Wakati nchi yetu, hususani Jiji letu la Dar-es-salaam lilipoondoka kwenye mfumo wa Analogia na kuingia mfumo wa dijitali, Tume ya mawasiliano nchini TCRA, ilituhakikishia wote tulio na TV kuwa ingawa nchi yetu inalazimika kuingia kwenye mfumo wa dijitali, ambapo kila mwenye TV atalazimika kuwa na king'amuzi, tukahakikishiwa kuwa zipo channel za hapa kwetu nchini, zipatazo 5 hivi zitakuwa zinaonekana bure, miongoni mwa channel hizo ni TBC1, StarTV, ITV na Channel ten, zitakuwa zinaonekana bure kabisa, hata kama hujalipia ada ya kila mwezi kwenye king'amuzi chako. Cha ajabu kabisa leo asubuhi wakati nawasha TV yangu, nilipatwa na mshangao mkubwa baada ya kuona hata zile channel ambazo nilikuwa naziona bure, zikawa zinasoma kwenye screen yangu NO ACCESS, NOT SUBSCRIBED!! Kwa maana hiyo hizo channel zote hazionekani tena!! Badala yake kuna channel moja tu ya kampuni ya Startimes, ambayo ndiyo inayoenekana bure, ambayo inaitwa STV Guide, ambayo ni channel maalum kwa ajili ya matangazo yao kampuni ya Startimes! Sijui wadau wenzangu mmeligundua hilo? Sasa ninalowauliza hawa jamaa wa Startimes pamoja na TCRA kwa nini wametufanyia utapeli wa kutuingiza kwenye mfumo wa dijitali na kutuhakikishia kuwa hata sisi walala hoi tusio na pesa za kuweza kulipia channel za pesa, tutaendelea kuziona channel za bure, mbona sasa wamekiuka ahadi yao na kututaka tulipie hata zile channel za bure??!! Au hao Startimes na TCRA wanafuata nyayo za mabosi wao CCM, kwa kupenda tu kudanganya na kutoa ahadi hewa kibao, kwa lengo tu la kuwarubuni wapiga kura wao??!! Sisi wateja tunayo haki ya kuwalazimisha hao Startimes watuonyeshe zile channel za bure kama yalivyo makubaliano yetu, kinyume cha hapo sisi wateja wa ving'amuzi vya Startimes, tutawaburuza mahakamani hao matapeli makubwa wa Startimes!!!