ika buloku ile BMW.

Wananchi walipotaka kujua kulikoni, maana stori za utekaji zimekua nyingi, jamaa wakajitetea wao ni watumishi wa serikali kitengo cha T.R.A na wapo kazini wakitekeleza majukumu yao.

Basi bwana, katika vuta nikuvute, Wananchi wakahoji, kama mpo kazini mbona usiku? Na tena bila escort ya polisi mwenye gwanda?

Jamaa walipoona Wananchi wamekaza na wanazidi kuongezeka(bodaboda walipaki kwa mbele na nyuma ya cluza hilo la serekali) ikabidi waliondoe gari kwa nguvu na hivyo kuishia kugonga bodaboda zilizokua zimewabuloku.

Wananchi kuona hivyo nao wakaanza kutimiza wajibu wao.

BADO HAIJADHIBITIKA KAMA NI KWELI WATEKAJI AU NI WATUMISHI

Hii stori mwenyewe nimekuta imeshatokea msije kunitafuta mimi ni raia mwema na ninampenda rais Samia.

Pia Soma: Ufafanuzi kuhusu shambulio la gari la watumishi wa TRA eneo la Tegeta, Dar es Salaam
20241205_221421.jpg
20241205_221858.jpg
20241205_221355.jpg
 
Back
Top Bottom