Tembo Warriors, Timu yetu ya Taifa ya Walemavu

Tembo Warriors, Timu yetu ya Taifa ya Walemavu

Greatthinker47

Senior Member
Joined
Sep 24, 2021
Posts
145
Reaction score
260
Jamani hii team yetu ya taifa ya Mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu inafanya vizuri sana huko kombe la dunia nchini Uturuki.

Wadau tusiwachukulie poa hawa vijana waliojitoa pamoja na ulemavu wao kulipapambania taifa letu vema huko Ughaibuni. Kama tujuavyo walipokutana na Mama Samia Suluhu alipendezwa na morali yao, wakapata fursa ya kwenda kujifua kwajili ya michuano ya kombe la dunia kwa watu wenye ulemavu wa mguu mmoja nchini Poland.

Ambapo katika mechi ya kujipima nguvu na team ya taifa ya nchi hiyo Poland vijana wetu waliibuka na ushindi wa goli 7 kwa sifuri. Pia katika draw tukajikuta tupo group moja na nchi hiyo ya Poland, Kazakhstan, na Spain kwa mujibu wa ulive leo jioni.

Inasemekana katika group hilo sisi ndiyo underdog kulingana na record walizonazo wenzetu, ila mechi yetu ya kwanza dhidi ya Spain tumeweza kutoka nao sare ya bila kufungana.

Kiukweli nafurahishwa na juhudi na mwenendo mzima wa tembo warriors, nadhani ni muda wetu sasa sisi Watanzania kuwafuatilia ndugu zetu na kuwatia moyo hata wakiwa katika majukumu yao wajue kuwa watanzania wenzao tupo nyuma yao.

Tumewatenga mno, ni nadra sana kuona wakizungumzwa pamoja na juhudi kubwa wanayoifanya huko uyghaibuni.

Ahsante, naomba kuwasilisha mada mezani, karibuni.
 
Tuombe tu siasa isije kuingia hapo...

Mungu awqfanyie wepesi wabebe kombe hilo
 
Team za wanawake na team za vijana pamoja na team za walemavu na beach soccer zinafanya vizuri kwasababu huko hakuna interest za mapapaa wakubwa wenye manufaa napo kama kwenye football za wakubwa.
 
Mi nasema hivi;hii nchi kama kweli tuna akili kuna maeneo ya kimichezo ya kuwekeza kuliko mingine. Mfano-sisi ni wazuri sana kwenye boxing kuliko michezo yote enzi na enzi,yet tumeudharau sana mchezo huu hadi pale Azam (na sasa Mo Dewji) walipoamua kututoa usingizini. Boxing ndo utambulisho wa taifa letu kama ilivyo riadha kwa Kenya na Ethiopia, golf kwa South Africa, soccer kwa nchi za Afrika Magharibi,n.k

Turudi kwenye mada

Kwa kuwa soka bado unabaki kuwa mchezo pendwa,basi Timu ya Soka ya Taifa ya Walemavu halisi ipewe uungwaji mkono mkubwa kuliko Timu ya Soka ya Taifa ya Walemavu wa bandia (akina Bocco). Kule Simba nako waitazame vizuri Simba Queens kuliko wale wapuuzi akina Kanoute.
 
Hahahaha duuh mkuu Kwa bocco apo umetisha Sana upo sahihi pale point yako inapolenga kwamba tuwekeze nguvu kubwa kwenye michezo ile inayotupeleka mbali katika macho ya dunia Kwanza, ni sahihi kabisa boxing na mpira huu wa walemavu tupo vizuri hata marathon uko kidogo tunajitahidi kuliko kandanda la kina majogoro
 
Back
Top Bottom