Teknolojia: Waumini Kanisani watoa Sadaka kwa Lipa Namba na kuchanja kadi za benki (Credit Card Payment)

Teknolojia: Waumini Kanisani watoa Sadaka kwa Lipa Namba na kuchanja kadi za benki (Credit Card Payment)

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Katika hatua dunia ipofikia sasa, Teknolojia inazidi kukimbiza kila sekta ya Dunia... mababu waliofakiriki kipindi cha utumwa wakifufuka Leo wanaweza kupigwa na butwaaa na kuacha vinywa wazi kama sisi tutakapo pigwa butwaa endapo tukifufuka mwaka 3025, yani miaka elfu 1000 toka sasa kwa jinsi Teknolojia itakavyokuwa imepamba moto.

Moja ya tukio lililoshangaza watu wengi hivi karibuni ni namna Teknolojia ilivyoshika kasi mpaka katika mahali pa Kuabudu. Moja ya video imeonekana ikisambaa ikionesha waumini wa kanisa moja huko ughaibuni wakitoa Sadaka kwa kutumia kadi za benki (Credit Card Payments). Kifaa kimeonekana kupita kwa waumini wenye kutoa sadaka na kisha wao kugusisha kadi zao za Benki


View: https://youtu.be/AmpxP2Z5R_0?si=fQlLdyrhe9hNPn2M
 
Safi sana, ni maendeleo mazuri mno katika kanisa 😂 waumini walambwe kwa kila style 🔥
 
Ila wawe waangalifu na mitego ya shetani wasije wakanasa
 
Back
Top Bottom