Tegeta Escrow: TANESCO yashindwa kesi dhidi ya IPTL. Yaamriwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 320!

...nashukuru kwa hii ruling..sasa waliolipa ule mzigo wa escrow warudisheee....maana imedhihirika pesa ililipwa kwa makosa....na ndiyo inadaiwa sasa....pesa waliyolipwa PAP na VIP kisanii ilikuwa makosa makubwa....maana hawakuwa sehemu ya mkataba/makubaliano ya kufungua escrow account....

....tulipiga sana kelele kipindi kile...sasa ruling imetoka....pesa za escrow waliobebeshwa warudisheeeeee.....
 
Haki ya MUNGU nimekumbuka kisa cha mchimba mashimo huingia mwenyewe, Iptl na washirika wake walipe ati, eeebbooo!!
 
Mnatamani sana Serikali ipandishe bei ya umeme ili muwe na ajenda majukwaani. Mmeula wa chuya. Hilo halitarokea kwa utawala wa Rais Magufuli
Lizaboni...wakati mwingine weka utaifa mbele. Sio kila issue unafanya ya kisiasa. Hapa tutaumia sana kwa upuuzi wa watu wachache wenye tamaa. Pesa itakayolipwa ingetumika kwenye miradi ya maendeleo. Kwa hali hii maendeleo ya uhakika yatakuwa madogo. Ni lini jinamizi ili litatutoka (IPTL)
 
Sasa ni wakati wa Rais Magufuli kwenda Stanbic kuwatafuta wale wanaosemekana waliobeba pesa kwenye masandarusi na magunia ili wafidie hii gharama ......!!
 
Kwa akili yako unamuona ni nani wa kurudisha hizo pesa? Acha tuendelee kukamuliwa kwenye bili ya umeme usishangae ile service charge ya kila mwezi ikarudi tena
 
Kama vipi Ozeh achapishe hela awalipe hao jamaa . Maana alihaidi kuchapisha hela..
 
Reactions: PhD
Inaumiza sana I wish wote waliohusika kusaini mkataba huu(kama ni Watanzania na walizaliwa Tanzania) kwa namna moja au nyingine washitakiwe kwani ni uhujumu uchumi naamini mtu mzalendo aisengeweza kukaa kwenye meza moja na hao matapeli na kusaini huu mkataba sad.
 
Kuna wakati natafakari sana hii nchi yetu halafu sipati jibu hii pesa iliwekwa escrow kwa ajili ya,kumlipa atakayeshinda kesi sasa kiherehere cha kuitoa na kuigawa ilikuwa ni cha nn? Aliyeidhinisha pesa kutolewa alipe hilo deni
 
Haya madai ni tofauti na yale ya DOWANSI ambayo tulitakiwa tulipe mabilioni tukajaribu kupiga vikelele kama kawaida yetu tukaishia njiani,wamerithishana au hii ya IPTL ni new brand?Kweli sisi ni viumbe wa ajabu.
Hii ni tofauti kabisa na dowans Mkuu kule wanapiga na huku wanapiga piga note kote
 
Bunge liliazimia serikali isiendelee kulipa IPTL na ile mitambo itaifishwe kwa nn hili halijufanyika??
 

Tujiandae kwa kipindi kirefu cha total black out kama sio mgao usio na ukomo!
Wale wa milioni 10 za mboga watakuwa wanachekelea kichinichini!!!
 
Achana na Lizaboni kama hutaki kupata presha!!
 
Itabidi wazilipe wenyewe,haya mambo ya watu kula hela halafu sisi tulipishwe hatuyataki.

Kweli kabisa sasa hivi gharama za umeme zitaanza kupanda. Walituondolea capacity charge sasa watarudisha tena.
Au tutaambiwa tuendelee kulipa kodi mbalimbali ili kufidia madeni ya kizembe kama haya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…