Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 59,045
- 94,974
Niliamua kufa ili niishi!
Nimekutana na vijana wengi na kugundua kuwa wengi hawajamaanisha. Umewahi kudhamiria kitu kwa kumaanisha na kujitoa bila kuogopa chochote wala yeyote?
Watu tuliokulia familia masikini huwezi kuondokana katika umasikini kama haupo tayari kujikataa na kujitoa kafara.
Nilipoamua kuingia kwenye ujasiriamali nilimwambia Mungu kuwa either nife au nipate ninachokitaka, sintakubali kuishi maisha ya kujipa matumaini na kusogeza siku mbele.
Najua unajiuliza "how". Ujasiriamali siyo lele mama. Ujasiriamali siyo bibi yako wa kumletea masihara. Lazima uwe na roho ngumu unless kama wazazi wako wamekurithisha mali. Wapo watu ambao walikuta vitu ni ready made na kuviendeleza na wapo wale ambao lazima ujitengenezee mwenyewe.
Ukianza kulia na kulalamika kwanini wazazi wako hawakukuachia chochote, utakufa masikini na kuishia kubangaiza and nobody cares.
Dunia ya biashara yataka uvumilivu uvumilivu uliopitiliza. Na utayari wa kukutana na kila aina ya mawaa. By the way dunia yenyewe ni ya muda tu hakuna atakayetoka salama nini cha kuogopa sasa? Aibu? Kufeli? Kuanguka? Kuachwa?Kukamatwa? Kuteseka? Nini cha kuogopa zaidi ya kifo na kifo chenyewe kipo hata ukikiogopa utakutana nacho tu?
Bora nife nikiwa na miaka michache yenye matokeo kuliko kuishi miaka 100 ya aibu, njaa, dharau, umasikini, ubangaizaji na uchuro.
Ngoja nirudi kwenye pointi hapa. Yeyote anayetaka kukuaminisha kuwa maisha ya ujasiriamali ni kitu simple na utapata hela ndani ya dakika ni mwizi. .
Ngoja nikupe full story, sijawahi sema mahali popote. Baada ya kuendesha kampuni yangu ya PPI kimafanikio nikajiona sasa ngoja nianze rasmi ndoto yangu ya kuanzisha chuo kikuu. Hizi akili siwezi kuzisahau kabisa.
Nikauza assets zote za kampuni iliyokuwa green acres Victoria na kuanza safari ya kuanzisha chuo Morogoro, nikanunua kompyuta za kutosha. Kwasababu nimewahi kuwa TCU nilikuwa na mahusiano mazuri na viongozi wa NACTE nikakamilisha vibali vyote yaani.
Nikaandaa vitabu vya curriculum vingine nikanunua VETA. Ee bwana chuo kikaanza hatimaye Geophrey Tenganamba ameanzisha chuo lakini ndani yangu nilikuwa na ndoto ya kumiliki Chuo kikuu. Yaani nikajipigia hesabu zangu ndani ya miaka 5 lazima nitakuwa na kibali cha kuwa chuo kikuu. Nikachora ramani kabisa ya chuo kikuu. Nikaanza kuuliza viwanja kilombero. Nikabuni na jina la chuo kikuu kabisa "UCOKI" UNIVERSITY COLLEGE OF KILOMBERO. Enzi hizo sijui chochote kuhusu venture capitalists yaani investors, wawekezaji nilikuwa najiendea mwenyewe kama lone wolf.
Akiba yangu yote nikapeleka kwenye media nikitegemea kuwa nikipata Ada nitalipa gharama zote na wafanyakazi wangu. Haya sasa wanafunzi mwanzoni walikuwa 15. Nikaongeza matangazo zaidi badala ya wanafunzi kuongezeka wakapungua watano. Kufanya tafiti nikagundua wote wanaenda chuo cha Saint. Joseph . Why?
Wao walikuwa wanafanya Matangazo sana na mashindano ya mamiss, disco kibao yaani full Fujo.... , wanafunzi warembo wanajaa huko. Mimi chuo changu hardcore. Wanafunzi waliobaki chuo changu walikuwa wagumu wagumu wote. Ilikuwa ni chuo cha watu wagumu, wenye hasira na maisha, wanaosoma kama vichaa. Masomo yalikuwa mengi mpaka ujasiriamali.
Kitabu kwenda mbele tena nawaaambia wanafunzi wangu mkimaliza hapa mtakuwa na uwezo wa kujiajiri kabisa.
Nilikuwa na nia ya dhati ya kubadili mfumo wa elimu but sikusoma soko langu vizuri. Nilidhani nawajua wateja wangu.Hawa vijana wa form four na six aisee wakiona wadada warembo wanakimbilia huko sijui ndiyo ujana. Hawa Vijana waliniangusha sana.
Biashara si lelemama.
Miezi mitatu natakiwa kulipa mishahara ya waalimu. Gharama nyingine nyingi za uendeshaji. Wakabaki wanafunzi watatu. Hapo walimu wameshtaki polisi kulipwa mishahara yao. Gharama nyingine nyingi ikiwa na mafundi wa ujenzi walikuwa wote wananisumbua. Kichwa kinawaka moto. Kila nilichogusa kilikuwa cha moto. Nikienda kwenye chuo changu mwenyewe nahisi kufa kufa. Nikajua kabisa hii battle nimeshapigwa chakali.Nisingepitia haya labda nisingekuwa hapa nilipo leo.
Mambo yalizidi kuwa magumu kuzidi. Nilikimbia Chuo changu mwenyewe na kwenda kujificha kibaigwa kwa mwezi mmoja, nilitafutwa na polisi kama fugitive na watu waliokuwa na uchungu na mimi nikatupa simu na namba yangu inayoishia 99.
Baada ya mwezi nikafanya maamuzi ninarudi kupambana na chochote nitakachokutana nacho njiani. Liwalo na liwe. Dada yangu anapiga simu "tafuta kazi mdogo wangu" ilikuwa ni ngumu kwa mtu aliyewahi kushika mamilioni ya pesa kwa wiki akasubiri mshahara wa laki tano kwa mwezi. Sikuwa tayari kurudi Misri. Safari ya Kaanani lazima iendelee.
Haya sasa nikarudi Morogoro na kushangaa kuwa kompyuta 25 zote zimeuzwa ikiwa ni pamoja na fenicha zote. Kila mtu ameuza kujilipa deni. Nikawaambia chukueni kila kitu niachieni uzima. Nikabaki ZERO yaani zero.
Nilichekwa "haha tulikuambia ukajiona mjanja" "eti chuo kikuu my foot" "nenda katafute ajira acha ukichaa wewe" "ukikua utaacha" "wewe unaota ukiamka utaacha". Wengine marafiki, ndugu yaani dah haya maisha .
Nikarudi Dsm kwa muda nikiwa kwishne kabisa hata marafiki zangu nawakimbia. Nikamtafuta Paul Mashauri "bro nimepigwa huku". Haya sasa nilipoenda kwa ofisi yake ya zamani ee bwana nikaambiwa Paul Mashauri alishafilisika "makubwa". Yaani tajiri niliyekuwa namuona kama mentor wangu na yeye karudi zero. Tukaonana. Aliponisimulia yaliyomkuta sikuamini. Yaani zero. Nikamsimulia yaliyonikuta alicheka sana. Akaniambia "Geophrey naanza upya" . Sikuamini akaanza kwa spidi Kusajili kampuni mpya nikiwa kama General Manager.
"Geophrey bado sina hela ya kukupa". Nikasema " bro nataka kujifunza ujuzi wa kuanza upya ".
Nilijifunza jambo kubwa kwa Paul, roho ya kuanza upya. Kama siyo Paul Mashauri sijui ningepata wapi hiyo roho na nilijifunza kwa vitendo kutoka kwa mtu aliyeanguka kama mimi. Tukatafuta ofisi kabisa.
Baada ya muda fulani nikamwambia Paul, nipo tayari kuondoka na kuanza safari yangu upya. Nikaondoka na kwenda Kenya.
Watu watauliza ulianzaje maisha Keny?
Nilikuwa mwandishi. Usisahau. Nilikuwa nimeandika vitabu na kuviweka amazon kindle ambavyo vilikuwa vinauzwa mpaka leo lakini sikuwa na uwezo wa kutoa hela kwa paypal hapa Tanzania. Nilipoenda Kenya nikafanikiwa kutoa na kuanza safari upya.
Nilikuwa na ndoto ya kuwa na Chuo kikuu lakini haikutokea vile nilivyotarajia. Haya yote ni maisha. Si kila kitu kitatokea vile unavyorajia mengine ni sehemu ya kukupika kuwa mtu sahihi kwaajili ya kile kilicho mbele yako usiache kuendelea.
Leo hii nikikumbuka nilikotoka namshukuru Mungu sana na zaidi siogopi chochote wala yeyote. Siogopi kufedheheshwa, siogopi kuachwa, siogopi kuanguka na siogopi kujaribu. Kama siyo mapito niliyopitia nisingekuwa na mwelekeo sahihi. Yapo mengi yaliyotokea niliyafurahia yote. Ninayapenda mapito yangu na nipo tayari kuguswa na mapito yangu ili niwe ninayetakiwa kuwa. Leo hii unasikia mtu anafundisha ujasiriamali au anaelezea ujasiriamali hajawahi hata kwenda BRELA hajui hata maumivu yake zaidi ya kusoma vitabu vya think and grow rich.
Mwingine anaongea mambo mepesi mepesi na kuwaaminisha watu ili achukue hela zao. Wengine wanataka makubwa lakini hawataki mapito. Huwezi kuwa bora bila mapito. Ninajivunia kwa niliyoyapitia may be leo nisingekuwa na ndoto ya fursa 101 wala sokoworld yaani alibaba of Africa wala mikakati ya wawekezaji.
Kila kitu unachokipitia unakipitia kwasababu unatakiwa kukipitia ili kuwa yule unayetakiwa kuwa.
Mimi ni Ndoto.
Mimi ni uwezekano.
Mimi ni Ushindi.
Source: Facebook page yake
Sent using Jamii Forums mobile app