Tetesi: Tenda zote za Serikali na makampuni binafsi kuwa monitored na serikali, mawakala binafsi hawana nafasi tena

[emoji23] [emoji23] [emoji23]
ndio maana yule Jamaa amejikaza akashindwa ameona aje akutishe tu!
 
Atashindwa,
Awape tenda wasukuma kama anavyojifaragua kwamba na yeye ni msukuma kumbe ni mkimbizi tu ila hayo mambo atashindwa na alishashindwa kitambo sana

Kuna vitu msd hawana wala hawawezi to supply Kwa wakati,

Vifaa vya shule, maabara they know nothing kuhusu hiyo business

Jiwe awe wazi tu, nchi imemshinda akae pembeni
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa hasemi tu lakini anaipiga vita sana sekta binafsi.
Halafu utashangaa huenda kashauriwa na Kabudi na Bashite!
Yaani Kabudi = Bashite?. Aman kweli siasa inapunguza hadhi ya watu!
 
 
Walipewa nafasi za juu katika biashara hii wakaleta kuua viwanda vyote, wakasambaza vitu hewa acha wanywe jeuri yao.
 
yameanza kutimia, soon tuturudi kwenye maduka ya ushirika.
 
Na bado zimezingua upigaji upo sana,,sijui anapodanganya inamsaidia nn
 
Hili ni tatizo linguine. Kwanza walianza na MSD kuifanya ndo muingizaji na msambazaji pekee wa vifaa tiba, vitendanishi na dawa kwa hospitali za serikali. Kwa uamuzi huu serikali ililenga kukwepa ongezeko la bei za bidhaa na huduma kutoka makampuni ya watu binafsi ambao ni mawakala (representatives) wa makampuni ya uzalishaji (manufacturers). Kwahiyo MSD inaagiza moja kwa moja kutoka kwa manufacturers na kusambaza mahospitalini.

Utaratibu huu wa kuwakwepa wasambazaji kutoka sekta binafsi una changamoto nyingi na kwahiyo bado haujawa na ufanisi. Kwanza, tofauti na makampuni binafsi, MSD hawatembei kwa wateja (hospitali) na kujua mahitaji yao (yaani hawafanyi sales and marketing). Wanachofanya ni kuwauzia wateja bidhaa walizonazo. Ubaya wake ni kwamba wateja wanakosa bidhaa wanazozihitaji na wanazozipata zinakuwa hazina ubora unaotakiwa.

Biashara hasa ya bidhaa za kisayansi ni very dynamic na inahitaji intelijensia ya hali ya juu kujua nini kinahitajika sokoni. MSD hawana intelijensia ya kibiashara kitu ambacho kinawafanya wasijue waingize bidhaa gani na kwa wakati gani. Mathalani, msimu huu wa masika wasambazaji wa kampuni binafsi tayari walishatambua kulikuwa na mahitaji ya kaseti za kupima homa ya dengue na sio malaria wakati MSD hawakuja hilo na kwa hiyo hawakuwa na kaseti za homa hiyo kwenye bohari lao bali za malaria. Matokeo yake kaseti hizo zikawa hadimu na bei yake ikawa juu Zaidi kuliko kawaida na zilipatikana kwa makampuni ya watu binafsi tu kwa bei ya sh. 300,000 hadi 350,000 na bei ya kipimo chenyewe huko mahospitalini ikawa hatari tupu (elfu 40-70).

Ukweli ni kwamba bei ya kaseti na huduma ya kipimo cha homa ya dengue haina tofauti na homa ya malaria ambayo kwa kawaida hugharimu sh. 3000-5000. Lakini bila kuzingatia kuwa dengue ni homa ya mpito, MSD nao baadae kabisa wakaanza kuingiza kontena za kaseti za dengue ambazo bila shaka zitaishia ku-expire. Cha ajabu ni kwamba ingawa bei ya kipimo hicho toka MSD ilipungua ukilinganisha na ile kutoka kwa wasambazaji binafsi, bado haikuweza kupungua kufikia bei ya kawaida ya sh. 3000-5000 wakati MSD kama wa serikali huingiza bidhaa kwa njia za mkato.

Changamoto nyingine ni kwamba baadhi ya vifaa tiba havihitaji kusambazwa tu kwa wateja, bali kuna huduma (after sale services) zinatakiwa ziendelee kutolewa na manufacturers. Kawaida ni kwamba, manufacturers hutoa huduma hii kupitia mawakala wao waliopo katika nchi husika ambao huwapa mafunzo maalumu ya kuweza kutoa huduma hiyo. Ukweli ni kwamba after sale-services ni “closed system” kwa maana si kila wakala anaweza kutoa huduma hiyo kwa vifaa tiba kutoka manufacturer mungine. Bali manufacturers wengi hawako tayari kufungamana na wakala mwenye mafungamano na washindani wao.

Kwahiyo MSD kama wakala hawataweza kufungamana na competing manufacturers kwa wakati mmoja kama vile BD, Thermo Scientific, Carestream, Philips, SonoScape, Fazzini, Uzumcu, Roche Diagnostics, Sysmex,Abbott, Human Diagnostics, FujiFilm, Liofilchem, Oxoid, Fiochett, Snibe, Eppendorf, Cephaid, Mindrey, Erba, Stago, Applied Biosystems, Himedia, Instrumentation Laboratory, Sharlau, Merk Millipore, Sigma Aldrich, Life Technologies, Omega, Qiagen, Promega, Bio-Rad, Tekkim Kimya, Zeiss, Optika, Olympus n.k. Kiufupi ni kwamba utaratibu wa biashara unaopendekezwa na serikali hautokuwa na tija bali ni kuharibu soko huria na utasababisha kuadimika kwa bidhaa shindani.
 
Inasiktisha sana...

Hapo kutakua na msongamono mkubwa sana wa ununuzi vifaa...

Unatoa order leo, unaipta baada ya miaka2 na pesa ishaliwa...

Mifumo ya serikali ipo slow sana...


Cc: mahondaw
 
Hap Sijaelewa ,ko inamaana kutakuwa hakuna manunuzi kupitia suppliers wa Gpsa?suppliers Msd?
 
Hapo kwenye mishahara athubutu, ndio atajua hata kunguru huwa anauma akizidiwa.
 
Kwa hii jiwe ataangukia pua tu,
Kwenye kupima ardhi tu wanachemsha, wanaweka kampuni binafsi, huyu jamaa ni kama mchawi/mwanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…