MTZ 255Dar
JF-Expert Member
- Sep 25, 2018
- 1,149
- 3,963
Jeshi la Anga la Israel, Israel Air Force(IAF) linafanya mashambulizi ya anga mbalimbali nchini Syria,hii ni baada ya Serikali ya rais Bashar Al Assad wa Syria kuangushwa na Waasi wa Hayat Tahirir Al-Sham(HTS) ambao wanaungwa mkono na nchi ya Uturuki.
Israel inasema kwamba,mashambulizi hayo yanalenga kuharibu silaha za hali ya juu,Maghala ya Makombora ya masafa marefu,mifumo ya ulinzi wa Anga na Viwanda vya Serikali vya kutengeneza Silaha vilivyokuwa vinaendeshwa na Iran. Israel inadai kwamba,haitaki Silaha hizo ziangukie mikononi mwa Waasi hao.
Israel siku ambayo waasi waliudhibiti mji mkuu wa Damascus, ilifanya mashambulizi Damascus yakilenga kituo cha utafiti cha MAZZERL kilichojihusisha na utengenezaji wa Makombora ya Mafasa ya Kati kilichokuwa chini ya Wakufunzi wa kijeshi kutoka Tehran. Pia, Israel imeshambulia kiwanda cha kutengeneza Silaha za Sumu kilichokuwa chini ya udhibiti wa Tehran.
Katika hatua isiyo ya kawaida,Jeshi la ardhini la Israel lililokuwa katika milima ya Golan,limeamliwa kuingia ndani ya Syria umbali wa Kilometa 14 kutoka Milima ya Golan na kuuteka MLIMA HERMON uliokuwa chini ya udhibiti wa jeshi la Syria.
Mlima huo uliopo kwenye Mpaka wa Lebanon na Syria ulikuwa unalindwa na wanajeshi wa Syria ambao Walikimbia wapigano ya waasi waliokuwa wanataka kuuteka pale Assad alipopinduliwa,jeshi la Israel liliingilia kati ya kuchukua udhibiti wa eneo hilo muhimu.