Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Nikiri wazi kuwa Tangia nimepata fahamu vyema mpaka hapa nilipofika sijawahi kushuhudia Tetemeko kali la Ardhi kama nililoshuhudia usiku huu wa manane. Ni Tetemeko kali,,kubwa na la ajabu sanaa kuwahi kushuhudia.limetetemesha na kuitikisa nyumba mpaka nikaona mlango unafunguka wenyewe.
Nyumba ,milango , madirisha yalikuwa yanatemeka na kupiga kelele utafikiri nyumba inataka kwenda chini na madirisha na milango inataka kung'oka. Hakuna usingizi uliosalia na kila jirani niliyempigia simu ilipokelewa kwa haraka sana kuashiria kuwa watu walikuwa tayari wapo macho na wengi wameamshwa na tetemeko hilo la maajabu na kubwa kuwahi shuhudiwa ukanda huu.
Nikiri wazi nimeishi mkoa wa Rukwa ambako kuna bonde la Ufa limepita pamoja na mikoa ya ,Mbeya na Songwe lakini hili la leo ni kiboko ni hatari ni la kuogofya kwelikweli ndugu zangu.
Mungu atusaidie sana na majanga ya aina hii.Nilikuwaga nasoma habari za matetemeko kwenye Physical Geography yaani Geography 1,kidato cha tano na Sita na kuendelea huko juu,ila leo kwa Vitendo ndio sasa nimeliona na kushuhudia kwa macho na masikio yangu kile nilichokuwa nakisoma darasani.
Nimejaribu kumpigia wa mbali kidogo ndani ya wilaya ya Mbozi naye kapokea simu haraka sana na kusema kuwa nako limepiga na kwamba walikuwa wanaangalia kama tofali zitaanza kuanguka.
Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Pia soma:
- Tetemeko la ardhi 14:57Hrs lapita mkoani Tabora
- Tetemeko dogo la ardhi limepita Moshi majira ya saa 7:21 mchana
- Tetemeko dogo la ardhi limepita Moshi majira ya saa 7:21 mchana
- Morogoro: Tetemeko la Ardhi limepita kati ya saa 12:31 - 12:32 mchana
- Tetemeko dogo la ardhi limepita Moshi majira ya saa 7:21 mchana
- Tetemeko la Ardhi latokea baadhi ya Mikoa ya Tanzania
- Tetemeko la ardhi la takribani sekunde Moja limepita mkoani Arusha na Manyara
- Tetemeko la ardhi latokea Dodoma, Singida
- Morogoro: Tetemeko la Ardhi limepita kati ya saa 12:31 - 12:32 mchana
- Tetemeko la Ardhi Kintinku
- China: Tetemeko la Ardhi laua Watu 116
- Afghanistan yakumbwa na tetemeko la ardhi la tatu ndani ya wiki moja
- Mikoa 11 iliyoko hatarini kukumbwa na Tetemeko la Ardhi
- Tetemeko la ardhi latokea Dodoma, Singida
- TMA: Uwepo wa kimbunga “Hidaya” katika bahari ya Hindi Mashariki mwa Pwani ya Mtwara
- Serikali: Watu 33 Wamefariki Kutokana na Mafuriko na Mvua Kubwa katika Mikoa ya Morogoro na Pwani