Tegeta Escrow: TANESCO yashindwa kesi dhidi ya IPTL. Yaamriwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 320!

Tegeta Escrow: TANESCO yashindwa kesi dhidi ya IPTL. Yaamriwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 320!

Mkataba unakuwa na kitu kinaitwa offer, offeror and offeree; hakuna mahala TANESCO na HSC-Bank wanaizo connection directly. Hivyo ndio vigezo vinavyobainisha involved parties in any contract dispute.

Mikataba halali iliyopo ni TANESCO na IPTL

Mkuu, kwani mtu akinunua deni la kampuni nyingine, maana yake yeye si ndio mdai mpya, au unataka kusemaje?
 
True lakini anamdai aliekopa kwake kwanza in this instance IPTL.
mkopo sio kwamba alipewa mechmar?.
Maanake IPTL ni kampuni iliyoundwa na VIP ya ruge na mechmar ya malaysia.
Waliokopa ni mechmar,ndoo maana inaonekana kama ruge hahusika na huo mkopo,ingekuwa imekopa IPTL ,basi Rugemalila nae angekuwa ni mdaiwa wa hilo deni kama sikosei
 
mkopo sio kwamba alipewa mechmar?.
Maanake IPTL ni kampuni iliyoundwa na VIP ya ruge na mechmar ya malaysia.
Waliokopa ni mechmar,ndoo maana inaonekana kama ruge hahusika na huo mkopo,ingekuwa imekopa IPTL ,basi Rugemalila nae angekuwa ni mdaiwa wa hilo deni kama sikosei
Inategemea biashara yako imesajiliwa vipi lakini a Private Limited Company (Ltd) kama IPTL or a Public Limited Company (PLC) wana different legal status; kampuni ya aina hizo ni separate entities from its owners. In other words unapokopa kwa jina la kampuni aijalishi nani kakopa inayodaiwa ni kampuni sio mtu ikifilisika procedure ni kuitiana administrator aje kufanya asset stripping za kampuni kulipa madeni yenu.

Ndio maana unaona ma CEO wa makampuni awashitakiwi na wadeni ata kama kuna ushahidi wa embezzlement bali na serikari kwa makosa ya embezzlement or any other fraudulent acts.
 
Hiyo mahakama inatambulika as long as nchi ni mwanachama wa WTO...
Ili kulinda biashara za kimataifa, ndio hizi mahakama zimeundwa...
Otherwise hakuna ambaye angekubali kuwekeza nchi ambazo kuna figisu figisu...lakini kwa sasa wanajua ukizingua wapi pa kukupeleka...
Ukibisha unapigwa ban ...hakuna kuuza wala kununua nje ya nchi yako...utasalimika (e.g. Zimbabwe)????
Acheni uongo nyie matapeli, hamna mahakama yoyote ya "kulinda biashara ya mataifa". Makampuni yote yanafuata sheria za nchi husika; hamna mahakama ya "kimataifa" inayoweza kuiamuru, kwa mfano Coca Cola company kuilipa TANESCO. Kama TANESCO ina bifu na Coca-Cola, inafungua madai mahakama za Marekani, siyo mahakama zenu hewa.

Ukibisha unapigwa ban ...hakuna kuuza wala kununua nje ya nchi yako...utasalimika (e.g. Zimbabwe)????
Zimbabwe hawajapigwa ban na mtu. Wamewekewa vizuizi vya uchumi kwa sababu Mugabe aliwanyang'nya mashamba Wazungu halafu hela za fidia alizopewa na Waingereza akazi-escrow(kuweka mfukoni). Haikuwa mahakama yoyote isipokuwa serikali zao ziliamua.
 
Premise ya uzi huu ina mushkeli. Watu mnatoka povu na wengine wanachochea hoja za kipuuzi ku-deflect from real issue. Kila mtu anajua hizi "hukumu" ni za kutengenezwa.

Sidhani kama kuna suluhu kwa hili tatizo. Long as Chama Cha Matapeli kiko madarakani, kila mwaka "Mahakama za Kimataifa" zitakuwa zinaamuru TANESCO ilipe mamilioni ya pesa kwa sababu moja au nyingine. Halafu sijui huo uchumi wa viwanda utadondoka kutoka mbinguni, kwa sababu najua Tanzania haina uwezo wa kuanzisha viwanda peke yake, na hakuna mwekezaji halali atakubali kulanguliwa kwa umeme eti kusudi CCM iongoze milele.

Kitu kibaya zaidi ni kwamba hata mkipigia kura upinzani, CCM haiwezi kuachia madaraka kwa hiari, kwa hiyo unless wakoloni wanawaonea huruma na kuja kuwatimua, mtazidi kulipia umeme wa ghali kanda hii ya Afrika na bado umeme wenyewe utakuwa wa mgao.
 
Ni shida tupu!!!
Mnatupaka matope mnaposema tuliwapa ridhaa ya kumiliki bunduki.
 
Je ESCROW ni pesa ya UMMA au ya Singasinga wa CCM?? Hilo ndo nataka kufahamu kwanza kabla ya kuhangaika na maneno meeeeengi ya mwanasheria wa upande mmoja.
 
Kama ESCROW mbona heading ni SECROW.kwani inamajina mangapi?
 
Escrow ni dubwana lenye mizizi mirefu na nguvu hasa. Haligusiki hata kwa mikasi [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Duuuh, ina mana ancle Ruge nae inabidi arudishe sehemu ya mpunga aliochukua wakati jamaa alishagawa kwa washkaji wake!
 
Swali la msingi kabisa ni kuhusu muda wa mkataba kati ya TANESCO na IPTL;
Ulikuwa unaaza lini na kumalizika lini? Haya mengine ni mbwembwe tu. Ni lazima tuwe na mitazamo mipana kabla hata ya kutumia utaalam ubobezi katika maamuzi.
 
Back
Top Bottom