Tetemeko kubwa lazikumba Uturuki na Syria. Watu zaidi ya 36,257 Wafariki Dunia

Tetemeko kubwa lazikumba Uturuki na Syria. Watu zaidi ya 36,257 Wafariki Dunia

Marekani walikufa 3000 mpaka leo tunakumbuka hivi waarabu ni watu?
 
Vifo vimefika 43,000
Aisee
unajua sometimes unaona kama Maajabu.. mana huko ni kufutwa juu ya uso wa dunia watu 43 elfu ni wengi jamani..

ila nashangaa wale wadangaji bado wanadanga sasa tetemeko liko wapi nao wako wapi
 
Aisee
unajua sometimes unaona kama Maajabu.. mana huko ni kufutwa juu ya uso wa dunia watu 43 elfu ni wengi jamani..

ila nashangaa wale wadangaji bado wanadanga sasa tetemeko liko wapi nao wako wapi
Tetemeko limetokea mbali kidogo zaidi ya KM 100 kutoka Instanbul

Ila litatikisa uchumi wa Turkey utaendelea dondoka sana
 
Mwanamke 1aokolewa akiwa hai, baada ya kufunikwa kwa masaa 258 au siku 10 na Masaa 18
 
UPDATE, FEBRUARY 13: VIFO VYA #TURKEYEARTHQUAKE VYAFIKIA 36,257

Vikosi vinaendelea kuokoa walionusurika kwenye Vifusi vya majengo yaliyoangushwa na Matetemeko mawili ya ukubwa wa Richa 7.8 na 7.6 wakiwemo Watoto 2 wa miaka 10 na 13 waliotolewa kwenye Kifusi baada ya kusubiri kwa saa 183.

Hadi kufikia leo Februari 13, 2023, Mamlaka na Idara za Uokoaji zimeripoti kuwa Idadi ya waliofariki Nchini Syria ni watu 4,614 wakati vifo kwa upande wa Uturuki vimefikia 31,643.

Nchi hizo zilikumbwa na Matetemeko mawili siku ya Jumatatu Februari 6, 2023 kwa nyakati tofauti na kuharibu miundobinu ikiwa ni pamoja Majengo, Barabara na Mawasiliano.

Takriban Saa 100, baada ya matetemeko makubwa ya ardhi kuzikumba nchi za Syria na Turkey, zaidi ya vifo 21,000 vimerekodiwa huku vikosi vya Uokoaji ambavyo bado vinaendelea kufukua vifusi vimeweka wazi kuwa matumaini ya kuwapata manusra yanafifia
Vile vile hali ya baridi kali inatajwa kutishia maisha ya Maelfu ya walionusurika ambao sasa hawana Maazi, Maji na Chakula

Hapo awali, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilikadiria kuwa Idadi ya Vifo inaweza kufikia 20,000, hivi sasa limeeleza ni vigumu kujua madhara halisi ya tetemeko hilo


UPDATE: VIFO VYA TETEMEKO VYAFIKIA ZAIDI YA 17,000

Takriban watu 14,000 wamefariki Nchini Turkey, huku 3,162 wakifariki Nchini Syria kutokana na matetemeko mawili ya ardhi yaliyozikumba nchi hizo Februari 6, 2023

Hadi sasa zaidi ya raia 28,000 wa Uturuki wanaripotiwa kuhamishwa kutoka eneo la Kahramanmaras, lililoathiriwa kwa kiasi kikubwa na tetemeko hilo


UPDATE: VIFO VYA TURKEY EARTH QUAKE VYAFIKIA ZAIDI YA 15,000

Madhara ya Matetemeko mawili yenye kipimo cha Richa 7.8 na 7.6 yanazidi kuongezeka kadri muda unavyosogea ambapo hadi hivi sasa Turkey imerekodi zaidi ya vifo 12,300 na Syria takriban vifo 2,900

Wakati juhudi za uokoaji zikiendelea, mamia ya familia yanatajwa kuwa bado yamefukiwa na vifusi


UPDATE: VIFO VYA TURKEY EARTH QUAKE VYAFIKIA ZAIDI YA 11,200

Maafisa wa Uturuki wanasema watu 8,574 wamefariki nchini humo huku idadi ya vifo vilivyothibitishwa nchini Syria hadi sasa ni 2,662

Aidha, kufuatia malalamiko kuwa Mamlaka za Turkey zilichelewa kufika katika baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa, Rais Recep Tayyip Erdogan amesema kuwa Serikali inashughulikia miundombinu ya ndege na barabara, ili kurahisisha jitihada za uokozi


UPDATE: VIFO VYA TETEMEKO VYAZIDI 8,700

Kwa mujibu wa Shirika la Maafa nchini Turkey, idadi ya Vifo imeongezeka hadi 6,234, huku takriban watu 37,011 wakijeruhiwa

Vyombo vya Habari vya Serikali nchini Syria vimesema takriban watu 2,500 wameuawa huku idadi ya majeruhi ikishindikana kujulikana mara moja

Vikosi vya Uokoaji vinazidi kutafuta manusura waliofukiwa na vifusi, Kusini mwa Turkiyë na Kaskazini mwa Syria baada ya matetemeko makubwa mawili ya ardhi kuyakumba maeneo hayo Februari 06, 2023

Huku jitihada za uokoaji zikiendelea, mamlaka zimeonya kuwa idadi ya vifo inaendelea kuongezeka kutokana na kusuasua kwa zoezi la uokoaji, linaloathiriwa na baridi kali pamoja na uharibifu mkubwa wa Miundombinu
Tetemeko kubwa la ardhi la kipimo cha 7.9 limepiga katikati mwa Uturuki na Kaskazini-Magharibi mwa Syria siku ya Jumatatu, na kuua maelfu ya watu na kujeruhi mamia wakati majengo yakiporomoka


Uokoaji wa walionusurika kwenye vifusi katika eneo hilo lenye theluji unaendelea.

Shirika la maafa la Uturuki limesema watu 76 wameuawa, na 440 wamejeruhiwa, wakati mamlaka ilipotawanya timu za uokoaji na kusambaza ndege katika eneo karibu na mji wa Kahramanmaras, huku ikitangaza "kiwango cha 4 ya uokoaji" inayotaka usaidizi wa kimataifa.

Vyombo vya habari vya serikali ya Syria vimesema kuwa idadi kubwa ya majengo yameporomoka katika jimbo la Aleppo, huku chanzo cha habari katika utumishi wa umma cha Hama kikisema kuwa majengo pia yameporomoka huko.

UPDATES
Vifo zaidi ya 100 upande wa Uturuki, 39 Upande wa Syria huku watu wengi wakiwa bado chini ya vifusi.

Italia yaonya kuwa tsunami yaweza tokea kutokana na tetemeko hilo

UPDATE: WALIOFARIKI KWA TETEMEKO LA ARDHI UTURUKI NA SYRIA WAFIKIA 1500

Wakati shughuli za Uokoaji zikiendelea baada ya kutokea Tetemeko lenye kipimo cha Richa 7.8, zoezi hilo linaanza kukabiliwa na ugumu kutokana na Mamia ya Watu kunaswa kwenye vifusi

Zaidi ya watu 5000 wamejeruhiwa na wengine bado hawajulikani walipo na wana hali gani. Nchi za Cyprus, Misri na maeneo ya Lebanon yamepata Mtikisiko kutokana na Tetemeko hilo.

---

UPDATE: IDADI YA WALIOFARIKI KWA TETEMEKO LA ARDHI UTURUKI YAFIKIA WATU 1,800

Vifo zaidi vinazidi kuripotiwa kufuatia Tetemeko la ukubwa wa Richa 7.8 kuzipiga Uturuki na Syria usiku wa kuamkia Februari 6, 2023 na kuporomosha mamia ya Majengo wakati watu wakiwa wamelala

Idara ya Dharula Nchini Uturuki imeomba msaada kwa Jumuiya za Kimataifa baada ya kutokea Matetemeko mengine mawili yenye kipimo cha 7.5. Uingereza tayari imetuma Wataalamu 76 wa Utafutaji na Uokoaji.

UPDATE: Zaidi ya watu 2,300 wamepoteza maisha huku waokoaji wakiendelea kutafuta manusura

Zaidi ya watu 2,300 wamepoteza maisha huku waokoaji wakiendelea kutafuta manusura kutoka chini ya vifusi vya majengo yaliyoporomoka kutokana na Tetemeko kubwa la ardhi lililozikumba Uturuki na Syria leo Februari 6, 2023 na kuacha majeruhi zaidi ya 10,000 na wengine wakiwa hawana makazi.


UPDATE: Staa wa zamani wa Chelsea Christian Atsu akwama kwenye kifusi
Staa wa zamani wa Chelsea na Newcastle za England Christian Atsu (31) Raia wa Ghana ambaye kwa sasa anacheza Hatayspor ya Uturuki amekwama kwenye kifusi cha jengo lililoanguka baada ya tetemeko la ardhi.

Harakati za kumuokoa Atsu zinaendelea lakini kwenye tetemeko hilo lililotokea leo nchini Uturuki mitandao mbalimbali imeripoti kuwa watu zaidi ya 1400 wamefariki Dunia.

Atsu ambaye alijiunga na Chelsea 2013 na kuishia kutolewa kwa mkopo Newcastle na Everton, alikuwa sehemu ya mchezo wa Ligi Kuu Uturuki jana kati ya timu yake ya Hatayspor dhidi ya Kasimpasa ambapo aliisaidia kupata ushindi wa 1-0 akifunga goli dakika ya 90+


UPDATE: Matetemeko mengi madogo 100 yatokea baada ya lile kubwa

Takriban matetemeko 100 yenye ukubwa wa 4.0 au zaidi yametokea tangu tetemeko la ardhi lenye kipimo cha 7.8 lilipotokea Kusini mwa Uturuki Jumatatu asubuhi saa za huko, kulingana na Utafiti wa Jiolojia wa Kituo cha Marekani.

Kadiri muda kutoka kwa tetemeko la ardhi la asili unavyoongezeka, frequency na ukubwa wa matetemeko ya baadaye hupungua.

Hata hivyo, matetemeko ya kipimo cha 5.0 hadi 6.0 bado inaweza kutokea nchini humo na kuleta hatari ya uharibifu zaidi. Hii inaleta tishio kwa zoezi la uokozi linaloendelea na kwa timu za uokoaji na manusura.


UPDATE: WALIOFARIKI KWA TETEMEKO LA ARDHI UTURUKI, SYRIA NI ZAIDI YA WATU 4,300

Ripoti za idadi ya waliofariki inaendelea kuongezeka kufuatia Tetemeko la Ardhi la ukubwa wa 7.8 kwa kipimo cha Richa, kuzipiga Uturuki na Syria usiku wa kuamkia Februari 6, 2023.

Watu 2,921 wameripotiwa kufariki Nchini Uturuki huku zaidi ya 15,000 wakijeruhiwa, upande wa Syria imeripotiwa waliofariki ni watu 1,444; ikifanya jumla ya vifo kufikia 4,365, inaelezwa idadi inatarajiwa kuongezeka.

Rais wa Korea Kusini, Yoon Suk-yeol amesema Nchi yake itatuma timu ya waokoaji na vifaa vya matibabu ya dharura Nchini Uturuki ili kusaidia uokoaji unaoendelea.


UPDATE: VIFO VYAFIKIA 8,700

Kwa mujibu wa Shirika la Maafa Nchini Turkey, idadi ya Vifo imefikia 6,234, huku takriban Watu 37,011 wakijeruhiwa

Vyombo vya Habari vya Serikali Nchini Syria vimesema takriban Watu 2,500 wameuawa huku idadi ya Majeruhi ikishindikana kujulikana mara moja.

UPDATE: VIFO VYA #TURKEYEARTHQUAKE VYAFIKIA ZAIDI YA 11,200

Maafisa wa Uturuki wanasema Watu 8,574 wamefariki Nchini humo huku idadi ya vifo vilivyothibitishwa Nchini #Syria hadi sasa ni 2,662

Rais wa #Turkey, Recep Tayyip Erdogan, amesema Serikali inashughulikia Miundombinu ya Ndege na Barabara, ili kurahisisha jitihada za uokozi.

Tetemeko lingine limetokea leo, 1 hour ago.. lenye 6.4 magnitude
 
Inasikitisha, nimechek Aljazeera watu wanahofu na maisha yao wamekaa nje tu.
 
Inasikitisha, nimechek Aljazeera watu wanahofu na maisha yao wamekaa nje tu.
kuna mambo hata ukiyatafakari unakosa majibu ya wahanga..
wanajiskiaje saizi wanaishi kwa mashaka maisha yamegeuzwa juu chini ndani ya wiki2 uhai wao umekua kama mawindo
 
Tetemeko la Sichuan China mwaka 2008. Lile la Sumatra mwaka 2004. Kashmir mwaka 2005.

Kumbe ulikuwa unazungumzia kuanzia 2010 na kuendelea? Ungebainisha basi. Mimi nilikuwa hasa naijibu comment hii hapa ya David Harvey
China ina matetemeko mengi makubwa zaidi na wahanga wengi zaidi
 
Hatari sana Mungu atunusuru nawaza ikitokea kariakoo hatoki mtu
Halafu kwa Afrika tanzania imo kwenye nchi zenye hatari ya matetemeko. Ila bahati yetu ni kwamba matetemeko yetu mara nyingi sio makubwa kwa sababu sisi yanasababishwa na miamba ya plate ya bara ya Afrika inaachana, yani bonde la ufa lile, lina achana, tofauti na huko kwengine, miamba inakutana haiachiani matetemeko yao ni makubwa zaidi
 
Back
Top Bottom