Tetemeko kali la Ardhi latikisa Mkoa wa Songwe

Tetemeko kali la Ardhi latikisa Mkoa wa Songwe

Lucas pole sana nafurahi kuona umetoka salama

Ila kumbe we kichwa advance ulisoma PGM!🤸
 
Laitinmngejua huyo bibi anachowafanyia, 2030 mtajuta kulitaja hilo jina.
 
Wewe ni kijana ambae huna akili, embu jitafakari mkuu au tukuongezee akili bandia
 
Wewe ni kijana mjinga sana!

Tetemeko na hiyo aya ya mwisho vina uhusiano gani??
 
Usilete utani kwenye Tetemeko

Wewe ndiye unaleta utani na kuifanya habari nzima ionekane ni upuuzi. Sasa huyo mama anahusika nini na hilo tetemeko? Ndiye aliyekuletea tetemeko au ndiye aliyelizuia lisikuletee madhara? Kweli uchawa huondoa akili. Yawezekana hata ukijikwaa huwa unamshukuru mama na kumwambia kazi iendelee!! Unamdhihaki huyo mama na kumkufuru Mungu pia.
 
View attachment 3005379

Ndugu zangu Watanzania,

Nikiri wazi kuwa Tangia nimepata fahamu vyema mpaka hapa nilipofika sijawahi kushuhudia Tetemeko kali la Ardhi kama nililoshuhudia usiku huu wa manane. Ni Tetemeko kali,,kubwa na la ajabu sanaa kuwahi kushuhudia.limetetemesha na kuitikisa nyumba mpaka nikaona mlango unafunguka wenyewe.

Nyumba ,milango , madirisha yalikuwa yanatemeka na kupiga kelele utafikiri nyumba inataka kwenda chini na madirisha na milango inataka kung'oka. Hakuna usingizi uliosalia na kila jirani niliyempigia simu ilipokelewa kwa haraka sana kuashiria kuwa watu walikuwa tayari wapo macho na wengi wameamshwa na tetemeko hilo la maajabu na kubwa kuwahi shuhudiwa ukanda huu.

Nikiri wazi nimeishi mkoa wa Rukwa ambako kuna bonde la Ufa limepita pamoja na mikoa ya ,Mbeya na Songwe lakini hili la leo ni kiboko ni hatari ni la kuogofya kwelikweli ndugu zangu.

Mungu atusaidie sana na majanga ya aina hii.Nilikuwaga nasoma habari za matetemeko kwenye Physical Geography yaani Geography 1,kidato cha tano na Sita na kuendelea huko juu,ila leo kwa Vitendo ndio sasa nimeliona na kushuhudia kwa macho na masikio yangu kile nilichokuwa nakisoma darasani.

Nimejaribu kumpigia wa mbali kidogo ndani ya wilaya ya Mbozi naye kapokea simu haraka sana na kusema kuwa nako limepiga na kwamba walikuwa wanaangalia kama tofali zitaanza kuanguka.

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Tumshukuru Mungu ,Watanzania wabubujikwa na machozi kusikia kama upo salama na tetemeko limepita bila kuacha madhara ila siku nyingine kumbuka kuchukua kavideo kadogo au kurekodi sauti wasikie milango iliyofungwa kwa kufuli ikijifungua!
 
Kama hakuna maafa yaliyotokea,ni jambo la kumshukuru Mungu kwa kuwaepusha na janga hilo.
 
Usilete utani kwenye Tetemeko
Wewe ndio unaleta utani, tetemeko la ukubwa wa Ritcher scale 4.5 ndio unaliita Tetemeko kali sana?!.
Acha propaganda zako kwa kila jambo, hilo ni tetemeko dogo la kawaida tu, acha uoga!!.
 
Back
Top Bottom