Dalton Elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 968
- 1,978
Zaidi ya watu 20 wamefariki dunia baada ya tetemeko la ardhi la kipimo cha 6.0 kupiga mashariki mwa Afghanistan, karibu na mpaka wake na Pakistan.
Zaidi ya watu 115 waliojeruhiwa wamepelekwa hospitali katika majimbo ya Nangarhar na Kunar, maafisa walisema.
Tetemeko hilo la kina kirefu cha kilomita 8 (maili 5), lilitokea saa 23:47 saa za eneo (19:17 GMT) siku ya Jumapili, kulingana na Utafiti wa Jiolojia wa Marekani.
Tangu wakati huo, kumetokea takriban mitetemeko mitatu baadaye - yenye ukubwa wa kuanzia 4.5 na 5.2.
Kwa sekunde kadhaa tetemeko hilo lilitikisa katika mji mkuu wa Afghanistan Kabul, karibu kilomita 200 na mji mkuu wa Pakistan Islamabad karibu kilomita 400, AFP iliripoti.
Kitovu cha tetemeko la ardhi kilikuwa umbali wa kilomita 27 kutoka Jalalabad, mji mkuu wa mkoa wa Nangarhar na mji wa tano kwa ukubwa nchini Afghanistan.
Tetemeko hilo limetokea baada ya jimbo la Nangarhar kukumbwa na mafuriko kati ya Ijumaa na Jumamosi, ambayo yaliharibu mali na kuua watu watano, kulingana na mamlaka.