Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Yapi hayo fanya kazi kaka. Soma na maandiko matakatifu wekeza maana hata kale kadogo kana manufaa. Tatizo letu ni kuwekeza kwenye vimwana kaka huko hakuna faida ndugu yangu. wenzenu wakiinuka mnadai mafisadi, mtaishia maneno tu badala ya kufanya kazi za maendeleo
Fausta,
Nilikwishasoma maandiko matakatifu siku nyingi sana mpaka nikawa na idea ya kuishi Cyber Village baada ya kuona siwezi kuingia katika mfumo.
Pili wewe hunifahamu mimi kama ni mtu wa aina gani lakini nakuhakikishia kwamba mimi ni mtu mwenye heshima zangu na ninaheshimiwa kwa ujuzi na maarifa yangu na kipato huku Cyber Village hakinipigi chenga, kwani ninakipata kihalali kwa utaalam wangu. Usione nimesema occupation hio ukadhani ninakudhihaki.
Nikutanie kidogo, siku moja nilijiuliza hivi huku Cyber Village siwezi kuokota hata senti ishirini tu? Lakini ukifanza kazi kwa bidii basi unakuwa "rewarded".
Lakini hawa watu achana nao kabisa wameendelea na nina wazo la kuwashauri wana JF wote tujenge Cyber Village yetu Tanzania na iwe na kila kitu tunachohitaji.
Mimi napenda majadiliano yenye kujenga na sio kubomoa, wewe hupangi hoja unakuja nazo zikiwa hazijakamilika, lakini karibu hapa jamvini hiki na usije ukalidharau kabisa.
NB:
Halafu nani amekupa wazo kwamba sisi ni wawekezaji kwenye vimwana?