Greatthinker47
Senior Member
- Sep 24, 2021
- 145
- 260
Jamani hii team yetu ya taifa ya Mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu inafanya vizuri sana huko kombe la dunia nchini Uturuki.
Wadau tusiwachukulie poa hawa vijana waliojitoa pamoja na ulemavu wao kulipapambania taifa letu vema huko Ughaibuni. Kama tujuavyo walipokutana na Mama Samia Suluhu alipendezwa na morali yao, wakapata fursa ya kwenda kujifua kwajili ya michuano ya kombe la dunia kwa watu wenye ulemavu wa mguu mmoja nchini Poland.
Ambapo katika mechi ya kujipima nguvu na team ya taifa ya nchi hiyo Poland vijana wetu waliibuka na ushindi wa goli 7 kwa sifuri. Pia katika draw tukajikuta tupo group moja na nchi hiyo ya Poland, Kazakhstan, na Spain kwa mujibu wa ulive leo jioni.
Inasemekana katika group hilo sisi ndiyo underdog kulingana na record walizonazo wenzetu, ila mechi yetu ya kwanza dhidi ya Spain tumeweza kutoka nao sare ya bila kufungana.
Kiukweli nafurahishwa na juhudi na mwenendo mzima wa tembo warriors, nadhani ni muda wetu sasa sisi Watanzania kuwafuatilia ndugu zetu na kuwatia moyo hata wakiwa katika majukumu yao wajue kuwa watanzania wenzao tupo nyuma yao.
Tumewatenga mno, ni nadra sana kuona wakizungumzwa pamoja na juhudi kubwa wanayoifanya huko uyghaibuni.
Ahsante, naomba kuwasilisha mada mezani, karibuni.