Temeke, Dar: Ahukumiwa kifungo cha maisha kwa kumlawiti mtoto wa kiume mwenye miaka tisa

Temeke, Dar: Ahukumiwa kifungo cha maisha kwa kumlawiti mtoto wa kiume mwenye miaka tisa

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Dar es Salaam.

Mahakama ya Wilaya ya Temeke imemuhukumu Mkazi wa Chamanzi, Said Wanie (35) kifungo cha maisha kwa kosa la kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka tisa.

Pia mahakama hiyo imemuagiza mshtakiwa huyo kumlipa mtoto huyo fidia ya kiasi cha Sh500,000.

Kati ya Mei 3, 2020 maeneo ya Chamanzi Wilaya ya Temeke mshtakiwa huyo alimlawiti mtoto huyo huku akijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria.

Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mkazi, Anna Mpessa alisema mahakama hiyo imejiridhisha na ushahidi uliotolewa na mtoto mwenyewe pamoja na vielelezo vilivyotolewa na daktari vikionyesha kuwa mtoto huyo amelawitiwa.

Mpessa alisema katika ushahidi uliotolewa na mtoto mwenyewe ulidai kuwa akiwa maeneo ya nyumbani kwao anacheza mshtakiwa huyo alifika na kumwambia alikuwa anaitwa na mtu aliyetambulika kwa jina moja la Musa ambaye ni mlinzi wa Shule ya Sekondari ya Chamanzi.

Alisema mtoto huyo aliieleza mahakama hiyo kuwa aliongozana mshtakiwa huyo mpaka kwenye choo cha shule hiyo na alipoingia ndani alifunga mlango kisha akamvua nguo na kummwagia maji mwili mzima baadaye alianza kumlawiti.

Chanzo: Mwananchi
 
Hivi watu hawajifunzi kutoka kwa wengine hizo adhabu za mahakama? najiuliza alikuwa anatafuta nini kwa mtoto wa miaka 9? au ni kurukwa na kili uchizi, kujitoa ufahamu au masharti ya mganga? aaaah acha aoge hizo mvua zote
 
Daah! Kwa mwendo huu kongole kwa serikali kufunga sites chafu!
 
Nimefarijika anaenda kunyea ndoo maisha yake yote.
 
Jamaa nae anaenda kuolewa gerezani
Nyapara amfire sana uyo jamaa
 
... daah! Kwa mwendo huu kongole kwa serikali kufunga sites chafu!
Tena wamechelewa sana kuzifunga! Lakini pia watufungie na mtandao wa Telegram maana kwa sasa imekuwa ni gulio.
 
Hivi watu hawajifunzi kutoka kwa wengine hizo adhabu za mahakama? najiuliza alikuwa anatafuta nini kwa mtoto wa miaka 9? au ni kurukwa na kili uchizi, kujitoa ufahamu au masharti ya mganga? aaaah acha aoge hizo mvua zote
Daah ndo hapo Sasa an
 
Back
Top Bottom