Gordian Anduru
JF-Expert Member
- Apr 16, 2021
- 369
- 747
Wafanyakazi wa posta walishangazwa kuona barua yenye anwani inayosomeka “Kwenda kwa Mungu, Baba SLP, Mbinguni”.
Baada ya kujiuliza pa kuipeleka wakaamua kuifungua na kuisoma, ilikuwa imeandikwa “ Kwako Mungu Baba Mimi ni mjane kikongwe kuna vibaka wameniibia shilingi laki moja, mwezi huu sina kabisa hela ya matumizi naomba unisaidie Shilingi Laki moja Mungu wangu nimekwama”.
Wafanyakazi wa posta wakahisi kuwa bibi kachanganyikiwa labda uzee maana huwezi kuandika barua kwenda mbinguni, kwa kumhurumia wakaamua kujichangisha wenyewe ikapatikana shilingi elfu sabini.
Wakaiweka kwenye bahasha na kutuma kwenye anwani yule bibi.
Siku kadhaa baadae wakakuta barua nyingine toka kwa bibi Yule Yule walipoifungua wakakuta imeandikwa. “Kwako Mungu Baba nakushukuru sana kwa kujibu ombi langu, Mwezi umeenda vizuri,
Najua uliniwekea Laki Moja ile wale wafanyakazi wa posta wezi sana wamenichomolea elfu thelathini zangu”