Tegeta Escrow: TANESCO yashindwa kesi dhidi ya IPTL. Yaamriwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 320!

Tegeta Escrow: TANESCO yashindwa kesi dhidi ya IPTL. Yaamriwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 320!

Ngoja tusubiri mkuu atasema nini? maana ninavyomjua.IPO namna.
 
Inasikitisha mno manake kila kesi Serikali inashindwa tatizo liko wapi?
 
Hiyo ndo ccm wapiga dili wao nawao hao hao wanasema wanazui ufisadi maajabu
 
Haya madai ni tofauti na yale ya DOWANSI ambayo tulitakiwa tulipe mabilioni tukajaribu kupiga vikelele kama kawaida yetu tukaishia njiani,wamerithishana au hii ya IPTL ni new brand?Kweli sisi ni viumbe wa ajabu.
 
Nasikitika sana kwa kweli,, inauma sana.

Waliosababisha natamani kama walifanya kwa makusudi ili kutukomoa basi wawajibishwe. Ni mzigo mkubwa sana kwa walipa kodi kulipa vitu visivyoeleweka.

Naamini kabisa uongozi uliopo madarakani utafanya kila liwezekanalo kuondoa mzigo huu usiwaangukie walalahoi.

Hela yote hii kama ingewekezwa kwenye elimu ingejenga shule nyingi sana, ingeingizwa kwenye afya ni vijiji vingi vingepata zahanati na madawa bure kabisa.

Ingeweza hata kuingizwa kati ya viwanda vilivyokufa na kufufua kimoja wapo na tukapiga hatua moja mbele.
Ndiyo hivyo sasa mdau hiyo pesa inaenda kwa wajanja wenye uchungu na nchi yao wakafaidi,tuliachia nyani shamba na sasa tunavuna mabua.Hawa wataalam wetu wa mikataba sijui hata walikua wapi mikataba kandamizi km huu unafanyika?
 
Mkuu sijui atakuja na lipi maana kesha sema hajaribiwi na watu wanaendelea kumjaribu, kuna mwingine alisema anadai akaambiwa halipwi ng'oo, waache kumsumbua "hapa kazi tu" sio madai tu.
 
Viongoz wa serikali na ccm ndio wanaonufaika na hiyo iptl...

Haiwezekani iptl walipwe pasipo kutoa huduma yoyote...

Tanesco inakusanya mapato kwa raia na pesa hizo kulipa wajanja wachache ifike mwisho kwa kuvunja mkataba na iptl..
 
Kama mnakumbuka katika ile kashfa ya ESCROW iliyokuwa ikishughulikiwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali enzi hizo ikiongozwa na Zitto na Marehemu Deo, waliibana Serikali kwa nini imeruhusu uchotaji wa fedha za Escrow kumlipa Harbinder Sing wa IPTL wakati mgogoro baina ya TANESCO/ IPTL na standard chartered bank Hong Kong ulikuwa haujamalizika.

Sasa Katika hukumu ya mahakama ya usuluhishi Benki hiyo imeshinda na TANESCO wanatakiwa kulipa zaidi ya bilioni 300. Fedha za Escrow akaunti zimeshatoka na kalipwa Sing na mafisadi wengine serikalini. Serikali ilipuuza Bunge leo mtanzania ndiye ataumia kwa kuongezewa gharama za umeme ili kulipa déni hilo.

Na la kuchekesha zaidi, Serikali ya awamu ya tano inamuogopa sing na wanaendelea kumlipa kila mwezi huku aliwaibia fedha za ESCROW. Mapambano ya ufisadi yamekuwa selective kwa kulipa visasi kwa watu badala ya kupambana na mifumo ya kifisadi kama ya IPTL.
 
Ngoja tusikie kauli ya kaka Yohana, kuwa hatutalipa!! Si alishwahi kusema hivyo hapo nyuma
 
Waliotufikisha hapo wanaeleweka wachukuliwe hatua.
 
Back
Top Bottom