Tenda ya Bandari Bagamoyo itangazwe upya kwa uwazi

Tenda ya Bandari Bagamoyo itangazwe upya kwa uwazi

Hatutaweza kupata mkataba mzuri kama mwekezaji anajua yuko peke yake! Tunachotaka tunajua na mradi utangazwe kama tenda ili wadau wengine na mashirika mengine nayo yaweze kuleta tenda zao. Kuna watu serikalini na wanasiasa wameshawekwa mfukoni na China kwa kupewa visafari na visemina vya kijinga bila kujua hiyo ni mipango ya kutufanya tukubali mkataba mbaya.

Hivyo mimi nashauri tutangaze upya tenda badala ya kuongea na wawekezaji kama vile tunabembeleza. Muda ushapita sana na kuna wawekezaji wengine wengi sana na nchi yetu imeingia uchumi wa kati hivyo ni wakati tofauti na ule wa kikwete.

Lakini kitu kingine kimoja mkataba na pesa ya ujenzi isiendane na uendeshaji wa bandari. Tukisema uendeshaji sijui awe mchina kwasababu ametupa pesa hatutaweza kumtoa hata kama uendeshaji sio mzuri. Hivyo uendeshaji wa bandari usiwe wa wawekezaji! Yaani mkataba ulivyo kwa sasa hatuwapi sababu ya kuongea na sisi kama wanajua hatuna sehemu ya kwenda

Mfano nchi za G7 zinaanzisha hii


Zitto , Pascal Mayalla
yaani katika jambo tunatakiwa kuwa serious kama taifa basi ni huu mkataba.
 
Tenda ya nini tena? Serikari yetu haitoi hata mia kwenye hizo US $ Billion 10 gharama za mradi mzima.
Tukopeshwe hiyo pesa ili tuwe na access ya kukusanya kodi na kuitengenezea business plan bandari yenyewe!

Yaani waje wafanye kazi watumie reli yetu kusafirisha mizigo yao sisi TRA yetu izuiwe kuingia hapa kukusanya kodi?

Halafu tukusanye pesa nyingine kutoka vyanzo vingine tulipie mkopo wa SGR?

Tutakuwa taifa la kipumbavu sana!!
 
Watanzania wengi hawajui wanachooongea! Hii bandari ni mkopo na ndiyo maana tuliambiwa nchi nyingine Wachina wamechukuwa bandari kwasababu nchi imeshidwa kulipa madeni sasa kama lilikuwa sio deni hili tishio linatoka wapi? Hata Kenya bandari ni ya Wakenya sema mkopo na wajenzi ni wa China. Nchi nyingi zikitoa mkopo zinataka mjenzi wao kama ilivyo kwenye kipande cha reli ya kisasa ambacho China wanatoa mikopo watajenga wenyewe na sio Uturuki kama Morogoro mpaka Dodoma.
Kwenye huu mradi kuna sehemu ya viwanda hivi vingeweza vikawa binafsi lakini bandari yenyewe itakuwa maajabu kama haitakuwa ya Watanzania na ndiyo maana gharama ni muhimu sana kuhakiki kwasababu ni mkopo. Kama ni mkopo na design ya bandari wamiliki ni Tanzania kuna ugumu gani kutafuta pesa kwa njia tofauti badala ya kuongea na kampuni moja kwa miaka 20! Uwezo wa kulipa $10B Tanzania tunao kama bandari itatumika vizuri hatuna haja wala haraka ya kuingia mikataba mibaya. Pamoja na riba haitazidi $500 kwa mwaka kwa miaka 25
Mkuu kwa kukusahihisha tu, huu siyo mkopo. Ni kwamba hawa watu wana invest. Ni sawa sawa na Dangote. Tofauti ni kwamba the type of the project is different na yule anayewekeza kwenye kiwanda ndiyo maana kuna a lot of issues around. Kwa maana hiyo watu kulinganisha huu mradi na ule wa Sri Lanka ni kosa kubwa. Haifanani hata kidogo.

Anachosema mleta mada ni sawa na kusema tenda ya kujenga Dangote itangazwe na serikali ya Tanzania, which is totally wrong.
 
Mkuu kwa kukusahihisha tu, huu siyo mkopo. Ni kwamba hawa watu wana invest. Ni sawa sawa na Dangote. Tofauti ni kwamba the type of the project is different na yule anayewekeza kwenye kiwanda ndiyo maana kuna a lot of issues around. Kwa maana hiyo watu kulinganisha huu mradi na ule wa Sri Lanka ni kosa kubwa. Haifanani hata kidogo.

Anachosema mleta mada ni sawa na kusema tenda ya kujenga Dangote itangazwe na serikali ya Tanzania, which is totally wrong.


Mradi huu una tofauti gani na Kenya?. Kiwanda cha Dangote ni chake kisheria kesho anaweza kuamua kukivunja au kuondoka! Bandari sio hivyo hili ni deni la serikali !. Na kama sio hivi basi Mradi ni mbaya sana na hautakiwi kuendelea maana kuna sababu gani ya msingi ya kuwapa wawekezaji mizigo yetu yote ya bandari zetu za Dar na Tanga na kupoteza mapato kama mapato yanaenda kwa China? hii ni biashara gani?.

Kwa mawazo yangu huu mradi unakuzwa kwa munufaa binafsi ya wanasiasa mfano sababu ya kwamba meli kubwa haziwezi kufika pale kwanini kusifunguliwe kampuni moja kama ilivyo Twiga na kuwa na bandari zote mbili ili waweze kugawa mizogo ambayo haiwezi kwenda Dar kwasababu ya ukubwa wa meli ndiyo zije bagamoyo. Hii itapunguza gharama za ujenzi wa bandari kwasababu wanajenga kama vile hakuna bandari hapo Dar na ni kubwa tu inampaka reli na mpaka sasa wanapanua bandari ya Dar. Cost itapungua na zile industrial park watakazo jenga zitajilipa zenyewe maana watakuwa wanakodisha kwa kampuni binafsi magodauni na sehemu za magari. Hii project ingeweza kuwa ya $5B tu na sio $10B ukizingatia kuna bandari ya Dar lakini kuna watu wengi wanapenda pesa iwe nyingi kama vile ni ya bure! mnafikiri Magu angeacha pesa ya bure!

Halafu Watanzania wengine hawafuatilii hata sera za China wameshasema wanategemea kufanya bandari iwe kama base yao ya kijeshi pamoja na ya msumbiji na hii imetolewa na chama chao cha kijamaa! na ndiyo maana wanataka pawe kama balozini ili kisheria tusiweze kuwazuia wanajua sisi tunaongeka hivyo miaka 30 ijayo watakuwa wameshabadilisha mikataba na kuongeza muda kuwa miaka 99 na ndiyo maana walikuwa wameshaweka bunge letu mfukoni!. Hizi tunajifunza nini kwenye bunge la kikomunisti wakati ni chama kimoja cha kidikteta! Jamani tuweni wepesi tuacheni ushabiki kama ule ulio wauwa wapendwa wetu kwa ushabiki wa kitoto wa Corona

Lakini kibaya wana mtindo wa kuongeza gharama za ujenzi ili uwe tegemezi milele


When we look at Africa, we see many countries chasing dreams of a better economic future while burying themselves in massive amounts of infrastructure-induced debt that they may not be able to actually afford. There have already been warning signs: the $4 Addis Ababa-Djibouti Railway ended up costing Ethiopia nearly a quarter of it’s total 2016 budget, Nigeria had to renegotiate a deal with their Chinese contractor due to their failure to pay, and Kenya’s 80% Chinese-financed railway from Mombasa to Nairobi has already gone four times over budget, costing the country upwards of 6% of it’s GDP. In 2012, the IMF found that China owned 15% of Africa’s external debt, and hardly three years later roughly two-thirds of all new loans were coming from China. This has some analysts issuing warnings about debt traps – with some even going as far as calling what China is doing a new form colonialism.

What does China get out of this?​

ICOAST-CHINA-ECONOMY-TRANSPORT

Chinese and Ivorians technicians work on the construction site of a new container terminal at the ... [+]
AFP/GETTY IMAGES
China needs what Africa has for long-term economic and political stability. Over a third of China's oil comes from Africa, as does 20% of the country’s cotton. Africa has roughly half of the world’s stock of manganese, an essential ingredient for steel production, and the Democratic Republic of the Congo on its own possesses half of the planet’s cobalt. Africa also has significant amounts of coltan, which is needed for electronics, as well as half of the world’s known supply of carbonatites, a rock formation that’s the primary source of rare earths.
However, there is a common misconception that all Chinese projects in Africa have the backing of Beijing. More often than not, Chinese SOEs are operating in Africa on purely for-profit ventures that don’t have the ambitions of their government in mind. However, it can be difficult to separate China’s commercial intentions in Africa from the strategic, as, in many cases, the two inevitably overlap. The internationalization of Chinese construction firms and IT companies as well as the building of infrastructure to better extract and export African resources, are key concerns for Beijing. So while the infrastructure being built on the ground may not necessarily be orchestrated by Beijing it does ultimately play into China’s broader geo-economic interests.

Follow me on Twitter or LinkedIn. Check out my website or some of my other work here.
Wade Shepard
 
Wewe ndiyo hujui ni ujinga kubinafsisha bandari ya nchi!! Bandari sio kiwanda cha cement. Vile viwanda walivyopanga kujenga unaweza kujenga kama mwekezaji lakini Bandari yenyewe ni mkopo sio uwekezaji. Tulifanya kama uwekezaji bandari yenyewe na kujitoa kama nchi hapo tutakuwa tumekwisha tujiulize mapato ya bandari ya Dar kwa sasa tutawapa China?

Bandari itakuwa ya Nani? Tanzania au China na Oman? Yaani tuligenga bomba la gas kwa mkopo halafu tuwape taifa jingine bandari!? huu ni ujinga wa hali ya juu sana
Nenda kasome wewe acha kukariri maisha kama mkopo unaenda kukopa pesa kwenye ma bank au taasisi za kifedha duniani au unaenda kukopa nchi yoyote sasa tuseme unayosema ni sawa matusi ya nini kwa mchina umeenda kukopa kakataa nenda kakope sehemu nyingine jenga mbona SGR umekopa issue iko wapi. Unataka kuniambia mradi wa SGR na wa umeme ni kama Bandari ya bagamoyo? SGR na Umeme umekopa umepata pesa umetoa tender umewapa walioshinda wanajenga sasa haya ya Bagamoyo imekuwaje tena? kama pesa unazo unatoa tender unajengewa tena unaringa wewe mwenye kutoa pesa. Bagamoyo ni uwekezaji sio tender ya ujenzi.
 
Mkuu kwa kukusahihisha tu, huu siyo mkopo. Ni kwamba hawa watu wana invest. Ni sawa sawa na Dangote. Tofauti ni kwamba the type of the project is different na yule anayewekeza kwenye kiwanda ndiyo maana kuna a lot of issues around. Kwa maana hiyo watu kulinganisha huu mradi na ule wa Sri Lanka ni kosa kubwa. Haifanani hata kidogo.

Anachosema mleta mada ni sawa na kusema tenda ya kujenga Dangote itangazwe na serikali ya Tanzania, which is totally wrong.
Huyu mtu haelewi wala hataki kuelewa ulichoandika kama hajaelewa tena wala usimjibu maana ulichoandika ni 100% facts. Kufananisha na Srilanka sijui ni upotoshaji wa hali ya juu huu sio mkopo turudie tena huu sio mkopo. Bravo kwa maelezo yaliyojitosheleza anayetaka kujifunza asome kimya.
 
Kutafuta mwekezaji sio kitu rahisi kama watu wengi wanavyofikiri sio kitu cha kutangaza na watu wakatender kama kazi za barabara ni tofauti kabisa. Tuiachie Serikali wafanyekazi zake na sisi wananchi tusubiri matokeo kweni ni serikali yetu itahojiwa na Bunge letu tukufu.
Mkuu kwani Tanzania tuna mabunge mawili? Mimi najua la Ndugai hilo tukufu ni lipi na linaongozwa na Nani?
 
Mimi nashauri badala ya kutangaza tenda ya bandari ya Bagamoyo,

Itangazwe tenda ya kuboresha bandari ya Tanga kwani tunategemea hivi karibuni kupata mradi wa kusafirisha mafuta toka Uganda.
 
Hiyo ya bagamoyo is already some people's curse .wanajijua .zitangazwe shares ,mashirika na wananchi tuweke historia. Manchi makubwa yako busy kuwamegea watu wao chanjo Kwanza na kutafuta njia ya kutupiga ie EU inazuia tusiingie kwao kama hujachanjwa chanjo Yao. Sisi viongozi wetu wanapigana vikumbo kutupiga ili majamaa yafurahi na kuwapa sofa ati ninwanademokrasia na Wana utawala wa Sheria
 
Mwambieni waachane na kutangaza habari zasimba kama ilivo kwa diamond
 
Nenda kasome wewe acha kukariri maisha kama mkopo unaenda kukopa pesa kwenye ma bank au taasisi za kifedha duniani au unaenda kukopa nchi yoyote sasa tuseme unayosema ni sawa matusi ya nini kwa mchina umeenda kukopa kakataa nenda kakope sehemu nyingine jenga mbona SGR umekopa issue iko wapi. Unataka kuniambia mradi wa SGR na wa umeme ni kama Bandari ya bagamoyo? SGR na Umeme umekopa umepata pesa umetoa tender umewapa walioshinda wanajenga sasa haya ya Bagamoyo imekuwaje tena? kama pesa unazo unatoa tender unajengewa tena unaringa wewe mwenye kutoa pesa. Bagamoyo ni uwekezaji sio tender ya ujenzi.

Naona unakubaliana na mimi sijui beef iko wapi?
 
Back
Top Bottom