Nasikitika sana kwa kweli,, inauma sana.
Waliosababisha natamani kama walifanya kwa makusudi ili kutukomoa basi wawajibishwe. Ni mzigo mkubwa sana kwa walipa kodi kulipa vitu visivyoeleweka.
Naamini kabisa uongozi uliopo madarakani utafanya kila liwezekanalo kuondoa mzigo huu usiwaangukie walalahoi.
Hela yote hii kama ingewekezwa kwenye elimu ingejenga shule nyingi sana, ingeingizwa kwenye afya ni vijiji vingi vingepata zahanati na madawa bure kabisa.
Ingeweza hata kuingizwa kati ya viwanda vilivyokufa na kufufua kimoja wapo na tukapiga hatua moja mbele.