Tengeneza dawa usiku za kuondosha sumu mwilini asubuhi uinywe sumu itaondoka

Mkuu hii Nanaa ndio nn sijakuelewa!! ama umemaanisha nanasi!!
asaubuhi umemaanisha asubuhi ama!!! nijuze tafadhali!!

Nanaa kwa Dar unaweza kuipata soko la Kariakoo, soko mjinga la Mkunguni na Bibi titi au soko la mabaniani, Zanaki Street opposite na Zanzibar Hotel. Ukiwaaambia nanaa tu wanakupatia.
 
Thread nzuri sana MziziMkavu, ila ninakuomba sana unifahamishe zaidi kuongeza awareness
yangu. Je, mtu ukiwa na sumu (toxins) mwilini mwako unajisikiaje? Au kwa maneno mengine ni dalili
zipi zinazoonesha una sumu mwilini? Ntajuaje nina toxins mwilini? etc. Asante.
 
Last edited by a moderator:
Utakunywa kila glasi moja kama ilivyo hapo kwenye picha Kuna chungwa,Tango,Nanaa na limau zote zipo glasi 4 utakunywa hiyo dawa kwa muda wa siku 3 utafanya hivyo hivyo kila siku dawa mpya.
 

Mh dr MziziMkavu,hayo malimao nayakamua na maji au kama yalivyo?
 

Asante sana mzizi mkavu, nataka kujaribu hii kitu. Ila nahisi sijaelewa vizuri hizo picha na maelezo. Ifuatavyo ndivyo nilivyo elewa, kama sivyo please nisaidie kwa lugha nyepesi

Siku ya kwanza: Limao vipande viwili
Siku ya pili: nusu ndimu, nusu tango na nanaa (mint)
Siku ya tatu: Mint na limau nusu
Siku ya nne: Nusu tango na limau nusu

NB/ Hivyo vyote vinatakiwa vilale kwenye maji na ninywe asubuhi kabla sijala chochote

Nipo sawa mkuu, Picha zimenichanganya sana,
 
Mkuu ili zoezi linafanyika kwa muda wa siku ngapi???? Au nikinywa mara moja tu inatosha???
 
Mh dr MziziMkavu,hayo malimao nayakamua na maji au kama yalivyo?
Angalia picha jinsi yalivyo n andio hivyo hivyo ufanye .

Angalia jinsi picha ilivyo na ndio hivyo hivyo utakavyo fanya

Mkuu ili zoezi linafanyika kwa muda wa siku ngapi???? Au nikinywa mara moja tu
inatosha???
Kama utaweza kila mwezi
fanya japo mara 1 kwa siku moja au mara 3 kwa mwezi pia sio mbaya zaidi. Dawa ingine unafanya hivi:

KUTOA SUMU MWILINI
Dawa za kemikali husababisha sumo mwilini na husababisha kupata baadhi ya maradhi. Unashauriwa kutumia maji ya ndimu glasi moja kunywa kwa kila mwezi ili kuondoa sumu mwilini
 

kitambi lazima kiishe
 
Mi huwa nasikia mtu akila sumu anywe maziwa kumbe huwa haisaidii.
 
nashukuru kwa somo mkuu lakini tuweke wazi kuna litakalo tokea baada ya hapo maana kuna siku nilikunnywa dawa ya aina hii ilinibidi nisiende ofisini maana tumbo lilifungua kwa hii vipi?na hasa maji ya tango
 
Utakunywa kila glasi moja kama ilivyo hapo kwenye picha Kuna chungwa,Tango,Nanaa na limau zote zipo glasi 4 utakunywa hiyo dawa kwa muda wa siku 3 utafanya hivyo hivyo kila siku dawa mpya.

Asante sana kwa ufafanuzi mzuri.
 
Baada ya kunywa huo mchanganyiko asubuhi,natakiwa kukaa muda gani ili kuanza kula? Au nikimaliza tu naweza piga chai vitumbua hapohapo?
 
Baada ya kunywa huo mchanganyiko asubuhi,natakiwa kukaa muda gani ili kuanza kula? Au nikimaliza tu naweza piga chai vitumbua hapohapo?
baada ya kunywa hiyo dawa unatakiwa ukae japo saa 1 ipite ndipo waweza kula hivyo vitumbuwa vyako na machopo chopo yako ya asubuhi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…