Wizara ya Madini
Govt Institution
- Apr 12, 2025
- 50
- 20
Hayo, yameelezwa leo Juni 19, 2025 na Kaimu Meneja wa Kitengo cha Uwazi na Uwajibikaji kutoka Taasisi ya TEITI - Bw. Erick Ketagory alipo mwakilisha Katibu Mtendaji wa Taasisi ya TEITI katika Jukwaa la Uziduaji la mwaka 2025 linalofanyika Jijini Dodoma. Jukwaa hilo limeandaliwa na Asasi ya Kiraia ya Hakirasilimali.
Bw. Ketagory amesema kuwa, TEITI imeanza kutekeleza takwa la uwekaji wazi wa Mikataba ambayo Serikali imeingia na Kampuni za Madini, Mafuta na Gesi Asilia ambapo Mikataba hiyo inapatikana katika tovuti ya TEITI.
Akielezea kuhusu uwekaji wazi wa majina ya wamiliki wa makampuni katika Sekta ya Madini, Mafuta na Gesi Asilia, TEITI imekamilisha ujenzi wa Rejista husika(Beneficial Ownership Register) ambayo ipo wazi kwa matumizi ya umma ambayo inapatikana kupitia bo.teiti.go.tz.
Bw. Ketagory amesisitiza kuwa Milango wa TEITI ipo wazi kwa ajili ya kushirikiana na wadau mbalimbali ili kutekeleza kikamilifu matakwa ya Sheria inayosimamia TEITI na vigezo vya Kimataifa vya EITI.
Zifuatazo ni picha katika Matukio.