Temeke: Mgawo mkali wa Umeme kuliko hata ule uliotangazwa, wanakata mchana na usiku hakuna ratiba

Temeke: Mgawo mkali wa Umeme kuliko hata ule uliotangazwa, wanakata mchana na usiku hakuna ratiba

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Haieleweki sababu yake hasa ni nini , ukiuliza Wafanyakazi wa Tanesco hawana majibu ? bali wanasema kwamba wao wameelekezwa kukata tu.

Tunafahamu kwamba Temeke mara zote inatajwa kuishi watu duni , lakini watu wake siyo duni kama Tanesco ilivyokaririshwa, wanazo akili na iko siku watalipa huu uchafu , yaani wao kwa wiki sasa wanakatiwa umeme mchana na usiku na wamenyamaza tu. sisi wenye viwanda tunatumia gharama kubwa mno kwenye uzalishaji na hakuna anayejali.

Lakini iko siku mtajua umuhimu wa Temeke , Endeleeni
 
Temeke ni kila siku. Siku moja nimepita kule Keko viwandani nikakuta mashine zimezima hakuna umeme, vibarua wameshika tama hawajui watakula nini.

Kumbuka hao watu huenda kazini na nauli tu. Ama kweli mafisadi hayana huruma kabisa.
Aibu kubwa sana kwa ccm
 
Halafu utakuta wapuuzi wanaleta mada mama anapendwa sana😏😏,wenye fresh food shops watakua wamefirisika mpaka sasa.
 
Ulitaka wakate masaki hebu vumilieni nani aliwambia mkaishi temeke .kwanza furahini mnapata time nzuri kukabana vichochoron
 
Back
Top Bottom