Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Akizungumza jijini Dar es Salaam, jana Januari 12, 2026, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), Mosses Mabamba amesema ukarabati wa kivuko hicho umekamilika kwa mafanikio.
Amesema kazi zilizofanyika ni pamoja na kubadilisha injini na mifumo ya umeme, ukarabati uliodumu kwa siku nne na kugharimu shilingi milioni 30.
Mabamba ameeleza kuwa majaribio ya mwisho yatafanyika asubuhi ya leo na endapo yatakamilika bila changamoto, kivuko hicho kitaanza kutoa huduma kuanzia saa nane mchana.
Wananchi wanaotegemea kivuko hicho wameeleza kufurahishwa na kurejea kwa huduma hiyo, wakisema itarahisisha shughuli zao za kila siku ikiwemo kwenda kazini, shuleni na kufanya biashara.
Hata hivyo, wananchi hao wameiomba Serikali kuendelea kuboresha na kuimarisha huduma za vivuko ili kuepuka adha zinazojirudia mara kwa mara.
Wakati huo huo, Serikali imesema inaendelea kutekeleza mpango wa muda mrefu wa kuboresha usafiri wa majini, ikiwemo ukarabati wa kivuko cha MV Magogoni.
Kivuko hicho kinatarajiwa kuanza kutoa huduma mwezi Aprili na kitakuwa na uwezo wa kubeba abiria 2,000 na magari 60 kwa safari moja.