Tegeta Escrow: TANESCO yashindwa kesi dhidi ya IPTL. Yaamriwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 320!

Tegeta Escrow: TANESCO yashindwa kesi dhidi ya IPTL. Yaamriwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 320!

Kalasinga ni mtu wa kupull string behind the scene!katupatia kweli
nilipigia mistari eneo la rweyongeza advocates firm
Sasa, huu uzalendo unaopigiwa upatu kwenye kila jukwaa ni upi? Au ni ile sala ya mtakatifu shetani ya fuateni niyanenayo, matendo yangu niachieni? Nitakuwa wa kwanza kuishangaa hii serikali ya kuhubiri uzalendo na nitakuwa wa nwisho kuamini kushtakiwa kwa wahusika wote wa escrow katika mahakama mpya ya mafisadi.
Laiti mamlaka ya kuwashtaki wahusika wote na kuchagua majaji wazalendo w kuisikiliza kesi ningelipewa mimi, aminini ningefukua makaburi yote kuusaka ukweli na nisingelikuwa na simile. Mbona wangekuwa na magereza yao wenyewe kama ya guantanamo! Ni wakati wa rais kuwaonyesha wanyonge kile anachokisimamia na kukihubiri na au awalk talks zake katika hili ili liwe funzo kwa wanaofanyia matumbo yao.
 
Tanzania inayokusanya Trillion 1 point something kwa kila mwezi. Kulipa wafanyakazi wake Kwa kila mwezi ni takribani Billion 570. Deni la Taifa lapanda mpaka kila kukicha hadi Trillion 50. Na Serikali kuilipa IPTL zaidi ya Billion 300 jamani naombeni tujadali haya yaliyoko mezani. Ahsanteni [emoji120]
 
Ngoja tuone.
Tunakoelekea tutaanza kula nyasi.
Nchi ya viwanda
 
Tanzania isipo kuwa na vyanzo vingine vya kupata hela mbali na kodi haitakaa ipige hatua maendeleo tutaendelea kuyaona kwa wazungu tuu.
 
Hili zigo tunalo tu, tutake tusitake, ongezeni bei ya umeme ili tulilipe tu, maana tukizidi kukata rufaa ndio deni linazidi kusonga. Walio saini kwa niaba ya Jamhuri wapo wametuliaaa wanacheki muvi linavyotupelekesha.
 
Hamkujua ccm ni ileile,hapa hakuna viwanda wala nini ni kulipa madeni tuuu!
 
Hiyo ndio agenda yao kama taifa hiyo SCB-HK parent company ni SCB-UK wao wanachotaka watambulike kama wamiliki wa IPTL balozi (wa UK) keshatumia nguvu sana kulazimisha hii agenda na wanapofungua kesi za madai huko wanafungua kama wamiliki wa IPTL ndio maana mahakama inaweza toa hizo ruling. Na hakuna anaetaka kujua their legal ownership huko wanapofungua.

Ata wewe kesho ukienda kufungua partnership company kuna vigezo vyake vinavyokutambulisha wewe na huyo partner mwingine huko BRELLA kupitia partnership deed, mfano how partnership comes to an end other than in natural legal aspects kama death, each partners rights; etc with what was drafted in the partnership deed.

Sasa ikitokea mmbia mwenzako kaenda kuchukua mkopo kwa jina la kampuni (which is disputable) halafu baadae huyo mdeni anadai wewe aupo tena na yeye kutumia deni ndio mmiliki mpya. Wewe si utasema hapana nipe deni nilipe mimi sikutambui wewe na wala sheria aimtambui kwenye deed of ownership. Hapo ndio mzozo wa umiliki wa IPTL ulipo mahakama imeamua kwakuwa Rugemalira anatambulika kama mmoja wa mmbia na karidhia kuuza partnership rights zake kwa PAP kwa hivyo PAP ndio mmiliki mpya.

Pamoja na hayo mahakama pia imemtaka PAP kama mmiliki mpya wa IPTL akija mdeni wowote wa IPTL au TANESCO amalizane nae. Wao IPTL awaja kataa deni lilioachwa na mmbia mwingine na wako tayari kulilipa isipokuwa mdeni ataki malipo ya deni yeye anachotaka ni umiliki kamili wa IPTL kwa vigezo gani vya sheria ndio ataki kuja Tanzania anakimbilia huko kwa wazungu wenzake.

TUSISINGIZIE WAZUNGU MAKOSA YAKO KWA UONGOZI MBAYA NA WAKITAPELI. NANI ALIYETOWA PESA KUTOKA KWENYE ACCOUNT YA TEGETA? SIO WAZUNGU. NA HIZO PESA ZILIGAWANISHWAJE? MAJINA YA WAKINA CHENGE, TIBAIJUKA NA WENGINE SELIKALINI YALITAJWA, LAKINI KUNA MAJINA MENGINE MPAKA SASA YAMEWEKWA SIRI. SASA SERIKALI INABIDI IWAAMBIE WANANCHI PESA ZA ACCOUNT TEGETA ZIRILUHUSIWA VIPI KUCHUKULIWA KWENYE ACCOUNT NA ZIKAGAWANYWA KWA WATU WENYE VYEO SERIKALINI NA WAKATI KESI YA MADAI INAENDELEA?. JAMANI PENGINE WAKUBWA ZETU WANAONA WATANZANIA WAJINGA, LAKINI SIO WAJINGA, WATANZANIA WANAPENDA AMANI. WATU WALIOTUMIA HIZI PESA, KUMBUKENI WAKATI MNAKAA MEZANI NA FAMILIA ZENU MUKILA WATANZANIA WENGINE WANALALA NJAA KWA KUWA MUMEWAZUDURUMU CHAKULA CHAO KUPITIA KWENYE WIZI HUU. MUKIENDA KANISANI, AU MISITIKINI MUNGU MUNAYEMUOMBA NA ALIYEWAUMBA NI YULE YULE ALIYEWAUMBA MUNAOWADHURUMU. NA KITU CHA MWISHO NI KWAMBA HAKUNA PAMOJA NA WIZI HUU WA KIMACHAMACHO, LAKINI HAYO MAJUMBA MAKUBWA YA WIZI MWISHO WAKE NI KABURI.
 
Waliofanya makubaliano na mikataba ya namna hiyo ni wasomi wa nchi hii, adhabu yao ni kutaifishwa kila walicho nancho na familia zao, na wanastahili KUNYONGWA hadi kifo.
 
Hilo lilihojiwa sana wakati wa like sakata lakini majibu yalikuwa ya kisiasa majibu halisi ndio haya tulipe zaidi ya shs bn 320 na riba na tozo maumivu makali sana mshahara utaongezwa kweli??
Namna hii Tanzania ya viwanda tutaiona kweli?
 
Hili zigo tunalo tu, tutake tusitake, ongezeni bei ya umeme ili tulilipe tu, maana tukizidi kukata rufaa ndio deni linazidi kusonga. Walio saini kwa niaba ya Jamhuri wapo wametuliaaa wanacheki muvi linavyotupelekesha.
Tumeuzwa utumwani na machief Mangungo wa kileo.
 
Hili zigo tunalo tu, tutake tusitake, ongezeni bei ya umeme ili tulilipe tu, maana tukizidi kukata rufaa ndio deni linazidi kusonga. Walio saini kwa niaba ya Jamhuri wapo wametuliaaa wanacheki muvi linavyotupelekesha.
Tumeuzwa utumwani na machief Mangungo wa kileo.
 
Kwahiyo hapo sisi watumiaji ndo imekula kwetu nchi hii ina mambo ya kijinga sana na hili shirika sijui kwanini wanashindwa kulipa mshindani wake kama ilivyo mitandao ya simu mana lingeshajifia siku nyingi huduma mbovu ila maingizo yao makubwa

Tanesco ni mali ya serekali 100%, deal nyingi kubwa za wakubwa serekalini zimepitishwa huko, IPTL, Escrow n.k. Tukiwalaumu watendaji wa Tanesco ni kuwaonea tu
 
Back
Top Bottom