Tengeneza Mkono wa Mbele na Nyuma Gym Kwa Kufanya Hivi....

mkuu me nasema pushup fulani hivi ukipiga mikono unakuwa unafanya kama unapiga skullcrushers hutengenezi alama ya kopa kwenye vidole unaiweka mikono kawaida tu ila ukitoka juu lazima vipepsi viguse chini je nzuri kwa triceps vp nikichanganya na diamond push up
 
Mkuu ninazozijua mimi ni kama hizi.

Kama una picha ya hizi unazozisema naomba ushee nasi ili tujifunze kitu kipya.

Ila hata hivyo kuchanganya haliwezi kua tatizo hii ni kwakua aina zote mbili zina lengo moja la kujenga triceps. Hivyo unaweza ukaanza na Diamond push ups na kumalizia hizo zingine au kinyume chake.
 
poa mkuu ngoja nirushe video
 
sorry nashindwa kuiupload kila nikijaribu inagoma
Log in kupitia browser yako yaani mfano Uc Browser au Opera.
Utakuta kialama cha alerts naamini na alert yangu itakuepo ingia tu hapo utakuta kiicon cha kuattach utatumia hiko hiko kuchukua video na kuiweka humu.
 
kama hizo kwenye video
 
Attachments

mkuu tayari nimeweka video
 
kama hizo kwenye video
Mkuu nimeona.
Ni mara yangu ya kwanza kuziona push ups za hivi itabidi niibe ujuzi hapa.

Ila ni kama nilivyosema, kua kwa maoni yangu kufanya mazoezi mawili au hata kumi tofauti lakini yanatengeneza kitu kile kile siyo vibaya.
Cha msingi ni kupangilia zoezi lipi lianze na lipi lifuatie.
 
Notifications za jf ni jipu
 
poa mkuu
 
Shukran mkuu nitayafanyia kazi maoni yako.
 
Day 1- Nikaanza push ups kwa kupiga reps 10 raundi 4. Hiyo ni baada ya push ups zingine. Sina mkao mzuri nashindwa kuviweka viwiko chini.

Day 2- Nimepanda reps 12 kwa raundi 4. Bado mkao unanisumbua.

Day 3- Naamua kuweka miguu juu kama video ilivyoonesha. Viwiko vinagusa kama inavyotakiwa, naendelea na reps 12 kwa raundi 4.

Day 4- Naendelea kuweka miguu juu. Napanda reps, 15 kwa raundi 4.

Day 5- Narudia kuweka miguu chini kwa raundi 4 za reps 15 na raundi 4 za miguu juu reps 15.

Ni workout nzuri, inatia pressure kwenye triceps binafsi naona ni nusu ya kufanya skull crushers kwa mwili wako.

Narecommend mtu anayetaka triceps afanye.
 
Pamoja mkuu.
somo zuri aisee nimeanza juzi hili zoezi hapa nilipo mikono hainyooki, na nikiinyoosha ni maumivu sijapata ona. Naomba uniambie nitumie dawa gani coz hii ni baraaa nashindwa fanya kazi nyingine.
 
somo zuri aisee nimeanza juzi hili zoezi hapa nilipo mikono hainyooki, na nikiinyoosha ni maumivu sijapata ona. Naomba uniambie nitumie dawa gani coz hii ni baraaa nashindwa fanya kazi nyingine.
Hiyo kitu haiihitaji dawa mkuu, badala yake unatakiwa kuendelea na zoezi lako kama kawaida.

Kama unashindwa kwenda raundi ulizoenda mwanzo, punguza raundi na reps baadaye unakua sawa.

Ili kuepuka strain kua kubwa usifanye zoezi la aina moja kila siku.
 
Nimekusoma mkuu ntafanya hivyo, kitu kingine mkono wa kishoto unakuwa weak sana je nnaweza fanya mazoezi kwa tofauti ya reps kati ya kushoto na kulia.
 
Nimekusoma mkuu ntafanya hivyo, kitu kingine mkono wa kishoto unakuwa weak sana je nnaweza fanya mazoezi kwa tofauti ya reps kati ya kushoto na kulia.
Sishauri hilo kufanya hivyo kutapelekea kusiwe na makuzi yanayowiana.
Kama unaona mkono unakua na udhaifu hivyo basi fanya zoezi kwa uzito wa kawaida (light weight).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…