Tetesi: Azam Tv kutoonyesha La liga msimu huu

Tetesi: Azam Tv kutoonyesha La liga msimu huu

Kumekuwa na uvumi kuwa kampuni ya Azam Tv wameamua kutokuongeza tena mkataba wake wa kuonyesha ligi kuu ya Uhispania, maarufu kama La Liga. Hivyo kufanya chaneli yao ya Azam Sports HD iliyokuwa ikitumika kurusha matangazo ya mechi za Laliga kujikita zaidi kuonyesha ligi ya VPL.

Inadaiwa hasara imekuwa kubwa, matangazo wanayanunua kwa bei kubwa sana, huku wakiuza kwa bei rahisi kwa wateja wao.

Hizi bado ni fununu hazijathibitishwa, ila ikiwa ni kweli, nawaona Dstv wakizidi kutunyonya kwani lazma watapandisha chaneli yao ya michezo ya Laliga kwenye vifurushi vya juu!

Ngoja tuone Azamtv wakithibitisha ukweli wa tetesi hizi!
Afadhali
 
Hiyo la liga tu wapate hasara, ndio wathubutu kwenye epl?!!! Kwa hivi vifurushi vya 18,000-28,000?!!kwanza hiyo haki tu kuipata ni balaa!! Kama unakumbuka kampuni ya G-TV, walikuwa wana bei ya 46,000,mbona hata msimu haukuisha wakachemka,??? Sio rahisi ki hivyo.
EPL pale n mawe hatari
FA hawanaga huruma kabsa
 
Back
Top Bottom