SoC02 Teknologia na Utamaduni Bora: Suluhu Bora ya Hitaji la Mabadiliko Yenye Tija Tanzania

SoC02 Teknologia na Utamaduni Bora: Suluhu Bora ya Hitaji la Mabadiliko Yenye Tija Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

kingqusa

New Member
Joined
Aug 17, 2022
Posts
3
Reaction score
2
GridArt_20220821_212323254.jpg

1. UTANGULIZI
Jamii ya Tanzania kama jamii nyingine za nchi za Afrika zenye historia ya kutawaliwa, inakumbwa na changamoto ya kustahimili maendeleo endelevu katika kila secta, iwe Elimu, Afya, Uchumi, Uwekezaji, Kilimo, Viwanda na hata Utalii. Licha ya uwepo wa mifumo bora ya kiuongozi na serikali, ujuzi na uwezo mkubwa wa wananchi, maendeleo katika sayansi na teknolojia pia utajiri mkubwa wa rasilimali kama vile ardhi, madini, maji, na malighafi nyingine ambazo ni muhimu katika dhana ya maendeleo ya taifa, bado taifa linakumbwa na ukinzani mkubwa katika jitihada za kushawishi na kuchochea Mabadiliko na maendeleo endelevu yenye kuinufaisha jamii nzima.

2. Sasa tunakosea wapi kama taifa?
Ikiwa nchi ni tajiri wa mali na amani, wakazi wana ujuzi na uwezo pia tuna mfumo bora wa siasa na uongozi inakuwaje tujiulize swali hili? Kwanini bado tunahitaji mabadiliko licha ya juhudi kubwa ya wanajamii, serikali na secta binafsi kuleta maendeleo?

Kama mnadharia, mchunguzi na mbunifu nina amini kuwa maswali haya ni matokeo ya changamoto zinazozalishwa na Utamaduni wa kizazi pamoja na mifumo ya kijamii isiyo rafiki. Ambavyo kwa pamoja vinakwamisha na kupunguza ufanisi wa jitihada za kuleta maendeleo ya kudumu na endelevu. Tukichimba undani wa chanzo cha Utamaduni na mifumo hii, itagundulika kuna mahusiano ya moja kwa moja na historia pana ya ukoloni, ukoloni maomboleo, utandawazi na athari zao katika mfumo wa tabia za watawaliwa na Utamaduni wao mama.

Hivyo basi, kutoka na upana wa tafakuri ya ni wapi tunakosea kama taifa kupelekea jamii kushindwa kupokea na kusababisha Mabadiliko na maendeleo ya pamoja, ni vigumu kupata jibu la moja kwa moja lenye kubeba msingi wa Mabadiliko yenye tija.

3. Je, tufanye nini ili kuleta Mabadiliko yenye tija?
Hakika hili ndilo swali lenye kubeba msingi wa suluhu halisi la hitaji la Mabadiliko katika jamii yetu. Ili jamii iweze kupokea vyema maendeleo endelevu na tuweze kujitegemea tunahitaji mchakato wa hiyari wa mageuzi ya kiutamaduni.

3.1 Ndoto ya kijana mbunifu na hitaji la mageuzi ya kiutamaduni.
Baada ya kupata uhuru wa nchi, sera ya Ujamaa na Kujitegemea iliyo asisiwa na baba wa taifa, Mwl. Julius Kambalage Nyerere, ilifanikiwa kutengeneza dira njema ya Utamaduni wa Ujamaa na undugu, lakini hatukufanikiwa kutimiza dira ya Kujitegemea na uwajibikaji. Baada ya sera hii, hapajakuwapo na mpango mwingine shirikishi wa kitaifa wenye dhima ya kufanya mageuzi ya kiutamaduni. Hivyo kupelekea ongezeko la ukinzani kati ya jamii na maendeleo ya taifa.

Ikiwa jamii inahitaji Utamaduni Bora, limekua jukumu la kijana mbunifu kubuni mpango wa kimageuzi ALTER "Associative Long Term Evolution Reach". Ambao ni MPANGO SHIRIKISHI WA KUFIKIA MAGEUZI YA KUDUMU kwa kutumia bunifu rafiki za kiteknolojia, biashara na Uwekezaji, vyenye uwezo wa kuathiri mfumo wa akili na tabia za wanajamii.

ALTER project.png

3.2 Mahusiano kati ya teknolojia na Utamaduni
Utamadani na Teknolojia vinauhusiano wa karibu. Utamadani unaunda mifumo ya jamii ambayo inahitaji ubunifu wa Teknolojia, pia ubunifu wa kiteknolojia na elimu ya sayansi vinapoingia katika jamii, huathiri mifumo, uhitaji na tabia za wanajamii hivyo Utamaduni wao. Kwa kanuni ya kinyume, ubunifu ukitumika kuunda mifumo yenye ideolojia sahihi, tunaweza kuleta athari sahihi katika Utamaduni kama vile Uwazi, Uwajibikaji, Usawa, Udhubutu, Ufumbuzi, Ubunifu zaidi, Uwekezaji na hata mashirikiano yenye tija katika kutimiza Ndoto ya pamoja ya Taifa letu.

3.3 Mchakato wa Mageuzi ya Kiutamaduni kwa kutumia mpango wa ALTER
Kwa kutumia mduara wa mahusiano kati ya Utamaduni na Teknolojia, Mpango wa ALTER utafanikiwa kuathiri mduara wa maisha ya mwanajamii kwa kugusa Akili, Kazi, Utajiri, Mapumziko, Roho, Afya, Mahusiano na Familia. Ili kufanikisha dhima hii, mpango wa ALTER unalenga kuunganisha nguzo kuu sita, ambazo ni Data, Systems, Frameworks, Business Units, na Jamii yenyewe.

ALTER central Unit [Connect]2.jpg


3.3.1 Hatua
Wazo lolote jipya hupitia changamoto kadhaa katika utekelezaji, licha ya changamoto hizi Mpango wa ALTER umefanikiwa kupiga hatua. Mpango wa ALTER una muundo Bora, juu ya UNITI mama ya kibiashara BROS "Bold & Royal Oath Society" ambayo ndiyo itakayobeba jukumu la utekelezaji wa mradi na wazo zina la mageuzi haya.

ALTER Project Formation.jpg


3.3.2 Mafanikio
Mpango wa ALTER umefanikiwa kufikia mafanikio yafuatayo,
  • Kutengeneza, kuonesha na kuthibitisha fursa za ajira za moja kwa moja kwa vijana zaidi ya 400 ndani ya miaka mitano ijayo.
  • Utengenezaji wa mfumo na bidhaa ya mfano ya DATA za pamoja "Global Data Framework", profiling system na kuandaa bunifu za kialgorithim zaidi ya 40 chini ya UNITI ya kibiashara ALTECH.
  • Uandaaji wa mpango wa awali wa E6-Hub "Educe, Equip, Expose, Explore, Experience and Express Hub"
Business Units Model.jpg

  • Kushawishi vijana zaidi ya 60 watakao shiriki na kujitolea nguvu kazi.
  • Kupata eneo la kutosha pamoja na jengo la maradhi, ofisi na Uwekezaji.
  • Kukusanya Ahadi za michango kutoka kwa jamii na watu wa karibu zenye thamani ya karibu Tsh 400,000/= ndani ya miezi miwili, kwa sharti la kukusanya endapo tutafikisha walau Tsh. 10,000,000/=
3.3.4 Hitaji la Mpango wa ALTER ilikukidhi lengo la Mageuzi kwa Ufanisi
Licha ya hatua na mafanikio haya bado mpango wa ALTER unakabiliwa na hitaji kubwa la kukusanya kiwango kikubwa cha pesa cha walau Tsh. 30,000,000/= kwa ajiri ya kumudu gharama za uanzilishi na uendeleshaji ndani ya miaka miwili.

4. Hitimisho
Maendeleo yenye tija katika jamii yanategemea sana Utamaduni sahihi katika jamii husika. Ilipatokee Mabadiliko yenye kuweka msingi wa utatuzi wa changamoto za jamii yetu ya Tanzania, tunahitaji kufanya na kupokea Mageuzi ya Kiutamaduni kwa kutumia mifumo rafiki na shirikishi haswa kwa jamii yenyewe. Mageuzi ya Kiutamaduni ni jambo linalowezekana. Kwa muundo na hitaji la jamii ya Tanzania, Teknolojia, Biashara na Uwekezaji ndizo njia Bora zaidi kufanikisha Mageuzi haya.

Mpango wa ALTER chini ya BROS, ni ndoto ya kijana wa kitanzania mwenye kubeba maono ya Biashara ya Mabadiliko kwa kulenga Mageuzi ya Utamaduni, haswa kwa kutumia msingi wa ubunifu na Uwekezaji. Naamini Jukwaa la Jamii, Stories of Change, Wadau na Wanajamii kwa ujumla, mtakua sehemu ya kuchangia rasilimali hitajika, haswa rasilimali pesa, ili kulipa nafasi wazo hili. Kwani ni kwa ajiri ya maslahi mapana ya jamii na nchi yetu pendwa ya Tanzania.

SAM_0084~2.jpg


Deogratious G. Mwakyusa
Mbeya Urban, MangaVeta
0656 844980.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom