Tegeta Escrow: TANESCO yashindwa kesi dhidi ya IPTL. Yaamriwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 320!

Tegeta Escrow: TANESCO yashindwa kesi dhidi ya IPTL. Yaamriwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 320!

Hapa ndio tutajua uhalisia wa rais kupambana na wezi na wahujum uchumi.....Time will telll
 
Umeshasikia kitu kinaitwa Rais hewa Mkuu!?tafakari kwa kina Mkuu.

Hapa ndio tutajua uhalisia wa rais kupambana na wezi na wahujum uchumi.....Time will telll
 
Pesa hizo walipe ccm. Ndizo walizotumia kugharamia uchaguzi . Porojo za majipu Kwisha.
 
Kuna tetesi kuwa habinder sing ndo mfadhili mkuu wa chama wakati wa uchaguzi wa raisi na hata wakati wa uchaguzi wa mwenyekiti wetu pitia ukurasa wa zitto kabwe facebook kaandika hayo
Habinder Singh anatumiwa tu, wenye dili ni hawa Chama Cha Matapeli.
 
Asante kwa kusaidia kutoa ufafanuzi Watanzania wengi huwa tunadhani sisi ni kisiwa kwamba tunaweza kupuuza Hukumu za Kimataifa eti kwa kujiliwaza kuwa "hatulipiii , hatulipiiii" kwa ufahamu wangu mpaka dakika hii umeme ninao tumia kuandika bado TUNALIPA TUUUU
Acha kuzuga, hamna "Mahakama" yoyote ya kimataifa inayoruhusu wizi na utapeli.
 
Mods, tafadhali tuwekee hiyo hukumu ya ICSID hapa ili kila mtu ajisomee mwenyewe (badala ya kusoma second-hand sources na kudanganyana).

Waombe wanasheria wa TANESCO wakupatie file ya kesi hii itakusaidia kuwa na uelewa mpana kwa hoja na maamuzi ya kesi inayojadiliwa hapa.

Jina la faili hili hapa

Standard Chartered Bank Hong Kong v
Tanzania Electric Supply Company
Limited (TANESCO) - ICSID Case No.
ARB/10/20 - Decision on Jurisdiction
and Liability - 12 February 2014
 
Wakamatwe wale waliokuwa wakiimba kuwa fedha sio za umma sasa tanesco ni shirika la umma na ndio wanaopaswa kulipa fedha hizo ndio watwambie sasa na kalasinga seth akamatwe alipe hela
 
Jana umeme wamekata Dar nzima (labda Tz nzima ...sijui) nikasema eeehhh ndio Escrow nini????
Tz nchi yangu umemkosea nini Mungu...
 
Viwanda vinahitaji umeme, wakati huo huo asilimia ya watanzania wanaopata access ya umeme ni ndogo,, Huku shirika kuu madeni kibao, project kibao zinaweza kusimama kwa ajili ya hilo deni,, duuuuuh serikari ya viwanda
 
Nakumbuka maneno yake machache kuwa 'IKIWEKWA WAZI KUWA PESA WALIZO PEWA KAMA MCHANGO WA SHULE NA NDUGU RUGEMALILA KUWA NI ZA WIZI AMA UDANGANYIFU WA AINA YOYOTE BASI WAO KAMA TAASISI WAKO TAYARI KURUDISHA FEDHA HIZO'

Mkuu, acha kumtetea huyu mama. Aliyekamatwa na ngozi ni mwizi pia.

Wote hawa PAP, Ruge, Tiba, Stanbic, Chenge, nk nk, wametakatisha fedha. Hivyo:
  1. Ni kuwadaka leo leo na kuwasweka ndani bila dhamana
  2. Kamata mali zao na za ndugu na za marafiki zao haraka
  3. Walipe deni la watu, kwa uwazi kabisa.
  4. Wasiruhusiwe kutisha mzigo watoto na vijukuu zetu, huku wao wana tamba na ma-Vogue ya wizi mitaani.
 
Na malipo ya escrow yametolewa baada ya mahakama kuamua mmiliki ni PAP kwa hivyo TANESCO wala mwanasheria mkuu aliye hukumiwa awakuwa na jinsi maana sheria ishasema. Walichotaka TANESCO mahakama itambue kama ulinzi wao akija mwingine kudai na yeye ndiye mmiliki wa IPTL waende kudaiana mahakamani ndio ilikuwa kigezo chao cha kutolewa hiyo hela na mahakama ikaridhia hivyo.

Ambacho hujakizungumzia ni jurisdiction. Je hiyo mahakamani iliyoamua mmiliki ni PAP ilikuwa ina uwezo huo, na sheria iliyotumika ni sahihi? Kama Tanesco walingia mikataba kutumia English law, huwezi tu kujiamulia kutumia sheria na mahakama za Tanzania. Soma kwanza hukumu nzima.
 
Ambacho hujakizungumzia ni jurisdiction. Je hiyo mahakamani iliyoamua mmiliki ni PAP ilikuwa ina uwezo huo, na sheria iliyotumika ni sahihi? Kama Tanesco walingia mikataba kutumia English law, huwezi tu kujiamulia kutumia sheria na mahakama za Tanzania. Soma kwanza hukumu nzima.
Hiyo mahakama inatambulika as long as nchi ni mwanachama wa WTO...
Ili kulinda biashara za kimataifa, ndio hizi mahakama zimeundwa...
Otherwise hakuna ambaye angekubali kuwekeza nchi ambazo kuna figisu figisu...lakini kwa sasa wanajua ukizingua wapi pa kukupeleka...
Ukibisha unapigwa ban ...hakuna kuuza wala kununua nje ya nchi yako...utasalimika (e.g. Zimbabwe)????
 
Naona Makosa makubwa ya TANESCO ni mawili. i kuwahi kulipipa PAP kabla hata ya kusubiri hukumu juu ya capacity charge na la pili ii. Kutosubiria mgogoro wa umiliki wa IPTL iliijue exactly inamlipa mmiliki halali
Haya mambo mengine ni siasa tu! JK angekuwa ana interest humo kwanini amtake gavana kuhakikisha TANESCO hailipi mara mbili?

Wewe unafikiri ni kwanini hayo makosa yalifanyika. Kuwahi na Kutosubiri. Si ni makusudi ili watu wapige hela hapo. Wewe unacheza na Sirikali ya CCM nini.
 
TANESCO ijitangaze bankruptcy protection ili isilipe! Halafu baadaye serikali ivunje shirika hilo na kuunda jingine tofauti kabisa katika msingi ambao halitarithi madeni ya TANESCO ila litanunua mali zote za TANESCO kwa bei ya karibu na bure. Kuna njia nyingi sana za kiufundi za kutumia ili kuepuka adha hiyo ya kulipa hela nyingi bila faida yoyote. Kwa mfano iwapo Shirika jipya litanunua mali zote za TANESCO kwa bilioni kumi na tano tu, basi Wadai wote wa TANESCO watagawana hizo bilioni kumi na tano tu. na hivyo ITPL inaweza kuambulia Bilini mbili tu!
 
Mawakili wa Shirika la Umeme (Tanesco) wanaona shirika hilo la nishati kimsingi limeokoa takribani dola za Marekani 248.3 (zaidi ya Sh. bilioni 540) katika hukumu hiyo, Nipashe imefahamu.

Tanesco imeamriwa kulipa kiasi hicho wiki iliyopita katika hukumu ya mgogoro wake wa muda mrefu wa kisheria juu ya kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).

Fedha zilizookolewa na Tanesco zinatokana na ukweli kuwa mwaka 2010 SCB-HK ilidai katika Baraza la Kimataifa la Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) jumla ya dola milioni 396.7 (zaidi ya Sh. bilioni 860) kutoka kwa shirika hilo la nishati.

Baraza la ICSID lenye makao yake jijini Washington DC, Marekani ni sehemu ya Benki ya Dunia na linagharimiwa na taasisi hiyo ya kimataifa ya fedha.

Kiasi cha fedha kilichookolewa kinaweza kuwa hata kikubwa zaidi kama Tanesco itadai kurejeshewa fedha kutoka kwa wamiliki wapya wa IPTL, kampuni ya Pan Africa Power Solutions (PAP), kwa sababu kwa kulipwa fedha zote za akaunti ya escrow, shirika la nishati la taifa lilipiga mahesabu yake katika viwango vya awali, ambavyo ilishavipinga katika baraza hilo la kimataifa kwa miaka kadhaa.

“Kwa hukumu ya hivi karibuni, hata PAP italazimika kurudisha kwa Tanesco kiasi kikubwa cha fedha ilicholipwa, kwa sababu fedha za escrow zililipwa kwa kutumia bei ya umeme ya zamani… Ndiyo sababu kwa kutazama (jambo hili) kisheria, Tanesco pia imepata ushindi mkubwa,” Richard Rweyongeza, wakili aliyeiwakilisha shirika hilo la umeme kwenye baraza hilo la kimataifa aliiambia Nipashe.

TANESCO IMESHINDA
Rweyongeza alikuwa akitoa tafsiri yake ya kisheria juu ya mgogoro huo uliofikia tamati Septemba 12.

“Kama utasoma hukumu kama inavyoonekana, inaweza kuonekana kuwa (shirika) limepoteza kila kitu, lakini nakuhakikishia, pande zote mbili zimeshinda na Tanesco imeshinda zaidi."

Kwa mujibu wa Rweyongeza, kama mahesabu ya ICSID yakifuatwa kikamilifu, hata kima cha tozo ya uwekezaji kinacholipwa kwa PAP kinaweza kupungua kwa karibu asilimia 50 mpaka kuwa Sh. bilioni 2.5 kwa mwezi.

Kwa sasa, shirika hilo limekuwa likilipa tozo ya uwekezaji kwa PAP inayofikia Sh. bilioni tano tangu Januari 2014.

“Ieleweke kuwa Tanesco ilikuwa ikipinga kiwango cha bei ya umeme kinachotozwa na IPTL, si kiasi cha mkopo kilichotolewa na benki za kigeni wakati wa ujenzi wa kituo cha kufua umeme cha Tegeta," alisema zaidi Rweyongeza kuiambia Nipashe.

"Sasa ukweli kuwa kiwango cha bei kimepunguzwa una matokeo makubwa kifedha ambayo yanakwenda mbali zaidi ya hukumu ya kulipa zaidi ya Sh. bilioni 320.

“Kwa kufanikiwa kupunguza kiasi cha hukumu kutoka pale kilipokuwa, kwetu ni mafanikio makubwa."

Kwa mujibu wa Rweyongeza, kama sakata la escrow lisingetokea, Tanesco ingepata ushindi wa asilimia 100 kwenye kesi hiyo, kwa sababu lalamiko lake kuu kwamba bei ya umeme inayotozwa na IPTL ni kubwa lilikubaliwa na baraza hilo la usuluhishi la kimataifa.

Uamuzi huo wa ICSID umekuja miaka mitatu tangu serikali iruhusu kitatanishi kufanyika kwa malipo ya dola milioni 200 (sawa na Sh. bilioni 440) kutoka katika akaunti ya Tegeta escrow kwenda kwa kampuni ya Harbinder Singh Sethi ya Pan Africa Power Solutions Tanzania Limited(PAP).

Agosti 2005, SCB-HK ilinunua kwa bei ya punguzo ya dola za Marekani 76.1 kutoka benki ya Malaysia ya Danaharta, baada ya benki hiyo kushindwa kurejesha deni lake la muda mrefu kutoka IPTL.

Bei halisi ya deni hilo ilikuwa dola milioni 101.7, kwa mujibu wa ushahidi uliopo. IPTL ilikopa zaidi ya dola milioni 100 mwaka 1998 kutoka kwa ubia wa mabenki ya Malaysia ili kujenga mtambo wa kufua umeme wa megawati 100 wa Tegeta.


Chanzo: Nipashe
 
Siku hizi kazi yao wanaifanyia kwenye magazeti hao mawakili mpaka Tanesco wanapewa adhabu ya kulipa zaidi ya bilioni 300 walikuwa wapi..
 
Back
Top Bottom