Tengeneza dawa usiku za kuondosha sumu mwilini asubuhi uinywe sumu itaondoka

Mkuu hii Nanaa ndio nn sijakuelewa!! ama umemaanisha nanasi!!
asaubuhi umemaanisha asubuhi ama!!! nijuze tafadhali!!

Nanaa kwa Dar unaweza kuipata soko la Kariakoo, soko mjinga la Mkunguni na Bibi titi au soko la mabaniani, Zanaki Street opposite na Zanzibar Hotel. Ukiwaaambia nanaa tu wanakupatia.
 
Thread nzuri sana MziziMkavu, ila ninakuomba sana unifahamishe zaidi kuongeza awareness
yangu. Je, mtu ukiwa na sumu (toxins) mwilini mwako unajisikiaje? Au kwa maneno mengine ni dalili
zipi zinazoonesha una sumu mwilini? Ntajuaje nina toxins mwilini? etc. Asante.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu MziziMkavu,kwanza nakupongeza sana kwa utayari wako kila mara wa kushare mambo mengi sana mazuri na yenye manufaa kwa watu wote wanaopenda kujifunza.Big up brother.naomba nifafanulie, baada ya kuwa nimekwisha loweka usiku kucha hayo malimao,matango na nanaa kila moja kwenye glasi yake, asubuhi wakati wa kunywa, nitakunywa kila kimoja kama kilivyo kwenye glasi yake au nachanganya maji ya vyote vitatu kwenye chombo kimoja? Na kamani kila moja kama ilivo kwenye glasi yake, kwa interval gani?
Utakunywa kila glasi moja kama ilivyo hapo kwenye picha Kuna chungwa,Tango,Nanaa na limau zote zipo glasi 4 utakunywa hiyo dawa kwa muda wa siku 3 utafanya hivyo hivyo kila siku dawa mpya.
 
1472965_553948204690486_472456741_n.jpg

Pata Malimao 2 weka ndani ya glasi ya maji baada ya kuyakata, Tango nusu kata weka ndani ya glasi ya maji, na majani ya Nanaa 10 au 10 weka katika glasi maji acha usiku kucha asaubuhi kabla ya kula kitu kunywa hayo maji utaondosha sumu iliyo mwilini mwako. Tumia kisha uje unipe feedback.

Mh dr MziziMkavu,hayo malimao nayakamua na maji au kama yalivyo?
 
Asante sana mzizi mkavu, nataka kujaribu hii kitu. Ila nahisi sijaelewa vizuri hizo picha na maelezo. Ifuatavyo ndivyo nilivyo elewa, kama sivyo please nisaidie kwa lugha nyepesi

Siku ya kwanza: Limao vipande viwili
Siku ya pili: nusu ndimu, nusu tango na nanaa (mint)
Siku ya tatu: Mint na limau nusu
Siku ya nne: Nusu tango na limau nusu

NB/ Hivyo vyote vinatakiwa vilale kwenye maji na ninywe asubuhi kabla sijala chochote

Nipo sawa mkuu, Picha zimenichanganya sana,
 
Mkuu ili zoezi linafanyika kwa muda wa siku ngapi???? Au nikinywa mara moja tu inatosha???
 
Mh dr MziziMkavu,hayo malimao nayakamua na maji au kama yalivyo?
Angalia picha jinsi yalivyo n andio hivyo hivyo ufanye .

Asante sana mzizi mkavu, nataka kujaribu hii kitu. Ila nahisi sijaelewa vizuri hizo picha na maelezo. Ifuatavyo ndivyo nilivyo elewa, kama sivyo please nisaidie kwa lugha nyepesi

Siku ya kwanza: Limao vipande viwili
Siku ya pili: nusu ndimu, nusu tango na nanaa (mint)
Siku ya tatu: Mint na limau nusu
Siku ya nne: Nusu tango na limau nusu

NB/ Hivyo vyote vinatakiwa vilale kwenye maji na ninywe asubuhi kabla sijala chochote

Nipo sawa mkuu, Picha zimenichanganya sana,
Angalia jinsi picha ilivyo na ndio hivyo hivyo utakavyo fanya

Mkuu ili zoezi linafanyika kwa muda wa siku ngapi???? Au nikinywa mara moja tu
inatosha???
Kama utaweza kila mwezi
fanya japo mara 1 kwa siku moja au mara 3 kwa mwezi pia sio mbaya zaidi. Dawa ingine unafanya hivi:

KUTOA SUMU MWILINI
Dawa za kemikali husababisha sumo mwilini na husababisha kupata baadhi ya maradhi. Unashauriwa kutumia maji ya ndimu glasi moja kunywa kwa kila mwezi ili kuondoa sumu mwilini
 
1472965_553948204690486_472456741_n.jpg

Pata Malimao 2 weka ndani ya glasi ya maji baada ya kuyakata, Tango nusu kata weka ndani ya glasi ya maji, na majani ya Nanaa 10 au 10 weka katika glasi maji acha usiku kucha asaubuhi kabla ya kula kitu kunywa hayo maji utaondosha sumu iliyo mwilini mwako. Tumia kisha uje unipe feedback.

kitambi lazima kiishe
 
nashukuru kwa somo mkuu lakini tuweke wazi kuna litakalo tokea baada ya hapo maana kuna siku nilikunnywa dawa ya aina hii ilinibidi nisiende ofisini maana tumbo lilifungua kwa hii vipi?na hasa maji ya tango
 
Utakunywa kila glasi moja kama ilivyo hapo kwenye picha Kuna chungwa,Tango,Nanaa na limau zote zipo glasi 4 utakunywa hiyo dawa kwa muda wa siku 3 utafanya hivyo hivyo kila siku dawa mpya.

Asante sana kwa ufafanuzi mzuri.
 
Baada ya kunywa huo mchanganyiko asubuhi,natakiwa kukaa muda gani ili kuanza kula? Au nikimaliza tu naweza piga chai vitumbua hapohapo?
 
baada ya kunywa hiyo dawa unatakiwa ukae japo saa 1 ipite ndipo waweza kula hivyo vitumbuwa vyako na machopo chopo yako ya asubuhi.
 
Back
Top Bottom